Saturday, September 07, 2013

PICHA ZAIDI ZA MATUKIO YA VURUGU ZA JUZI BUNGENI...!!!



IMG_0073IMG_0104

DAZ BABA ACHANGANYIKIWA NA KUWA KICHAA....WADAU WASEMA NI BANGI NA MADAWA YA KULEVYA


Habari kutoka kwa chanzo cha uhakika zinadai kuwa msanii wa zamani wa kundi Daz Nundaz na hitmaker wa ‘Figure Namba 8′ Daz Baba amechanganyikiwa kutokana na hivi karibuni kuonekana akifanya vitendo ambavyo havilingani na mtu mwenye akili timamu.

Chanzo hicho kimesema Daz alionekana maeneo ya Morogoro akiwa katika hali iliyowatia mashaka ndugu, mashabiki wa muziki pamoja na wasanii wenzake.

Rafiki wa karibu na Daz Baba amemwambia  mwandishi wetu  jana akiwa mkoani Morogoro kuwa hali ya msanii huyo ni mbaya na ana dalili zote za mtu ambaye  ni  Kichaa na amekuwa mtu wakuzunguka barabarani huku akifanya matukio ya ajabu.

MSIKITI WATEKETEA KWA MOTO MJINI DODOMA....MOTO WA JIKO WADAIWA KUWA CHANZO...!!!

Msikiti mkubwa wa barabara ya saba mjini Dodoma  umewaka  moto  mchana  huu  ikiwa  ni  muda  mfupi  baada  ya  swala  ya  mchana  kumalizika....

Akiongea  kwa  njia  ya  simu  na  Mwandishi wetu, mmoja  wa  mashuhuda  walioshuhudia  tukio  hilo  amedai  kuwa  chanzo  cha  moto  huo  ni  moto wa  JIKO  la  wakazi  wa    ghorofa ya  juu  ya  jengo  la  msikiti  huo...

Kwa  mujibu  wa  shuhuda  huyo, moto  huo  umefanikiwa  kudhibitiwa  na  jeshi  la  zima  moto  na  kwamba  hakuna  mtu  aliyepoteza  maisha  kutokana  na  
moto  huo.
Picha ya maktaba:

Friday, September 06, 2013

RAIS KIKWETE NA KAGAME WAMALIZA TOFAUTI ZAO NA KUKUBALIANA KUSHIRIKIANA KAMA ZAMANI


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Alhamisi, Septemba 5, 2013, amekutana kwa faragha na Rais wa Rwanda, Mheshimiwa Paul Kagame katika mazungumzo yaliyokwenda vizuri na kuwaridhisha viongozi hao wawili wa nchi jirani. 
 
Viongozi hao wamekutana kwa zaidi kidogo ya saa moja katika mkutano uliofanyika kwenye Hoteli ya Munyonyo Commonwealth Resort, nje kidogo ya mji wa Kampala, Uganda.
Katika mazungumzo hayo, Rais Kikwete na Rais Kagame wamekubaliana kuendelea kushirikiana katika kujenga uhusiano mzuri na wa kihistoria uliopo kati ya nchi hizo mbili.

MAGAZETI YA LEO IJUMAA SEPTEMBA 06, 2013

DSC 0038 e6e54
DSC 0039 38cfe

GHASIA KUBWA ZALIPUKA BUNGENI KUPINGA MUSWADA.....!!!

vurugusugu_dd67c.jpg
Jana, Bingwa wa Dunia wa uzani wa kati (super middle), unaotambuliwa na Shirikisho la Ngumi Duniani (WBF), Francis Cheka alitembelea Bunge baada ya kutwaa taji hilo karibuni na jana hiyohiyo, Bunge hilo lilishuhudia ngumi kavukavu katika vurugu kubwa pengine kuliko zote zilizowahi kutokea katika ukumbi wake.Katika masumbwi hayo yasiyo rasmi, Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi 'Sugu' anadaiwa kumpiga kichwa Askari wa Bunge na kumchania sare na kung'oa kipaza sauti.
Mbilinyi jana alisema alikuwa anatafutwa na polisi huku akisema hilo limemshangaza akidai kwamba yeye ndiye aliyeshambuliwa na askari huyo.
Vurugu hizo zilitokea baada ya Naibu Spika, Job Ndugai kuamuru kutolewa nje kwa Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe.
Katika vurugu hizo Mbilinyi alibebwa juujuu na polisi hadi nje ya ukumbi huku akiwa hana viatu.
Pamoja na tafrani hiyo, Ndugai alisema wakati akihitimisha kikao cha Bunge kipindi cha asubuhi kuwa amewasamehe wabunge wote waliohusika na kosa hilo la utovu wa nidhamu na kuwaruhusu kurejea kipindi cha jioni kuendelea na Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba. Hata hivyo, wabunge wote CUF, NCCR-Mageuzi na Chadema ambao baada ya tukio hilo walitoka nje ya ukumbi, hawakurejea na baadaye walitoa msimamo wa pamoja wakisema hawatashiriki katika mjadala huo.

BAADA YA DAYNA, BABA LEVO NAE AFUNGUKA NA KUDAI KUIBIWA KORASI YA WIMBO MPYA WA DIAMOND "MY NUMBER ONE"...!!!

https://fbcdn-sphotos-a-a.akamaihd.net/hphotos-ak-prn2/q83/1185392_659474667396477_477324071_n.jpg
NARUDIA tena nina asilimia 100 DAIMOND PLATNUM amecopy KORAS yangu coz nimekuwa nikimuimbia kila tunapokutana kwa lengo la kumshirikisha kwenye wimbo wangu (SWEATY SWEATY) ni zaidi ya miezi saba au nane imepita akinizungusha tu.
Na kwa kudhibitisha Hilo mimi nina DEMO 5 za KORASI yangu ambazo nimefanya kwenye studio mbali mbali Ya kwanza 1 kwa MORE FIRE magomeni 2 STUDIO SINZA 3 kwa TUDY THOMAS mbezi 4 kwa G BAKUZA KIGOMA 5 kwa MR T TOUCH mwenge... 
Ninaweza kuwasikilizisha watu demo zote Tano lakini sio kuuachia huo wimbo coz ntaonekana walewale wategemea KICK. wakati MIMI KWA SASA sihitaji kick ya mtu coz msimu huu nina nguvu ya kutosha. na nina jiamini.. ukitaka kuamini angalia kilichotokea FIESTA MTWARA JUZI..

MAWAZIRI WATEJA WA MACHANGUDOA WATAJWA.......!!!



BAADHI ya Mawaziri na askari polisi wametajwa kuwa ni wateja wakubwa wa wanawake wanaouza miili yao(Machangudoa).

Hayo yameelezwa na jukwaa la wanaharakati wanawake vijana (YFF), walipokuwa wakiwasilisha ujumbe wao kwa njia ya sanaa ya ngonjera, katika tamasha la 11 la Mtandao wa jinsia Tanzania (TGNP) linaloendelea eneo la Mabibo Jijini Dar es Salam.

"TATIZO LA UJENZI HOLELA NI KUBWA JIJINI DAR" SERIKALI

majengo_234e1.jpg
Serikali imekiri kuwa kumekuwa na ukiukwaji wa ujenzi ambao haufuati kanuni, taratibu na sheria zilizopo hususan katika Jiji la Dar es Salaam.
Kauli hiyo ilitolewa jana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Hawa Ghasia ambaye alisema kuwa Serikali imeliona jambo hilo na sasa inapitia sheria upya ili kurekebisha hali hiyo.
Waziri aliyataja maeneo ambayo yanahusika na ukiukwaji ni pamoja na utoaji wa vibali vya ujenzi pamoja na ubadirishwaji wa matumizi ya ardhi na uvamizi wa viwanja vya wazi.
Maeneo mengine ni ukiukwaki wa maadili ya kitaaluma usiozingatia sheria ya mwaka 2007 ya sheria ya mipango miji na kanuni za udhibiti wa ujenzi.

Alikuwa akijibu swali la Muhammed Amour Chombo (Magomeni,CCM) aliyetaka kujua Serikali ina mkakati gani wa kukomesha utovu wa nidhamu dhidi ya waliopewa dhamana ya kusimamia sheria za mipango miji katika kuruhusu ujenzi.

CHEKA ATINGA BUNGENI NA UBINGWA WA WBF



Waziri Mkuu Mh, Mizengo Pinda wanne kushoto akiwa na bingwa wa dunia wa mchezo wa masumbwi nchini Fransic Cheka baada ya kukaribishwa bungeni mjini Dodoma wengine kushoto Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D'  na bingwa wa mabara Fransic Miyeyusho kulia ni promota wa mchezo wa masumbwi nchini Mohamed Bawaziri,  na promota wa mpambano wa ubingwa wa Dunia ambao cheka anao kwa sasa Catherini Matili .

MAJI MAREFU AKIWA NA MABINGWA WA MCHEZO WA MASUMBWI NCHINI

Thursday, September 05, 2013

ANGALIA PICHA ZA RAIS KIKWETE WALIPOKUTANA NA KAGAME HUKO KAMPALA LEO...!!!


Rais Jakaya Kikwete leo amefanya mazungumzo na Rais Paul Kagame wa Rwanda katika mkutano wa saba wa kimataifa wa nchi za maziwa makuu, unaofanyika Kampala, Uganda.
Haijafahamika mara moja walichozungumza, hizi ni picha za mkutano wao.
9676681299_b3707d20a5_c
9676687273_13e1849eb2_b
9679917620_3f83a214d0_b
Marais hao wamekutana wakati ambapo uhusiano kati ya nchi hizo mbili unaendelea kuzorota.

DULLY SYKES AMFANANISHA DIAMOND NA KANUMBA...!!! NI BAADA YA VIDEO MPYA YA DIAMOND KUTOKA

Baada ya kuachia video yake mpya iliyofanywa kwa gharama ya  takribani milioni arobaini na tano za kitanzania, mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya Diamond Platnumz amefananishwa na marehemu Steven kanumba kwa jinsi anavyothubutu kufanya mambo makubwa kukuza Sanaa na kipaji chake tofauti na wasanii wengine wenye majina makubwa nchini.

  Hayo yameongelewa na Msanii dully sykes katika mahojiano yake na mtandao wa Bongo5 hii leo... Katika interview hiyo Dully amemuelezea marehemu kanumba kama ni mtu aliyethubutu kutumia nguvu, hali na mali, kwa ajili tuu ta kukuza jina lake kitu ambacho ni nadra sana kwa wasanii hasa wa Tanzania.
“Kanumba alikuwa ana uwezo wa hata kuchukua nauli yake ya kwenda sehemu kama Ghana kwenye tamasha la movie lakini ilimradi kujitengenezea status yake. Kwahiyo Diamond ni mtu ambaye tayari ameshajitolea kwaajili ya kuutetea muziki wetu.” Alisema Dully sykes

KIZAAZAA CHATOKEA TENA BUNGENI.....WABUNGE WA CHADEMA WATOKA NJE YA BUNGE BAADA YA MBOWE KUAMRIWA KUTOKA NJE...!!!

Wabunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wametoka nje muda huu baada ya Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni ambaye pia ni Mbunge wa Hai, Mhe. Freeman Mbowe kuamriwa atolewe nje na Naibu Spika wa Bunge Job Ndugai. 


Mbowe alisimama ili achangie lakini aliamriwa na Job Ndugai kukaa chini jambo ambalo hakuliafiki na kuendelea kusimama. Baada ya tukio hilo, Ndugai aliwaamuru askari wa bunge kumtoa nje Kiongozi huyo wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni na ndipo mzozo ulipotokea.

Hali hiyo ilitokea wakati wa Majadiliano ya Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Mabadiliko ya Katiba wa mwaka 2013. Mbowe aligoma kutolewa nje ya bunge baada ya askari kufika alipokuwa amekaa kwa lengo la kumtoa nje, ndipo ilipotokea sintofahamu na mzozo mkubwa ndani ya bunge hali iliyopelekea wabunge wote wa Chadema kutoka nje.

Hali kama hii pia ilitokea jana wakati muswada wa marekebisho ya pili ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 83 ukisomwa na kupelekea wabunge wa vyama vya Chadema, CUF na NCCR-Mageuzi kutoka nje wakishinikiza muswada huo usisomwe hadi maoni ya wadau kutoka Zanzibar yapatikane.

MAGAZETI LEO ALHAMISI SEPTEMBA 05, 2013

DSC 0020 2b75e
DSC 0021 88774

ATAFUNWA USO NA MWAJIRI WAKE NYUMBANI


IMG 4471 6ee8f
KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida mkazi wa Kijiji cha Nyabibuye Kakongo katika Wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma, Susuluka (16) anadaiwa kujeruhiwa vibaya usoni na bosi wake, Imani Paulo (36) kwa kung'atwa ng'atwa usoni na kisha kunyofolewa macho, pua na meno kubaki nje, kama ambavyo anaonekana pichani ukurasa wa mbele.

Tukio hilo ambalo tunaweza kulifananisha na dunia kuelekea kufika mwisho, limegusa hisia za watu wengi hasa wakazi wa Kibondo, huku wengine wakitokwa na machozi kutokana na kuguswa na ukatili ambao amefanyiwa kijana huyo.Tunaweza kufikiria kuwa tukio hilo ni sinema, lakini Mkuu wa Wilaya ya Kibondo, Venance Mwamotto, ameliambia Majira kuwa tukio hilo limetokea miezi miwili iliyopita.


Akizungumza na Majira katika mahojiano maalumu, Mwamotto, alisema kuwa kabla ya kijana huyo kujeruhiwa na bosi wake, alimtuma dukani ili akamnunulie soda.Aliliambia Majira kuwa baada ya kufika nyumbani alimkuta bosi wake akiwa amemkaba koo mbwa na kutokana na maumivu aliyokuwa akiyapata mbwa huyo, alianza kuhema akitoa ulimi nje.


DC Mwamotto alisema kuwa mtuhumiwa huyo ghafla alianza kuung'ata ulimi wa mbwa na kisha kumeza vipande jambo lililosababisha mbwa huyo kupiga kelele kutokana na maumivu.Aliongeza kuwa aliendelea kula vipande vya ulimi huo wa mbwa hadi alipoumaliza.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...