Friday, September 06, 2013

MAWAZIRI WATEJA WA MACHANGUDOA WATAJWA.......!!!



BAADHI ya Mawaziri na askari polisi wametajwa kuwa ni wateja wakubwa wa wanawake wanaouza miili yao(Machangudoa).

Hayo yameelezwa na jukwaa la wanaharakati wanawake vijana (YFF), walipokuwa wakiwasilisha ujumbe wao kwa njia ya sanaa ya ngonjera, katika tamasha la 11 la Mtandao wa jinsia Tanzania (TGNP) linaloendelea eneo la Mabibo Jijini Dar es Salam.

Wanaharakati hao wanawake vijana, walisema tatizo lipo kwenye jamii ambayo inawahukumu machangudoa bila kujiuliza kuwa wateja wa machangudoa hao ni akina nani.

‘’…siku yakiwanogea twala chipsi na kuku, jamani hebu tuulizane, kwani changudoa mteja wake nani? Kwa taarifa yako, Mawaziri wamo, wabunge wamo, mapolisi wamo na hii ni changamoto kwa jamii’’ walisema wanaharakati hao.

Akizungumza na wanahabari baada ya kutoka jukwaani, kiongozi wa wanaharakati hao, Aisha Kijavala, amesema wameamua kutoa ujumbe huo kwa washiriki wa tamasha hilo, ili jamii ijue wateja wa machangudoa hao na kwamba pindi wao wakiacha kununua ngono, pia wanawake wanaouza miili yao, wataacha kujiuza.

Tamasha hilo la 11 ndani ya miaka 20 tangu kuanzishwa kwa shirika lisilokuwa la kiserikali la Mtandao wa Jinsia Tanzania(TGNP), linatarajia kuisha kesho Septemba 6, mwaka huu.
Chanzo Kalulunga


No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...