Friday, August 30, 2013

KATIBA YATAKIWA IRUHUSU WAFUNGWA KUSHIRIKI TENDO LA NDOA NA WENZA WAO ILI KUPUNGUZA USAGAJI NA USHOGA GEREZANI

BAADHI ya wadau wa masuala ya jinsia wamependekeza kuwa ili kukabiliana na masuala ya ushoga na usagaji, Katiba Mpya iruhusu wafungwa kukutana kimwili na wenza wao, kwani vitendo hivyo chanzo chake ni gerezani hasa kwa vijana wanaokula 'unga' na kuvuta bangi.




Hayo yalisemwa juzi kwenye kikao cha maboresho ya Rasimu ya Katiba Mpya, kilichofanyika siku tatu kwenye Kijiji cha Makaburini kwa kuratibiwa na asasi ya Tanzania Environment Relatives Organization (TERO) ya mjini Korogwe kwa ufadhili ya Shirika la The Foundation for Civil Society la jijini Dar es Salaam. 

"Mfungwa akubaliwe kukutana kimwili na mume au mke wake. Kitendo cha kuwakatalia wafungwa kukutana kimwili na wake au waume zao kunachochea vitendo vya kufanya mapenzi ya jinsia moja na vijana wengi wameharibikia gerezani na kujikuta vitendo hivyo vinaingia mitaani"

RAIS KIKWETE AMUOMBA RAIS WA UGANDA AONGEE NA KAGAME ILI KUMALIZA UGOMVI ULIOPO


RAIS Jakaya Kikwete, amewasiliana na Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, ili azungumze na Rais wa Rwanda, Paul Kagame kwa nia ya kumaliza mvutano wa maneno kati yao kwa busara.
 
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, alisema hayo jana bungeni, alipokuwa akijibu swali la Kiongozi wa Upinzani bungeni, Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe (Chadema).
 
“Tunataka suala hili limalizike kwa njia ya busara, ili watu waendelee kuchapa kazi, ninaamini busara zitatumika kumaliza tatizo hilo,” alisema.

Akiuliza swali katika kipindi cha maswali ya Papo kwa Hapo kwa Waziri Mkuu jana, Mbowe alitaka kujua kauli ya Serikali na mikakati iliyopo kupata suluhu katika mvutano wa maneno uliojitokeza kati ya Rais Kikwete na Rais Kagame.
 
Pia Mbowe alitaka Serikali kuunda jopo la ushawishi wa kimataifa, kutokana na Rwanda kuonekana kushawishi nchi za Uganda na Kenya, jambo ambalo linaashiria kuitenga Tanzania katika shughuli mbalimbali za Jumuiya ya Afrika Mashariki.
 
Kwa mujibu wa Mbowe, kitendo cha marais wa Kenya, Uganda na Rwanda kukutana katika mikakati ya kuanza kutumia bandari ya Mombasa ambayo ingekuwa ya nchi za Afrika Mashariki, ni dalili kuwa Tanzania imeanza kutengwa.

Thursday, August 29, 2013

SHILOLE: MADEE AU OMMY DIMPOZ..?KILA MMOJA ANASWA NAE CHOBINGO....!!!

STAA wa Muziki wa Mduara, Zuwena Mohammed ‘Shilole’, amewashangaza wasanii wenzake baada ya kunaswa chobingo kwa nyakati tofauti akiwa na wasanii wenzake, Hamad Ally ‘Madee’ na Omari Faraj ‘Ommy Dimpoz’.

 Shilole akiwa na Madee.

Mpango mzima ‘uli-happen’ Agosti 25, mwaka huu ndani ya Ukumbi wa Singida Montel wakati wasanii hao walipokuwa katika shoo ya Serengeti Fiesta 2013 ‘Noma Sana’
Kwanza paparazi wetu alimfotoa Shilole picha kadhaa akiwa anafungwa zipu na Madee.


                                   ...Akiwa na Ommy Dimpoz.
 

BAADA YA KIMYA KIREFU, GK AIBUKA NA NGOMA MPYA

GK (katikati) akiwa na DJ Fetty (kushoto) na msanii Pauline Zongo (kulia) ndani ya Studio za Clouds FM  
 GK akiwa ndani ya Studio za Clouds FM wakati akielezea kuhusu ujio wake.
MSANII mahiri katika anga za muziki wa Bongofleva, Gwamaka Kaihura 'King Crazy GK' leo ameibuka na singo yake mpya iitwayo Baraka au Laana aliyomshirikisha msanii Yuzo. aka sita baada ya kuwa busy na masomo kitendo kilichopelekea kuupa kisogo muziki kwa muda na kuwafanya mashabiki wake kum-mis katika fani hiyo. Memba huyo wa East Coast Team ameachia ngoma yake mpya leo na anataraji kuachia video yake siku ya Ijumaa Agosti 30, mwaka huu. 
GK alisema kuwa amerudi kwenye game kwa nguvu zote na amewashukuru baadhi ya wadau kama Eric Shigongo, Ruge Mutahaba na Joseph Kusaga kwa kumtia hamasa ya kurudi kwa nguvu mpya baada ya kupotea kwa muda.

ETO'O AWASILI LONDON KUFANYIWA VIPIMO NA KUJIUNGA NA CHELSEA

eto c6562
Eto'o akiwasili London (HM)
eto2 85114
Chelsea inakaribia kumsajili mshambuliaji Samuel Eto'o kwa dili la mwaka mmoja lenye thamani ya £7million kwa mkataba wa mwaka mmoja leo Alhamisi baada ya kukiri kushindwa kumpata mshambuliaji wa Manchester United Wayne Rooney.

Eto'o, 32, amekubali kupunguza dau lake alilokuwa akilipwa na Anzhi kiasi cha £17m kwa mwaka na sasa atasaini atasaini akiwa huru.

Pamoja na hilo, lakini inaeleweka kwamba Anzhi wamemlipa Eto'o millioni kadhaa ili kuweza kumuondoa katika listi wachezaji wanaolipwa fedha nyingi ndaniya klabu ya Anzhi.

Eto'o aliwasili jijini London jana usiku na anategemewa kufanyiwa vipimo vya afya mchana wa leo katika uwanja wa mazoezi wa Chelsea Cobham. Chanzo: Shaffihdauda

MAGAZETI YA LEO ALHAMISI AGOSTI 29, 2013

DSC 0106 63caa
DSC 0107 9b33d
DSC 0108 3505d

MAPYA YAIBUKA KUHUSU TRAFIKI FEKI, KUMBE ALIKUWA MFUNGWA ALIYETOROKA JELA.... !!!

MAZITO tena yameibuka kuhusu yule trafiki feki James Hussein, mkazi wa Kimara Matangini, jijini Dar es Salaam ambaye yuko Gereza la Segerea, Dar akikabiliwa na kesi ya kujifanya askari wa usalama barabarani.

Habari za ndani kutoka Gereza la Isanga, Dodoma zinadai kuwa, trafiki huyo ana mambo mengi ya kushangaza ambayo Watanzania wengi hawayajui.

Mtoa habari wetu alisema kuwa, James Hussein si jina halisi la trafiki feki huyo. Alisema jina lake halisi ni Ali Kinanda.

“Yule jamaa anaitwa Ali Kinanda, sisi kumwona kwenye picha gazetini akijiita James Hussein tulishangaa sana,” kilisema chanzo chetu.

Chanzo kikazidi kudai kwamba, kuanzia mwaka 1984 jamaa huyo alikuwa ni askari magereza katika Gereza la Butimba, Mwanza hadi mwaka 1987 alipoacha.

Mtoa habari wetu aliendelea kumwanika trafiki feki huyo kuwa, mwaka 2002 mtuhumiwa huyo alidaiwa kupata msala wa tukio la ujambazi lililotokea Mpwapwa, Dodoma ambapo kesi yake iliunguruma hadi mwaka 2003 ambapo hukumu ilitolewa yeye na wenzake kwenda jela miaka 30.

''OCD' ''KUPIGA PICHA ZA UTUPU NI KOSA KISHERIA SASA OLE WAKO UPIGE HALAFU UKAMATWE CHAMOTO MTAKIONA''



Jeshi la Polisi Kanda ya Kinondoni limetoa kauri nzito kuhusu picha za udhalilishaji zilinazosambazwa na wasanii wetu wa bongo movie zikiwemo za Manaiki Sanga.

Akiongea katika mahojiano maarumu mkuu wa kituo cha Polisi Oysterbay “OCD” Mtafungwa alisema kuwa kimsingi kupiga picha za utupu ni kosa kisheria hivyo endapo muhusika akimatwa atashtakiwa kwa mujibu wa sheria.

Mtafungwa aliendelea kufafanua kuwa” Unajuwa Jeshi la Polisi lipo kwa ajili ya kusimamia sheria iliyowekwa na serikali hivyo huwa kuna namna ya kuwakamata wahusika hasa kama kumetokea malalamiko toka idara flani kuhusiana na matukio yoyote yanayopelekea uvunjifu wa amani au kupotosha maadili” Alisema Kamanda huyo kipenzi cha watu

Aidha Kamanda huyo aliendelea kufafanua “ Pia Jeshi la polisi linamamlaka ya kumkamata mharifu yeyote kwa muda wowote endapo kipindi hicho akikutwa anafanya uharifu ni pamoja na upigaji picha hizo chafu, Lakini kubwa tuhajitaji kumkata mtu na ushahidi ili iwe rahisi kumbana na kumfikisha mbele ya sheria” Alisema

Mtafungwa alimaliza kusema “ Tunaendelea kufatilia kupita mitandao ya kijamii ili kuona hizo picha zikoje halafu tuhaahidi kuwatolea taarifa hadharani kupita kwa msemaji wa Jeshi la Polisi Kanda ya Kinondoni RPC Wambura ambae kisheria ndiye mwenye mamlaka ya kusema” Alisema Mtafungwa

MWIGULU NCHEMBA ATAKA MBOWE NA DR. SLAA WAKAMATWE KWA MAUAJI YA RAIA

 MBUNGE wa Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba (CCM), amechafua hali ya hewa bungeni kwa kuitaka Serikali kuwachukuliwa hatua viongozi wa juu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA). Mbunge huyo alisema mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe pamoja na Katibu Mkuu wake, Dk. Wilbroad Slaa, wanapaswa kuchukuliwa hatua kwa madai ya kusababisha mauaji ya raia.

Mwigulu, ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bara, alisema katika kipindi cha miaka miwili tangu nchi ilipotoka kwenye uchaguzi, viongozi hao wamekuwa wakihamasisha maandamano na kusababisha umwagaji wa damu za Watanzania.

“Mheshimiwa Naibu Spika, katika kipindi cha miaka miwili tangu nchi yetu ilipomaliza Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010, Mbowe na Dk. Slaa wamekuwa wakitoa kauli za wazi na hata kusababisha mauaji ya watu bila hatia.

“Kutokana na hali hii, sijui Serikali inafanya nini katika kuwachukulia hatua, kwani viongozi hawa wamekuwa wakitafuta umaarufu wa kisiasa kwa kuchochea chuki na mauaji dhidi ya raia.

“Kwa hali hiyo, tangu kipindi hicho hadi leo hii wanasubiri nini badala ya kwenda kuwaweka jela, kwani huko ndiko wanatakiwa kuwa,” alisema.

Mwigulu, alisema kukosekana kwa maadili kwa baadhi ya viongozi wa siasa, ambao wamekuwa wakitumia majukwaa na kuhubiri umwagaji damu ni hatari kwa taifa.

Alisema viongozi hao wamekuwa wakitumia majukwaa hayo na kusababisha vifo vya wananchi, huku akitaja vurugu zilizotokea katika mikoa ya Morogoro, Iringa, Arusha na Singida.

Wednesday, August 28, 2013

MAGAZETI YA LEO JUMATANO AUGUST 28, 2013 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

.

.

.

CAG AANIKA TUHUMA ZA UFISADI WA MAGUFULI


MKAGUZI na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh amesema taarifa ya Sh bilioni 252 zilizokuwa zimeoneshwa katika taarifa ya Wizara ya Ujenzi, zilihamishwa kwenda Wakala wa Barabara (Tanroads) kulipia madeni ya wakandarasi na kwamba hapakuwa na ufisadi.  

Kihasibu fedha hizo zilipaswa kuoneshwa kwenye hesabu za mtumiaji halisi wa fedha ambaye ni Tanroads na siyo Wizara hiyo,” alisema Utouh.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Utouh alisema vyombo vya habari viliripoti suala hilo tofauti, baada ya Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) kukutana na wizara na kuhoji juu ya matumizi ya fedha hizo.
 
Utouh alisema baada ya PAC na Kamati ya Kudumu ya Serikali za Mitaa (LAAC) kupitia ripoti ya Wizara ya Ujenzi, kumejitokeza upotoshaji wa taarifa kuhusu hesabu za wizara hiyo na taarifa zisizo sahihi, zikidai kulikuwa na ufisadi.
 
Alisema fedha hizo zimeoneshwa kwenye taarifa ya hesabu za Wizara hiyo, kama vile ni miradi mipya ya mwaka 2011/2012 tofauti na uhalisia wake.

Utouh alisema uhalisia wa fedha hizo ni kuwa mara baada ya kupokewa na Wizara ya Ujenzi kutoka Hazina, zilihamishwa kwenda Tanroads kulipia madeni ya wakandarasi wa miradi ya barabara, iliyotekelezwa na wahandisi washauri, ambao walikuwa hawajalipwa kwenye mwaka wa fedha 2010/2011.
 
“Fedha hizi zilijumuishwa kimakosa kwenye hesabu za Wizara kama matumizi ya akaunti ya maendeleo, hivyo kuongeza matumizi ya Wizara kimakosa kwa kiasi hicho

"WABUNGE WENGI NI WAUZA UNGA NA MADAWA YA KULEVYA"....WILLIAM LUKUVI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi amesema baadhi ya majina ya wabunge yametajwa miongoni mwa watu wanaoshukiwa kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya lakini Serikali haiwezi kuwataja hadharani kwa haraka.
 

Majibu hayo ya Waziri Lukuvi yamekuja baada ya wabunge kumbana na wengine wakizomea baada ya kueleza ugumu wa kutaja majina ya washukiwa pasi na ushahidi wa kutosha.
 

“Serikali haiwezi kutaja majina haraka kiasi hicho kwani inaogopa kukurupuka na kushindwa mahakamani, hivyo lazima tuwe makini sana na jambo hilo. Hatuwezi kukurupuka tu eti ni fulani wakati hatuna vithibitisho.
 

“Kumbukeni wengine mpo humu ndani ya Bunge na tukianza wengi mtakwisha maana katika orodha hiyo kubwa na ninyi mmo na orodha ni kubwa kweli ambayo wakati mwingine inatakiwa umakini wa hali ya juu,” alisema Lukuvi alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Karatu (Chadema), Mchungaji Israel Natse.
 

Katika swali lake ambalo lilisababisha kelele za kuzomea, Natse alitaka majina hayo yatajwe hadharani. Hata hivyo, hali ilitulia baada ya Spika wa Bunge, Anne Makinda kuingilia kati na kusema: “Hii tabia ya zomeazomea siitaki humu ndani, acheni tabia hiyo lazima mumsikilize mtu kwa kile anachokisema kwanza lakini mtindo huu si mzuri...”

KODI YA SIMU BADO KIMBEMBE...!!!


                       Waziri wa Fedha, William Mgimwa

Wakati wananchi wakiwa hawajajua majaliwa yao juu maamuzi ya serikali kuhusu kilio chao dhidi ya kodi ya simu ya Sh. 1,000 kwa mwezi iliyopitishwa na Bunge la Bajeti ya mwaka 2013/14, kuna habari kwamba mzigo huo sasa unaweza kuhamishiwa kwenye ununuaji wa vocha.
Hofu hii inajengeka wakati Mkutano wa Bunge wa 11 ambao unatarajiwa kujadili suala la kodi ya simu ukianza mjini Dodoma huku kukiwa na habari kwamba serikali inatafakari uwezekano wa kupandisha ushuru kwenye vocha (excise duty) kwa asilimia 5.5.
Kama maamuzi hayo yatafikiwa ushuru huo utapaa hadi kufikia asilimia 20 kutoka asilimia 14.5 wa sasa.
Mpango huo wa serikali ni moja ya mikakati yake ya kuziba pengo la kiasi cha Sh. bilioni 178.5 kama kodi ya simu itaondolewa kwani ilikuwa imekadiriwa kuwa ingeingiza mapato ya kiwango hicho kwa mwaka wa fedha wa 2013/14.
 
Kama ushuru huo utaongezwa na kukubaliwa na wabunge, basi Tanzania itakuwa na ushuru mkubwa kwenye simu kuliko viwango vinavyotozwa na nchi zingine za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

ALIYEGEUZWA MTUMWA WA NGONO AANIKA 'UCHAFU' WA KANALI GHADAFI....!!!


Kanali Muammar Gaddafi aliamuru kutekwa kwa wasichana wa shule ambao baadaye walishikiliwa kama watumwa wa ngono kwenye eneo lake, kwa mujibu wa kitabu kuhusiana na dikteta huyo.

Msichana mmoja, aliyetajwa kama Soraya, alitekwa nyara wakati akiwa na umri wa miaka 15 na kushikiliwa kwa miaka mitano katika sehemu ya chini kwenye ngome yake yenye urefu wa maili sita nje kidogo ya mji wa Tripoli.

Anasema alibakwa ovyo-ovyo, kupigwa na kudhalilishwa kwa utaratibu wa takribani kila siku na kushuhudia udhalilishaji unaofanana na huo kwa wasichana na wavulana wengine.

Stori yake na nyingine za wengine ambao wanasema walibakwa na dikteta huyo zinasimuliwa kwenye kitabu cha "Gaddafi's Harem: The Story Of A Young Woman And The Abuses Of Power In Libya" kilichoandikwa na mwandishi wa kimataifa wa Ufaransa Annick Cojean.

Kitabu hicho kimeshauza zaidi ya nakala 100,000 tangu kilipochapishwa nchini Ufaransa mwaka jana na tafsiri ya Kiingereza itakuwa mitaani mwezi ujao.

MADIWANI WALIOTIMULIWA BUKOBA WARUDISHWA


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa imejadili na kutolea maamuzi pamoja na mambo mengine suala la Madiwani wanane waliotangazwa kufukuzwa uanachama na Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Kagera.

Katika maamuzi yake, Kamati Kuu imebatilisha uamuzi uliofanywa na Halmashauri Kuu CCM ya Mkoa wa Kagera Agosti 13, 2013 wa kuwafukuza uanachama Madiwani hao. Hivyo Madiwani hao wanane ni wanachama halali wa CCM.

Kamati Kuu imetoa uamuzi huo, baada ya kubaini kuwa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Kagera haikuzingatia Katiba ya CCM ya 1977 Toleo la 2012 Ibara ya 93 (15). Ibara hiyo inasomeka kuwa moja ya kazi ya Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa ni:-

“Kumwachisha au kumfukuza uongozi kiongozi yeyote ambaye uteuzi wake wa mwisho unafanywa na Halmashauri Kuu ya CCM ya Mkoa, isipokuwa kwa suala la kumvua uanachama au uongozi Diwani lisifanyike hadi Kamati Kuu imearifiwa na kutoa maelekezo”.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...