Monday, February 18, 2013

YULE MAMA ALIYEMLISHA KINYESI MTOTO NA KUMCHOMA NA MOTO AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MAISHA

Wilvina Mkandala (24) akitolewa mahakamani mara tu baada ya kusomewa hukumu ya kifungo cha maisaha 

Baadhi ya wakazi wa majengo alikokuwa anaishi mtuhumiwa wakimsifu hakimu kwa hukumu aliyotoa kwa mtuhumiwa huyo
Mtoto Aneth kabla ya kukatwa kwa mkono wake wa kushoto
Mtoto Aneth mara baada ya kukatwa mkono wa kushoto kwa ujumla mtoto huyu anaendelea vizuri na alishatoka hospitalini

MAHAKAMA ya Wilaya ya Mbeya imemhukumu kifungo cha maisha Wilvina Mkandara(24) kutokana na kesi iliyokuwa inamkabili ya kumtesa hadi kumsababishia ulemavu mtoto wa shemeji yake.
Akisoma hukumu hiyo Hakimu mkazi wa mahakama hiyo Gilbert Ndeuruo alisema mshakiwa amehukumiwa kutokana na kifungu cha 235 cha mwenendo wa makosa ya jinai cha mwaka 1985.
Amesema Mahakama inaweza kumtia hatiani mtuhumiwa kutokana na ushahidi wa mazingira au ushahidi wa moja kwa moja ambapo alisema mshtakiwa anahukumiwa kutokana na ushahidi wa mazingira kwa sababu mhangwa wa tukio hilo alishindwa kutoa ushahidi wa moja kwa moja.
Ameongeza kuwa mahakama hiyo imeona mshtakiwa anastahili adhabu kutokana na mtuhumiwa huyo kama mzazi kushindwa kujali afya ya mtoto ili hali alikuwa mama mlezi ikiwa ni pamoja na kumpeleka Hospitali kwa wakati ili apatiwe matibabu.
Ndeuruo amesema pia mahakama hiyo haikuridhishwa na na ushahidi wa mtuhumiwa alioutoa mahakamani kuwa majeraha yaliyokutwa mwilini mwa mhanga wa tukio hilo yalitokana na kuugua kwa tetekuwanga jambo ambalo alisema si la kweli.
Amesema kuwa mshtakiwa ametoa maelezo wakati wa utetezi wake yanayopingana na na maelezoya daktari aliyemtibu mgonjwa alipofikishwa hospitali wakati akitoa ushahidi mahakamani hapo.
Hata hivyo kabla ya kutoa hukumu hiyo Hakimu huyo alisema kutokana na ibara ya 16 ya sheria ya African Charter inayotaka Nchi itunge sheria ya kulinda haki za watoto ambapo Tanzania haina sheria hiyo hivyo kusababisha watu kuwanyanyasa watoto.
Hakimu huyo ametoa wito kwa taasisi zinazohusika kutunga sheria hiyo mara moja ili kulinda haki za watoto ambayo itatamka wazi adhabu kwa wale watakaobainika kuwatesa na kuwanyanyasa watoto.
Kwa upande wake mwendesha mashtaka wa Serikali Archiles Mulisa ameiiambia mahakama hiyo kumpa adhabu kali mtuhumiwa huyo ili liwe fundisho kwa wazazi wengine wenye tabia kama hizo ambao hajakamatwa.
Amesema kitendo kilichofanya na mshtakiwa huyo ni kitendo chakinyama ambacho kinatakiwa kulaaniwa vikali hivyo kupitia adhabu atakayopewa mtuhumiwa inaweza kupunguza unyasasaji kama huyo katika jamii.
Aidha mshtakiwa Wilvina alipotakiwa kujitetea ili apunguziwe adhabu kabla ya kusomewa aliomba mahakama hiyo impunguzie adhabu kwa kile alichodai kuwa ni mjamzito, pia hajui mtoto wake aliyemzaa alipo pamoja na mawasiliano na familia yake.
Akitoa hukumu hiyo hakimu Ndauruo amesema amesikitishwa na kitendo cha mtuhumiwa cha kuomba kupunguziwa adhabu kutokana nakutomwona mtoto wake hali inayoonesha kutomjali mtoto aliyemtendea kosa.
Ameongeza kuwa Mahakama imefuatilia historia ya nyuma ya mtuhumiwa ambayo haioneshi kama anamatukio kama hayo ambayo aliwahi kuyafanya lakini mtuhumiwa anastahili adhabu kali kama upande wa mashtaka ulivyo sahauri na kutokana na mhanga kuwa na ulemavu wa kudumu.
Amesema mahakama inamhukumu kifungo cha maisha kifungo kitakachothibitishwa na mahakama kuu kutokana na mtuhumiwa kuwa na haki ya kukata rufaa kama ameona ameonewa katika kesi hiyo.
 
Mwanamke huyo alipandishwa kizimbani Novemba 16, Mwaka chini ya Mwendesha mashtaka wa Serikali, Achiles Mulisa aliiambia Mahakama kuwa Mtuhumiwa Wilvina Mkandala (24) alitenda kosa la kusababisha majeraha akiwa na nia ovu ambayo imemsababishia ulemavu mtoto Aneth.

Benki ya CRDB yawashukuru wakazi wa Njombe kwa kuiwezesha kupata mafanikio makubwa.

Mkuu wa kituo cha Tumaini, Sister Coletha Ponela (kushoto) akifuatana na mkuu wa wilaya ya Njombe, Sarah Dumba pamoja na maofisa wa benki ya CRDB wakielekea ukumbi wa kituo cha Tumaini.
Meneja wa tawi la CRDB Njombe, Alison Andrew akiongea na watoto wa kituo cha Tumaini.
Mkuu wa wilaya ya Njombe Sarah Dumba akiongea na watoto wa kituo cha Tumaini.
Watoto wa kituo cha Tumaini wakiimba mbele ya mkuu wa wilaya na wageni kutoka benki ya CRDB.
Maafisa wa Benki ya CRDB wakishusha zawadi walizotoa kwa watoto wa kituo cha Tumaini.
Mkuu wa wilaya ya Njombe Sarah Dumba  akikabidhi zawadi.
Wafanyakazi wa benki ya CRDB, mkuu wa wilaya, watoto na walezi katika picha ya pamoja.
Wafanyakazi wa benki ya CRDB katika picha ya pamoja na mlezi wa kituo pamoja na mkuu wa wilaya.
Watoto wakionyesha michezo ya sarakasi.
Mlezi wa kituo sister Coletha akipokea akipokea zawadi ya Tshirt kutoka Benki ya CRDB.
 Baadhi ya wateja wa CRDB Njombe wakiwa katika tafrija na wafanyakazi wa Benki ya CRDB Njombe.
Njombe Jazz Band walikuwepo kuburudisha wageni waalikwa.
Wafanyakazi wa benki ya CRDB Njombe wakionyesha ujuzi mwingine wa kusakata rhumba.
Afisa Mikopo wa Benki ya CRDB Njombe akitoa somo la mikopo.
Wafanyakazi na wageni waalikwa wakiburudika kwa muziki.
Mmoja wa wateja wa Benki ya CRDB Njombe Edward Mwalongo, akitoa ushuhuda wake namna gani amenufaika kibiashara kupitia benki ya CRDB.

Baba Mtakatifu aanza wiki ya kufunga na kutoonekana hadharani.


Baba Mtakatifu Benedict wa 16 ameanza wiki yake ya mafungo ya kiroho ambapo atakuwa haonekani hadharani kwa wiki nzima ikiwa ni mwanzo wa safari yake ya kuelekea kuachia rasmi uongozi wa kanisa Katoliki na kusema kuwa ana matumaini ibada zake zitakuwa na mafanikio.
 Baba mtakatatifu atabakia Vatican na baadhi ya wasaidizi wake wa karibu kwa ajili ya ibada za awali za sikukuu ya Pasaka na atapata mapumziko mafupi kila siku kwa ajili ya kuonana na katibu wake Georg Gaenswein, ili kuyashughulikia masuala ya dharura ya kanisa.
 Baada ya wiki nzima ya ibada, Baba Mtakatifu atakutana na rais wa Italia, Giorgio Napolitano, tarehe 23 Februari kushiriki ibada ya Jumapili yake ya mwisho ifikapo tarehe 24 mwezi huu na kuzungumza hadharani kwa mara ya mwisho mbele ya waumini wapatao 10,000.
Kiongozi huyo wa kanisa Katoliki duniani ataachia uongozi rasmi tarehe 28 mwezi huu na inasemakana kuwa Waziri wa Utamaduni wa Vatican Kadinali Gianfranco Ravasi ndiye anayeonekana mtu mwenye nafasi kubwa ya kuchukua nafasi yake kwa muda mfupi au mrefu.

WAKAZI WA MBEYA WAJITOKEZA KWA WINGI KUIPOKEA TIMU YA MBEYA CITY KWA KUPANDA DARAJA KUSHIRIKI LIGI KUU MSIMU UJAO

Baadhi ya mashabiki wa timu yaMbeya City wakicheza na kusubiri timi iingie toka songea
Ni vituko mtindo mmoja jamaa kwa furaha ya timu ya Mbeya City kupanda daraja kushiriki ligi kuu anataka kuvua suruali


Chales Mwakipesile  Dr Samwel Lazaro  na mhandisi wa barabara wakipanga ratiba ya mapokezi

Hivi ndiyo timu ilivyopokelea maeneo ya uyole jijini Mbeya hapa timu ya Mbeya City inapokelewa na mashabiki wake

Watumishi wa jiji la Mbeya wakionyesha furaha yako kwa kucheza kiduku 

Baadhi ya waandishi wa habari wa mkoa wa Mbeya wakiwa makini kufuatilia matukio ya kuipokea Mbeya City

Mstahiki Meya wa jiji la Mbeya Athanas Kapunga mara baada ya kushuka toka wenye gari yake na ndiye aliyeongozana na timu hiyo toka songea akishangilia kwa furaha ya timu ya Mbeya City kupanda daraja

Nae pia mkurugenzi wa jiji la Mbeya JumaIdi hakuwa nyuma kuonyesha furaha yake kwa timu yake ya Mbeya City

Ni fuaraha na shangwe tu





Bibi huyu akicheza na kusema sasa tumepata timu yetu hii ndiyo timu ya Mbeya sasa du kumbe wabibi wamo nao kwenye michezo

Mashabiki wa Mbeya City

Mkurugenzi wa jiji la Mbeya Juma Idi na mkuu wa wilaya Mbeya Norman Sigalla wakikumbatiana kwa furaha wakati wa kuipokea timu hiyo katika ukumbi wa mkapa jijini Mbeya

Mkurugenzi wa jiji la Mbeya Juma Idi akiwashukuru wakazi wa jiji la mbeya kujitokeza kwa wingi kuipokea timu yao ya Mbeya City 

Mstahiki Meya wa jiji la Mbeya Athanas Kapunga akiongea na wapenzi wa timu ya Mbeya City mara baada ya timu hiyo kuwasili katika viwanja vya ukumbi wa mkapa jijini Mbeya


Wakuu wa idara mbalimbali za jiji la Mbeya wakimsikiliza meya wa jiji

Moja wa viongozi wa timu ya Mbeya City Emmanuel Kimbe akiwashukuru mashabiki na wakazi wa mbeya 

Kocha wa timu ya Mbeya City Juma mwambusi akiongea na wapenzi wa Mbeya City



Mkuu wa wilaya Mbeya Norman Sigalla akiwaasa wachezaji wa timu ya Mbeya City kuwa sasa ni wakati wa timu hii kuleta kombe la ligi kuu hapa mkoani Mbeya maana hi ndiyo timu yetu wakazi wa mkoa huu 



Picha ya pamoja

HUKUMU YA MWANAMKE ALIYEMLISHA MTOTO KINYESI NA KUMCHOMA MKONO NA KUSABABISHA MTOTO HUYO AKATWE MKONO NI LEO

WILVINA MKANDARA  HUKUMU YAKE NI LEO HABARI KAMILI TUTAWALETEA BAADA YA KUSOMWA KWA HUKUMU HIYO



PICHA NA MBEYA YETU

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...