Thursday, January 08, 2015

NAIBU WAZIRI AZOMEWA MCHANA KWEUPEEE...!!!

 
Naibu Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, Dk Makongoro Mahanga akisindikizwa na Polisi kutoka katika Ukumbi wa Arnautoglu Dar es Salaam jana, baada ya mafuasi wa Umoja wa Katiba ya Wananchi kumzonga alipokwenda kuhudhuria hafla ya kuapishwa wenyeviti wa Serikali za Mtaa wa Halmashauri ya Wilaya ya Ilala.

Wakati utata ukizidi kujitokeza katika uapishaji wa viongozi wa Serikali za Mitaa Mkoa wa Dar es Salaam kutokana na waliodaiwa kushinda kuwekwa kando na kuapishwa walioshindwa, Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dk Makongoro Mahanga jana alikumbana na zomeazomea hadi kulazimika kuondoka kwenye Ofisi za Manispaa ya Ilala, Arnatouglou ambako shughuli hiyo ilikuwa ikifanyika.
Dk Mahanga ambaye pia ni Mbunge wa Segerea (CCM), alizomewa akitakiwa kuondoka katika eneo hilo, akidaiwa kwamba angebadilisha matokeo na kuwapa ushindi wagombea wa chama chake.
Eneo hilo lilijaa wafuasi wa Chadema, CUF na CCM huku kila kundi likiwa limesindikiza wenyeviti wake kuapishwa katika shughuli ambayo ilifanyika kwa awamu tatu kwa kila jimbo; Segerea, Ilala na Ukonga kupewa saa mbili.
Waziri Mahanga aliwasili wakati wa zamu ya Segerea saa saba mchana, ndipo kundi la mashabiki wa upinzani lilipoanza kumzomea na kuimba nyimbo za kumkashifu na kutaka atoke katika ukumbi ulioandaliwa kwa ajili ya kuwaapisha wenyeviti. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

ESCROW YAWANG'OA WAFANYAKAZI 7 TRA

Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba (kulia), akimjulia hali aliyejifungua watoto pacha katika Hospitali ya Mwananyamala, Mwamvita Kilasi wakati waziri huyo alipokwenda hospitalini hapo kutoa misaada mbalimbali katika wodi ya watoto. Waziri huyo alikuwa akisheherekea siku yake ya kuzaliwa.

Sakata la ufisadi wa Sh306 bilioni katika Akaunti ya Tegeta Escrow limewang’oa wafanyakazi saba wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
Wafanyakazi hao wamesimamishwa kazi ikiwa ni mwendelezo wa utekelezaji wa maazimio manane ya Bunge kuhusu ripoti ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), kuhusu kashfa hiyo.
Wengine ambao tayari wameshawajibika katika kashfa hiyo ni aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema aliyejiuzulu, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka aliyefukuzwa kazi na Rais Jakaya Kikwete na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi aliyesimamishwa kupisha uchunguzi. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

SOMA MAGAZETI YA LEO JANUARI 08, 2015

.
.
. 
Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

POLISI UFARANSA WATOA PICHA ZA WASHUKIWA

Picha za washukiwa waliotajwa na polisi wa Ufaransa 

Polisi wa Ufaransa wametoa majina na picha ya washukiwa wawili waliohusika na shambulio katika ofisi za jarida la vibonzo nchini humo.
Polisi wamemtaja Said Kouachi na kaka yake Cherif wanaweza kuwa watu hatari na wenye silaha.
Cherif Kouachi aliwahi pia na kuhusika na kupeleka wapiganaji wenye msimamo mkali wa kidini nchini Iraq.
Vyombo vya Habari vya Ufaransa vimesema mtu wa tatu ambaye amegunduliwa pia kama ni mshukiwa Hamyd Mourad mwenye umri wa miaka 18 alijisalimisha polisi baada ya kuona jila lake katika mitandao ya kijamii.
Baadhi ya rafiki zake walisema katika mitandao hiyo kwamba alikuwa shule wakati shambulio hilo katika ofisi za jarida la vibonzo la Charlie Hebdo likitokea, ambako watu 12 waliuawa.
Uchunguzi mkali bado unaendelea kuwasaka watu hao wenye silaha.
Awali jarida hilo lilipandisha hasira kwa waislamu baada ya kuchapisha kibonzo walichodai kuwa ni Mtume Muhamad SAW. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

Na BBC

UN KUSHIRIKIANA NA DRC KUWAONDOA FDLR

Wanamgambo wa FDLR  
 
Umoja wa Mataifa umesema Rais Joseph Kabila ameahidi kuwa jeshi lake litaungana na la UN katika operesheni dhidi ya waasi wa FDLR.
kikosi cha wanajeshi elfu 20 wa umoja huo watashirikiana na wale wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo katika kampeni zilizopangwa kuanza karibuni dhidi ya waasi wa Kihutu wa Rwanda.
Wanamgambo wa Kihutu, wanaojulikana kama FDLR, wamekuwa wakilitumia eneo la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo kama kambi yao ya kufanya mnashambulizi dhidi ya serikali ya nchi jirani ya Rwanda.
Waasi hao wameshindwa kufikia muda wa mwisho wa kimataifa uliowekwa wiki hii wa kuweka silaha chini na kuondoka katika eneo hilo. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

MAREKANI KUPAMBANA NA UKIMWI AFRIKA

Baadhi ya dawa za kupunguza makali ya virusu vya ukimwi.  
 
Marekani itatoa madawa ya kupambana na ugonjwa wa ukimwi kwa zaidi ya watoto laki tatu wanaoishi na virusi vya ugonjwa huo.
Nchi hiyo imetangaza kwamba madawa hayo yatatolewa katika nchi zilizo kusini mwa jangwa la Sahara, barani Afrika, katika kipindi cha miaka miwili ijayo.
Hatua hiyo ni sehemu ya mpango wake wa dola milioni mia mbili zilizoandaliwa kwa ajili ya kupambana na virusi vya ukimwi na ukimwi.
Balozi wa Marekani, Deborah Birth amesema mpango huo utalenga pia kuzuia maambukizo ya virusi vya ukimwi toka kwa mama kwenda kwa mtoto.
Umoja wa Mataifa umesema asilimia 95 ya watoto walioambukizwa virusi vya ugonjwa wa ukimwi wanaishi katika nchi zilizo kusini mwa jangwa la Sahara. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

Na BBC

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...