Saturday, December 20, 2014
MBUNGE ADAI KUVULIWA NGUO BUNGENI
Kufuatia
vurugu na purukushani zilizoonekana katika bunge la Kenya wakati wa
kupitishwa kwa mswada wa usalama ,mbunge mmoja mwanamke sasa amejitokeza
na kudai kwamba wabunge wenzake watatu wanaume walijaribu kumvua nguo.
Mbunge
huyo Millie Odhiambo aliandika katika mtandao wake wa facebook kwamba
wabunge wengi walipigwa huku yeye akidai kupigwa ngumi machoni na mbunge
mmoja kabla ya wabunge wawili kujaribu kumvua nguo.Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.
MSAKO MKALI KWENYE MTANDAO WA INSTAGRAM
Mtandao
wa kijamii wa Instagram umefuta mamilioni ya akaunti za watumiaji wa
mtandao huo katika msako wake wa kufuta akaunti bandia zilizokuwa
zikituma ujumbe ovyo ovyo kwa watumiaji wengine wa mtandao huo.
Watu
waliokuwa wanatumia mtandao huo na kuwa na wafuasi wengi, walilalamika
sana kufuatia hatua hio na kuitaja kama "Instagram Rapture".Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.
Friday, December 19, 2014
HII NDIO LIST YA WASANII 10 WA NIGERIA WALIOVNJA REKODI YA KUTAFUTWA KUPITIA GOOGLE
Mwaka unaisha, kwenye ule mfululizo wa rekodi mbalimbali za mwaka
2014 bado kuna nyingine nyingi millardayo.com itakuwa ikikupatia. Tumezisikia rekodi nyingi za nje ya Afrika, sasa hivi moja ya
jitihada ninazozifanya ni kukusanya zile rekodi za Afrika na kukuletea
mtu wangu.
Davido ni mmoja ya mastaa ambao tukiuzungumzia muziki wa Afrika
Magharibi, jina lake ni moja ya majina ambayo yameng’aa sana kwa mwaka
2014. Mtandao wa Google umemtaja Davido kwamba ni staa namba moja kwa kwa wanamuziki wa Nigeria aliyetafutwa zaidi mwaka 2014 kwenye mtandao.
Kwenye list hiyo Phyno ameshika namba mbili na nafasi ya tatu kushikwa na the Marvin’s Queen, Tiwa Savage. List kamili hii hapa....
1. Davido
2. Phyno
3. Tiwa Savage
4. Don Jazzy
5. Timaya
6. Ice Prince
7. Olamide
8. Sean Tizzle
9. Lil’ Kesh
10. Burna Boy
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz,
ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali
na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715
221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.
KENYATTA ASAINI SHERIA KALI YA USALAMA
Rais
wa Kenya Uhuru Kenyatta, ameidhinisha sheria mpya ya usalama ambayo
inawezesha majasusi kunasa mawasiliano kisiri au kufanya udukuzi pamoja
na kuwazuia washukiwa wa ugaidi kwa mwaka mmoja kabla ya kuwafungulia
mashitaka.
Kenyatta anasema kuwa sheria hiyo mpya inahitajika kwa
ajili ya kukabiliana na tisho la ugaidi kutoka kwa kundi la wapiganaji
wa kiisilamu la Al Shabaab.Amesisitiza kuwa sheria hio haikiuki haki za binadamu wala kuwapokonya watu uhuru wa kujieleza.
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.
HILI NDILO GARI LINALOWEZA KUJIENDESHA KWA KUTUMIA SAA
Hakuna kitu kibaya kama kusahau ulikoegesha gari lako katika jengo la kuegeshea magari lenye goraf nyingi.
Lakini
hivi karibuni hautahihajika kupanda gorofa kutafuta gari lako kwani
kampuni ya kutengeza magari ya BMW, imetangaza kuzindia kifuaa ambacho
kinaweza kuyawezesha magari ya kampuni hio kujiegesha yenyewe kwa
kubonyeza tu kifaa hicho.Hata hivyo dereva wa gari hilo atalazimika kuvaa saa ya Smartphone mkononi ambayo ataibonyeza na kuiamrisha kwa sauti gari hilo kwenda kujiegesha.
Gari hilo kwa amri ya dereva litatoka liliko baada ya dereva kushuka na kwenda lenyewe kwa kuhesabu muda utakalichukua kwenda kutafuta sehemu ya kujiegesha.
WENGER AIOGOPA LIVERPOOL KUFUATIA KIPIGO
Kocha
wa kilabu ya Arsenal Arsene Wenger amekiri kwamba anaogopa kichapo cha
5-1 alichokipata wakati timu yake ilipochuana na Liverpool msimu
uliopita, lakini akaongeza kuwa hatarajii kichapo kama hicho wakati timu
hizo mbili zitakapokutana siku ya jumapili.
Arsenal ilikuwa
imefungwa mabao 4-0 kufikia dakika ya 20 wakati wa mechi hiyo iliochezwa
Anfield huku Liverpool ikiongozwa na mshambuliaji hatari ambaye
ameihama kilabu hiyo Luis Suarez.Mechi hiyo ilikamilika ikiwa 5-1 dhidi
ya Arsenal.Lakini meneja huyo wa Arsenal anaamini mengi yamebadilika katika kipindi cha miezi 10,ikiwemo kuondoka kwa Suarez na jeraha la mshambuliaji Daniel Sturridge na mafanikio yake ya kumsajili Alexis Sanchez kutoka Barcelona mbele ya Breanda Rodgers.
Walikuwa wazuri sana katika safu ya mashambulizi,lakini msimu huu wamefunga mabao 19 pekee,hawana tena moto wa kufunga mabao waliokuwa nao.
Walianza kwa mori siku hiyo na sisi tulishindwa kujibu mashambulizi yao.
Kila mechi unayoshindwa inakua kovu katika moyo milele.Lakini tuna kumbukumbu nzuri katika uwanja wa liverpool.
Tulishinda mechi nyingi sana katika uwanja huo,lakini utakumbuka kwamba juma moja baadaye tuliweza kuishinda timu hiyo hiyo tulipocheza nayo nyumbani katika kombe la FA.' Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.
FIFA SASA KUCHAPISHA RIPOTI YA GARCIA
Maafisa
wakuu wa shirikisho la FIFA wamekubaliana kuchapisha ripoti yote kuhusu
uchunguzi wa madai ya ufisadi uliotokea wakati wa kutolewa kwa
kandarasi za kombe la dunia kwa mataifa ya Urusi mwaka 2018 na Qatar
mwaka 2022.
Wamekubaliana kutoa kurasa 430 za uchunguzi wa Michael
Garcia baada ya kufanya mkutano kufuatia pendekezo la mkuu wa kufuata
maagizo Domenica Scala.Ripoti hiyo itawekwa wazi baada ya uchunguzi unaondelea kuhusu watu watano kukamilika na inatarajiwa kufanyiwa uhariri ili kuficha majina ya mashahidi.
Hatua hiyo ya kuichapisha ripoti hiyo inaonyesha mabadiliko ya sera baada ya FIFA kukataa shinikizo kutoka kwa Garcia mwenyewe na wengine kutoa ripoti hiyo.
Garcia alijiuzulu siku ya Jumatano baada ya ombi lake la kupinga ripoti fupi ya uchunguzi wake iliotolewa na mwenyekiti wa kamati ya maadili katika shirikisho hilo Hans-Joachim Eckert kukataliwa.
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.
Thursday, December 18, 2014
PROFESA TIBAIJUKA: SINA HATIA, SIWEZI KUJIUZULU
Siku Moja baada ya kujiuzuri kwa Mwanasheria
mkuu Jaji Fredrick Werema, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya
Makazi, Profesa Anna Tibaijuka kwa mara nyingine amejitokeza hadharani
na kutoa msimamo wake kwamba hana sababu ya kujiuzuru kwenye nafasi yake
kwa kuwa hakuhusika kwa namna yeyote kwenye sakata la uchotwaji wa
mabilioni kwenye akaunti ya Escrow.
Akizungumza na waandishi wa habari asubuhi jijini
Dar es Salaam, Profesa Tibaijuka amesema kuwa pamoja na kuwepo kwa
shinikizo la kutaka kujiuzuru, yeye binafsi ameona hana sababu ya
kufanya hivyo kwani kufanya hivyo ni kukubali kuwa amehusika moja kwa
moja kwenye kashfa hiyo jambo ambalo si la kweli.
Profesa Tibaijuka amekwenda mbali zaidi na kusema
kuwa uvumi unaoendelea kusambazwa mitaani ni ishara mbaya kwani
unawaaminisha wananchi kuwa amehusika katika sakata hilo wakati yeye
hajahusika na jambo lolote.
“Huu uvumi unatakiwa kuachwa, sioni sababu yeyote
ya mimi kujiuzuru kwa kuwa sijahusika kwa namna yeyote kwenye sakata
hili la Escrow” anasema Profesa Anna Tibaijuka. Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz,
ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali
na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715
221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.
RAIS KIKWETE AKATISHA ZIARA YA PINDA UARABUNI
Waziri Mkuu ambaye yuko katika ziara ya kutembelea
nchi za Falme za Kiarabu, ikiwa ni sehemu ya kudumisha ushirikiano na
kutafuta wawekezaji, amekatisha ziara hiyo siku mbili baada ya
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema kujiuzulu kutokana
na kashfa ya Escrow.
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.
ASILIMIA 97 WACHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA 2015
Jumla ya wanafunzi 438,960 kati ya wanafunzi 451,392 waliohiyimu elimu ya msingi mwaka huu wamechaguliwa kujiunga na masomo ya kidato cha kwanza mwakani.
Idadi hiyo ni sawa an asilimia 97 ya wanafunzi wote waliofanya mtihani huo.
Taarifa ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa
na Serikali za Mitaa (Tamisemi) kwa waandishi wa habari leo imesema
ufaulu huo umeongezeka kwa asilimia 1.08 ikilinganishwa na mwaka jana.
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year
POLISI WAZUIA MAZISHI YA AISHA MADINDA HADI KESHO
Jeshi la
polisi limezuia mazishi ya aliyekuwa mnenguaji wa Twanga Pepeta na Extra
Bongo, Aisha Madinda hadi hapo mwili wake utakapofanyiwa uchunguzi
kutokana na utata wa kifo chake.
Akizungumza na Mwananchi, dada wa marehemu,
Hamida Mbegu alisema Polisi waliwaambia kuwa mwili huo unahitaji
kufanyiwa vipimo ili kubaini sababu za kifo chake, japokuwa familia
haikuwa tayari kwa jambo hilo.
Alisema Polisi walisisitiza kuwa ni lazima mwili ufanyiwe vipimo kutokana na kuwapo kwa utata wa kifo hicho.
Hamida amesema kwa mujibu wa polisi vipimo
vitafanyika asubuhi, hivyo baada ya vipimo kumalizika mwili utapelekwa
Kigamboni ambako ndiyo familia imekusanyika na baada ya swala ya Ijumaa
utazikwa kwenye makaburi ya familia yaliyopo Kibada, Kigamboni.
Akizungumzia suala hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Camilius Wambura, alisema kuwa kutokana na mazingira ya kifo hicho ni lazima Polisi wajiridhishe kwa kuufanyia mwili vipimo.
WABUNGE WARUSHIANA NGUMI BUNGENI...!!!
Wabunge
wa Kenya wametofautiana vikali bungeni na kuvuana mashati huku
wakirushiana ngumi kufuatia mjadala kuhusu mswada tatanishi wa usalama
ambao wabunge wa upinzani wanasema unakiuka uhuru wa wakenya.
Bunge
lililazimika kuahirisha vikao vyake kwa dakika 30 badala ya kujadili
mswada tatanishi kuhusu usalama wa nchi. Kikao cha leo kilikuwa kikao
maalum ambacho kilipaswa kupitisha mswada huo ambao baadaye
utaidhinishwa na Rais kuwa sheria.Wabunge wa upinzani walipinga mswada huo na kuanza kurusha karatasi sakafuni huku wakitatiza shughuli bungeni humo.
Subscribe to:
Posts (Atom)