Saturday, December 20, 2014

MBUNGE ADAI KUVULIWA NGUO BUNGENI

Muheshimiwa Millie Odhiambo ni mbunge wa eneo bunge la Mbita nchini kenya aliyedaiwa kuwa wabunge wenzake walijaribu kumvua nguo wakati walipokuwa wakipinga mswada wa usalama uliopitishwa katika bunge hilo siku ya alhamisi. 

Kufuatia vurugu na purukushani zilizoonekana katika bunge la Kenya wakati wa kupitishwa kwa mswada wa usalama ,mbunge mmoja mwanamke sasa amejitokeza na kudai kwamba wabunge wenzake watatu wanaume walijaribu kumvua nguo.
Mbunge huyo Millie Odhiambo aliandika katika mtandao wake wa facebook kwamba wabunge wengi walipigwa huku yeye akidai kupigwa ngumi machoni na mbunge mmoja kabla ya wabunge wawili kujaribu kumvua nguo.
 Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

Hivi ndivyo ujumbe huo ulivyosoma katika mtandao wake wa facebook:
''Tulijaribu kulemaza kikao hicho asubuhi yote.lakini ilipofika mwendo wa saa nane waliwasili wakiwa wamejitayarisha ya kutosha.Wabunge wengi walipigwa.Mimi mwenyewe nilipigwa ngumi machoni na mbunge mmoja huku wengine wawili wakijaribu kunivua nguo.lakini mimi si wa kulia lia kwamba nimepigwa kofi! Mbunge aliyenipiga amejua kwamba mimi ni mbunge wa Mbita aliyechaguliwa na wala si kuteuliwa.Walipojaribu kunivua nguo mimi mwenyewe niliwamalizia kuwavulia nguo.Mimi siogopi na nashkuru nilivyoumbwa.Sitakubali kutishwa kwa kutumia jinsia yangu'',aliandika bi Millie..
Maandishi haya baadaye yalifuatiwa na mengine yaliosema kuwa ameenda kupigwa picha na kuangaliwa jicho lake hospitali.

Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

Na BBC

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...