Mwaka
huu unaoishia unasemekana kuwa na kiwango cha juu zaidi cha joto
duniani na kwa Uingereza tangu kumbukumbu zianze kutunzwa.
Makadirio
ya awali yanaonyesha kuwa katika miezi kumi ya kwanza ya mwaka 2014,
wastani wa kiwango cha hali ya joto duniani kilikuwa 0.57C juu ya
wastani uliokuwepo muda mrefu.Na miezi kumi na mmoja ya kwanza nchini Uingereza imezalisha wastani wa joto la 1.6C likiwa juu ya wastani uliokuwepo kwa muda mrefu.Utafiti mwingine uliofanywa na Ofisi ya Hali ya Hewa ya Uingereza umeonyesha kuwa ongezeko la viwango vya joto vilivyoshuhudiwa, visingetokea bila ya ongezeko la gesi zinazoharibu mazingira kutokana na shughuli za binadamu. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, ukitaka kuwa wa kwanza kupata habari zetu Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz