Waziri
wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid na Kushoto ni Katibu Mkuu
wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,Charles Pallangyo.
Utangulizi
Wizara ya
Afya na Ustawi wa Jamii inapenda kutoa taarifa kwa Umma juu ya mwenendo
wa ugonjwa wa homa ya dengue yaani “dengue fever” hapa nchini.Ugonjwa
huu umethibitishwabaada ya sampuli zilizochukuliwa kutoka kwa watu
waliohisiwa kuwa na ugonjwa huu jijini Dar es Salaam kupelekwa kwenye
maabara yetu ya Taifa Dar es salaam na kuthibitisha kuwa na virusi vya
homa ya dengue mnamo mwishoni mwa mwezi wa Januari 2014. Hadi sasa idadi
ya wagonjwa ambao wamethibishwa kuwa na ugonjwa huuni 400 na Vifo 3.
Kwa wiki iliyoshia tarehe 9 Mei 2014 ya idadi ya wagonjwa waliogundulika
mkoani Dar es salaam ni 60 (42-Kinondoni, 14-Temeke na 4-Ilala) na
idadi ya wagonjwa waliopo wodini mpaka sasa ni 13.
Aidha, mlipuko wa ugonjwa huu si mpya hapa nchini kwani uligundulika kwa
mara ya
kwanza mnamo Juni 2010 mkoani Dar es Salaam ambapo idadi ya watu 40
walithibitika kuwa na ugonjwa. Pia, kati ya mwezi Mei hadi Julai
2013,wagonjwa 172 walithibitishwa kuugua ugonjwa huu.
Homa ya Dengue
Homa ya dengue ni ugonjwa unaosababishwa na kirusi ambacho kinaenezwa na mbu wa aina ya Aedes.
Dengue in
ugonjwa uliosambaa duniani katika nchi za ukanda wa joto. Takribani
asilimia 40 ya watu wote duniani wanaishi katika nchi zenye ugonjwa huu.
Takwimu za Shirika la Afya Duniani zinathibitisha kuwa takribani
matukio milioni 5 ya Dengue yanatolewa taarifa kila mwaka. Watu laki 5
hulazwa hospitali kwa kuathirika na Dengue kali. Homa ya Dengue
imeshatokea katika nchi zipatazo 34 barani Afrika.
Hapa Afrika
Dengue ni ugonjwa unaojulikana kwa kiwango kidogo sana. Licha ya kwamba
milipuko ya kwanza imetokea tangu mwanzoni wa karne ya 19. Matukio ya
Ugonjwa huu yameongezeka Afrika tangu miaka ya 1980, matukio mengi
yakitokea nchi za ukanda wa Mashariki mwa Afrika ikiwa ni pamoja na
Msumbiji, Somalia, Kenya, Komoro, Djibouti na Tanzania. Ikumbukwe kuwa
jina “Dengue” linatokana na neno “Dinga” la kiswahili linalolomaanisha
ugonjwa unaotakana na pepo yaani Kudinga pepo. Mabaharia wa Kispanish
walipokuja kwenye pwani ya Afrika Mashariki walirudi kwao na kuuita
“Dengue”.