Maelfu ya Wananchi wa Kata ya kikuyu kusini wakiandamana katika mitaa ya mji wa Dodoma kwa ajili ya kupinga kubomolewa na mamraka ya ustawishaji makao makuu [CDA] wanaotarajia kubomoa nyumba, mapagale na misingi ya wakazi hao.
Hukumu hiyo imetolewa leo na Hakimu
Mkazi, Aloyce Katemana baada ya Wakili wa Serikali Mwandamizi, Tumaini
Kweka kusoma maelezo ya awali na mshtakiwa huyo kukiri alitoa taarifa ya
uongo kwa polisi kuhusu tukio hilo.
Kabla ya hukumu hiyo, Mulundi aliomba
Mahakama impunguzie adhabu kwa kuwa hilo lilikuwa kosa lake la kwanza.
Pia alijitetea kuwa Juni 27, 2012 akiwa Arusha alitekwa na kupelekwa Dar
es Salaam ambako alikuwa hana mwenyeji wala hakuwahi kufika.
Alisema kutokana na kutekwa huko
alichanginyikiwa hivyo kukubali chochote alichoambiwa afanye kwa kuwa
aliyemteka alikuwa na silaha na alimwelekeza mambo ya kuzungumza.
"Mheshimiwa kwa ajili ya vitisho
hivyo, nilikwenda Kawe katika Kanisa la Ufufuo na Uzima lililoko kwenye
eneo la Tanganyika Packers, mbele ya Mchungaji Joseph Malwa Kiliba na
kuungama kuwa ni miongoni mwa watu waliomtesa Dk Ulimboka katika Msitu
wa Pande," alisema Mulundi na kuongeza:
"Siwalaumu Serikali, upande wa mashtaka wala polisi kwa kitendo cha kuniweka gerezani kwa muda mrefu, najilaumu mimi mwenyewe."
Kabla ya kutolewa kwa hukumu hiyo,
Kweka aliiambia Mahakama kuwa hana kumbukumbu za uhalifu za mshtakiwa
lakini aliomba apewe adhabu kali kutokana na mazingira ya tukio hilo.
Akitoa hukumu, Hakimu Katema alisema alifikia uamuzi huo kwa kuzingatia maombi ya mshtakiwa ya kupunguziwa adhabu.