HUKU ikidaiwa kwamba ni wapenzi, mastaa wawili wa
fani tofauti, mcheza filamu na mwanamuziki, Zuwena Mohammed ‘Shilole’
na msakata kabumbu wa klabu ya Simba, Mrisho Ngassa, Jumatano iliyopita
walizua timbwili katika klabu ya usiku ya SunSiro iliyopo Ubungo
jijini Dar.

Zuwena
Mohammed ‘Shilole’.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, Ngassa alifika katika klabu hiyo saa saba za usiku kushuhudia Bendi ya Mashujaa iliyokuwa ikitumbuiza akifuatana na watu wawili, mmoja mwanaume na mwingine mwanamke.
Inadaiwa kuwa Shilole alipoingia ukumbini humo na kuonana na Ngassa aliyekuwa na kampani yake, alipandwa na hasira na kuanza kujibishana naye.
Chanzo kinatiririka kuwa kabla Shilole hajaingia ukumbini humo, alimuomba kijana anayeuza pipi aitwaye Abdallah Rashid amuoshee gari lake kwani lilikuwa limechafuka bila ya kukubaliana naye bei.
Baada ya Shilole kutoka kwa hasira kutokana na kujibishana na Ngassa, moja kwa moja aliingia kwenye gari lake na kutaka kuondoka bila ya kumlipa kijana aliyemuoshea gari lake.
“Kwani unanidai shilingi ngapi?” Shilole alimuuliza kijana aliyesema kwamba anadai shilingi elfu tano.
“Baada ya Shilole kutajiwa kiasi hicho, alikataa kulipa kwa kuwa ni kikubwa na kumfanya kijana huyo kuwa mbogo na kuanza kurushiana maneno na staa huyo,” kilisema chanzo chetu.
Chanzo hicho kikaendelea kutoboa kuwa wakati kijana huyo akipigizana kelele na Shilole, Ngassa alitokea na kumvaa huku akimuuliza kwa nini anagombana na wanawake na kuanza kurushiana naye maneno, kiasi cha kutaka kuzipiga lakini wakatulizwa na wasamaria wema.
“Ngassa alikunjwa na jamaa ambaye alikuwa amekasirika kutokana na kudhulumiwa haki yake,” kilisema chanzo chetu.
Hata hivyo, baada ya ugomvi huo, Shilole na Ngassa kila mmoja aliingia kwenye gari lake na kutokomea bila kumlipa aliyeosha gari.
Baadhi ya mashuhuda walisema kuwa Ngassa na Shilole walikuwa na ugomvi uliohusiana na masuala ya kimapenzi.
“Hata yule mwanamke aliyekuwa na Ngassa alisema kwamba Shilole anahangaika kumfuata Ngassa wakati mcheza soka huyo hamtaki,” kilisema chanzo chetu.

Aidha, Ngassa alikanusha madai ya kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Shilole kwa kusema kuwa hawezi kutembea na msanii wa filamu.
Naye Shilole alipopigiwa simu alisema kuwa timbwili lilizuka kati yake na mtu aliyeosha gari lake bila ya ridhaa yake.
“Miye nimeenda pale kimpango wangu wala sikumfuata Ngassa ingawaje kweli nilimuona lakini wala sikuongea naye,” alisema staa wa muziki na filamu.

Shilole.
Paparazi
wetu alipompigia simu Ngassa kumuuliza kuhusiana na timbwili hilo,
alikiri kutokea na kusema kuwa alikuwa akimsaidia Shilole.Aidha, Ngassa alikanusha madai ya kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Shilole kwa kusema kuwa hawezi kutembea na msanii wa filamu.
Naye Shilole alipopigiwa simu alisema kuwa timbwili lilizuka kati yake na mtu aliyeosha gari lake bila ya ridhaa yake.
“Miye nimeenda pale kimpango wangu wala sikumfuata Ngassa ingawaje kweli nilimuona lakini wala sikuongea naye,” alisema staa wa muziki na filamu.
CHANZO; GLOBAL PUBLISHERZ

Dk Steven Ulimboka akiwa chumba cha wagonjwa
mahututi MOI.
Mkurugenzi Mtendaji
wa Hali halisi publishers Ltd, Saed Kubenea akiwa katika wodi ya
Hospitali ya Apollo, New Delhinchi INDIA mara baada ya
kufanyiwa Upasuaji macho, Kubenea
amekuwa akitibiwa katika Hospitali hiyo tokea mwaka 2008 alipomwagiwa
tindikali katika ofisi yake jijini Dar es Salaam na hii ni operesheni
yake ya tano.

Meneja
wa bia ya Kilimanjaro Bw. George Kavishe akizungumza na waandishi wa
habari katika ofisi za TBL Masaki wakati alipozungumzia uzinduzi wa Tuzo
za Kilimanjaro Music Award na kuasiniwa kawa mkataba wa udhamini wa
Tuzo hizo kati ya kampuni ya TBL na BASATA.
Kushilla
Thomas Mkurugenzi wa Masoko wa TBL akibadilishana hati na Godfrey
Mngereza Kaimu Katibu Mtendaji wa BASATA baada ya kusainiwa kwa mkataba
huo, huku viongozi wengi9ne wa TBL na BASATA wakipiga makofi.