Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Naiz Majani.
JUMLA
ya wajawazito 35 wamefamyiwa uchunguzi wa kipimo cha
magonjwa ya moyo kwa watoto wachanga waliopo tumboni mwa mama zao (FETAL
ECHOCARDIOGRAPHY) ili kujuwa kama wanamatatizo ya moyo au la.
Majibu
ya kipimo hicho yalionyesha kuwa kati ya hao watoto watano walikutwa na
matatizo ya moyo jambo ambalo litawawezesha kupata matibabu mapema
pindi watakapozaliwa.
Hayo
yamesemwa na Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto kutoka
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Naiz Majani wakati akiongea na
waandishi wa habari hivi karibuni.
Dkt.
Naiz alisema kipimo hicho hakina madhara yoyote kwa mama na mtoto na
kina uwezo wa kugundua endapo mtoto ameathirika na ugonjwa wa moyo na
hivyo kumuandaa mama mjamzito kwaajili ya uzazi salama.
“Mojawapo
ya dalili za mama mjamzito ambazo zinaweza pelekea kupata mtoto mwenye
tatizo la ugonjwa wa moyo ni pamoja na ugonjwa wa kisukari,shinikizo la
damu,matumizi ya dawa za muda mrefu,mimba ya mapacha, kuwepo na mtu
mwenye tatizo la moyo katika familia na mimba pandikizi”.
“Ninawaomba
kina mama wajawazito wenye moja ya dalili nilizozitaja waje tuwafanyie
kipimo hiki kipindi ambacho mimba zao zitakuwa na umri wa kati ya
miezi minne hadi saba hii itawasaidia kugundua afya za watoto wao na
kuepuka na vifo vya mara baada ya kuzaliwa vinavyotokea kipindi cha
mwezi mmoja hadi mwaka”, alisema Dkt. Naiz.
Alizitaja
changamoto wanazokabiliana nazo kuwa ni pamoja na uelewa mdogo wa
kinamama wajawazito juu ya kipimo hicho kwa kufikiria kuwa kinamadhara
jambo ambalo siyo kweli kwani kipimo hicho hakina madhara yoyote
kiafya.
Taasisi
ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ilianza kutoa huduma hiyo tangu mwezi wa
tatu mwaka huu ili kupunguza vifo vya watoto vinavyotokana na
magonjwa ya moyo mara baada ya mtoto kuzaliwa.
Na Sweetbert Hudson.