SERIKALI ya Marekani juzi ilitangaza kutaifisha mali za bilionea Mtanzania, Ali Khatib Haji Hassan, maarufu Shikuba pamoja na mtandao wake wa kimataifa wa biashara ya dawa za kulevya.
Shikuba ambaye ni mfanyabiashara maarufu Dar es Salaam, anamiliki msururu wa biashara kama vile maduka ya kubadili fedha (bureau de change), kampuni za ulinzi, majumba na utitiri wa magari ya kifahari.
Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Fedha ya Marekani kupitia ofisi yake ya Udhibiti wa Mali Haramu za Raia wa Kigeni (OFAC), Shikuba na taasisi yake wameangukia katika sheria za nchi hiyo za kudhibiti mapapa wa unga wa kigeni (Kingpin Act).
Mbali ya sababu za kisheria, Marekani imesema bilionea huyo amekuwa akitumia faida haramu kutokana na biashara zake chafu kuhonga maofisa wa Serikali ya Tanzania ili asikamatwe na kushtakiwa. Like page yetu ya facebook Jambo Tz