Monday, June 09, 2014

BAJETI YAMPELEKA JK DODOMA


kikwete_36f36.jpg
Rais Jakaya Kikwete anatarajiwa kuwasili Dodoma keshokutwa, ikiwa ni siku moja kabla ya kuwasilishwa kwa Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2014/15.
Habari zilizopatikana jana zinasema Rais ataongoza kikao cha Baraza la Mawaziri kitakachopewa muhtasari kuhusu Bajeti ya Serikali ya mwaka ujao wa fedha na baadaye atafuatilia uwasilishaji wa bajeti hiyo bungeni akiwa Dodoma.
Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Salva Rweyemamu alisema asingeweza kuzungumzia suala hilo kwa kuwa yuko likizo lakini akaweka bayana kwamba kwa kawaida kabla ya bajeti kuwasilishwa bungeni, lazima Baraza la Mawaziri lipewe muhtasari wa bajeti husika.
"Ni kawaida kabla ya bajeti kuwasilishwa, Rais huongoza kikao cha Baraza la Mawaziri yaani pre budget cabinet meeting ambako Waziri wa Fedha hutoa briefing (muhtasari) kuhusu maeneo muhimu ya bajeti, kwa hiyo siyo jambo jipya ni suala la kawaida," alisema Rweyemamu.
Itakumbukwa kuwa mwaka jana kabla ya kusomwa kwa bajeti ya 2013/14, Rais Kikwete alikuwa Dodoma ambako pamoja na kukutana na mawaziri, pia alifanya kikao na Kamati ya Bunge ya Bajeti.
Hata hivyo, uwepo wake mjini Dodoma safari hii umekuja wakati kukiwa na dalili za mvutano mkubwa kati ya Bunge na Serikali kutokana na kutotolewa kwa fedha za kutosha za maendeleo kwa mwaka wa fedha unaoisha Juni 30 mwaka huu. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

ADUMAA KWA MIAKA 18, AOMBA MSAADA WA KUTIBIWA...!!!


dumaapx_72c1c.gif
Farida Abdallah (18), ambaye amedumaa kwa miaka 18.
Wazazi wa binti mwenye ulemavu wa viungo na akili, Farida Abdalah (18) mkazi wa Lukobe Juu mkoani Morogoro wameiomba Serikali, wasamaria wema na wadau mbalimbali kumsaidia binti yao huyo ambaye kwa sasa amelazwa katika hospitali ya rufaa na anaendelea kufanyiwa uchunguzi wa afya yake.
Pia wazazi hao ambao walionekana kuwa na hali ngumu ya kimaisha

waliomba msaada wa kupatiwa matibabu ya viungo na akili kwa binti yao ili aweze kutembea na kujitambua, kwani kwa sasa binti huyo amekuwa akilala tu kitandani.

Maisha ya binti huyo ambaye umri wake haulingani na umbo lake yameguswa na watu wengi, kwani amekuwa haongei, halii, hasikii na wala hajitambui hivyo amekuwa akivalishwa nepi na kubebwa kama mtoto mchanga.

Akitoa historia ya binti huyo kwa mwandishi wa habari hizi jana mama mzazi wa binti huyo Mwajuma Abdalah alisema kuwa Farida alizaliwa mwaka 1996 wilayani Muheza mkoani Tanga na alijifungulia nyumbani. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MAMBO 20 MUHIMU KUHUSU KOMBE LA DUNIA



1 — Mechi zote za Kombe la Dunia 1930 nchini Uruguay  zilichezwa kwenye jiji moja: Montevideo.
2 — Beki wa Sweden, Jan Olsson, alikuwa akivaa jezi namba 2, beki huyo ndiye aliyemdhibiti vilivyo nyota wa Uholanzi, Johan Cruyff aliyekuwa akisifika kwa aina yake ya ugeukaji  na kuwatoroka mabeki “Cruyff Turn” kwenye fainali za mwaka 1974, Ujerumani Magharibi.
3 — Gwiji wa Brazil, Pele ni mchezaji pekee aliyetwaa  makombe matatu ya dunia akiwa anacheza mwaka: 1958, 1962 na 1970.
4 — Idadi ya wachezaji waliofunga mabao matatu katika mechi  mbili za Kombe la Dunia: Mhungary Sandor Kocsis (zote mwaka 1954), Mfaransa, Just Fontaine (1958), Mjerumani,  Gerd Muller (1970) na Gabriel Batistuta (moja 1994 na moja 1998).
5 — Mshambuliaji wa Russia, Oleg Salenko ndiye  anayeshikilria rekodi ya kufunga mabao matano katika mechi moja ya Kombe la Dunia, wakati Russia waliposhinda 6-1  dhidi ya Cameroon fainali za 1994 nchini Marekani. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MAGAZETI YA LEO JUMATATU JUNI 09, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS


.

.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

PAPA AWAPOKEA MARAIS WA ISRAEL NA PALESTINA VATICAN

Mahmoud Abbas, Papa na Shimon Peres Vatikani
Kiongozi wa Kanisa Katoliki Papa Francis amewakaribisha Rais wa Israil, Shimon Peres, na mwenzake kutoka Palestina, Mahmoud Abbas, katika maombi ya aina ya kipekee katika makao makuu ya Kanisa Katoliki ya Vatican. Viongozi hao wawili walikutana na Papa nje ya makaazi yake kabla ya kuandamana naye, wakiandamana na kiongozi wa Kanisa la Ordhodoz, Partriarch Artholomew kwa hafula maalumu katika Medani ya Vatican. Akiongea katika hafula hiyo Papa alisema ujasiri na nguvu vinahitjika katika juhudi za kuleta amani.

"Kuleta amani kunahitji ujasiri mkubwa kuliko vita. Kunahitaji ujasiri wa kusema ndio kwa mkutano na La kwa vita; ndio kwa mashauriano na La kwa makabiliano; ndio kwa kuheshimu mikataba na La kwa uchokozi; Ndio kwa ukweli na La kwa Uongo; kwa haya yote tunahitaji ujasiri na nguvu moyoni," Papa alisema
Na katika hotuba yake Bwana Peres alisema alitakia vizazi vyote vijavyo amani ya kudumu:
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz


"Rafiki wapenzi, Nilikuwa mchanga, na sasa nimezeeka. Nilishuhudia vita, Nilionja amani. Sitawahi kusahau familia zilizofiwa, wazazi na watoto waliolipia gharama kubwa kwa vita hivyo. Na maisha yangu yote sitakoma kuitisha amani, kwa niaba ya vizazi vijavyo. Naomba sisi sote tuuungani mikono na kufurahi kwa sababu ni wajibu wetu kufanya hivyo kwa niaba ya watoto wetu.

UWANJA WA NDEGE WASHAMBULIWA PAKISTAN

Wanajeshi wa Pakistan wakiwa kwenye uwanja wa ndege wa Karachi kukabiliana na washambulizi.
Mapambano ya risasi yaliyodumu saa tano katika uwanja wa mji mkubwa zaidi nchini Pakistani ,Karachi yamewauwa watu 23 wakiwemo washambuliaji wote 10.
Washambuliaji hao waliokuwa na silaha nzito nzito waliingia sehemu ya majengo ya uwanja huo kupitia njia zinazotumiwa na ndege za mizigo au zile zinazotumiwa kuwapokea wageni wenye hadhi na sifa yaani V.I.Ps.
Walipenya usiku wa manane na kuanza kuwashambulia maafisa usalama kwa gruneti na kwa kuwafyatulia risasi.
Makamanda katika jeshi waliitwa kukabiliana na washambuliaji hao na milio ya risasi ilisikika hadi alfajiri wakati hali ilipodhibitiwa. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Haijabainika vyema ni akina nani hasa walioshambulia lakini yamewahi kufanyika mashambulio kama hayo hasa katika maeneo ya wanajeshi wa angani na wa majini ambapo wanamgambo wa Taliban walihusika.
Na BBC

Sunday, June 08, 2014

TANZIA: MZEE SMALL AFARIKI DUNIA

1_e4ab8.jpg
Mzee Small enzi za uhai wake.
Muigizaji mkongwe nchini, Said Ngamba maarufu kwa jina la Mzee Small amefariki dunia usiku huu akiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar. Mzee Small amefariki kwa ugonjwa wa presha baada ya kuugua kwa muda mrefu kabla ya kuzidiwa jana na kupelekwa Muhimbili. Mtoto wa marehemu aitwaye, Muhidin amethibitisha kifo cha Mzee Small. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI JUNI 08, 2014 YA DINI, MICHEZO NA HARD NEWS

..
.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

ANGALIA PICHA ZA HARUSI YA MBUNGE JOSHUA NASSARI ILIVYOFANA



2_31d12.jpg
Mbunge wa Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Samwel Nassari jana amefunga ndoa na Anande Nko kwenye Kanisa la Pentekoste lililopo Kilinga, Arumeru jijini Arusha ikifuatiwa na sherehe kubwa iliyofanyika katika Viwanja vya Usa-River Academy jirani na Hoteli ya Ngurdoto.
Sherehe hiyo ilianza saa 7:00 mchana  ambapo watu wote walialikwa wakiwemo ndugu, marafiki, jamaa na wananchi wote wa Arumeru Mashariki ambao wamepiga 'mpunga' wa kutosha na vinywaji hadi kila mtu akaondoka akisema 'Nassari ameacha historia'. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
CHANZO: Mitandao ya Kijamii.

RAIS MPYA WA MISRI KUAPISHWA

Raia wanaomuunga mkono Abdel Fatah al sisi
Usalama umeimarishwa katika mji mkuu wa Misri, Cairo kabla ya kufanyika kwa sherehe ya kumuapisha rasmi rais mpya wa taifa hilo Abdel Fatah el Sisi.
Rais huyo mteule atakula kiapo chake cha kuchukua mamlaka katika mahakama kuu ya kikatiba mjini Cairo.
Alishinda uchaguzi wa urais wa mwezi uliopita kwa wingi wa kura ijapokuwa idadi ya waliojitokeza kushiriki katika shughuli hiyo ilikuwa chini ya asilimia 50.
Uchaguzi huo unajiri miezi michache tu baada ya kiongozi huyo kumpindua madarakani aliyekuwa rais wa taifa hilo Mohammed Morsi.
Mkuu huyo wa jeshi wa zamani ameanzisha msako dhidi ya wanaompinga mbali na kukipiga marufuku chama cha Morsi cha Muslim Brotherhood. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Na BBC Swahili

Saturday, June 07, 2014

MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI JUNI 07, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS


.

.
.
.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MAHAKAMANI KWA KOSA LA KUAGIZA MAITI IKATWE MIGUU...!!!


Mwandalizi mmoja wa mazishi nchini Afrika Kusini, anayedaiwa kuwaagiza wafanyakazi wake kuikata miguu ya maiti moja aliyodai kuwa ndefu sana alifikishwa mahakamani Ijumaa.
Ronel Mostert anayemiliki chumba cha kuhifadhi maiti ambacho pia huendesha shughuli za mazishi, alitoa amri hiyo kwa lengo la kuhakikisha kuwa maiti hiyo ingetosha katika jeneza. Anakabiliwa na kosa la kumkata miguu maiti.
Mfanyakazi mmoja aliimbia mahakama kuwa Ronel alimuagiza kuchukua kifaa kimoja cha kukata ili kuikata miguu hiyo ya marehemu na kwamba jambo hilo limekuwa likimsumbua sana kimawazo.
Mwili marehemu ulifukuliwa ili kusaidia katika uchunguzi wa polisi.Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Na BBC

MADEREVA WA UMMA WAGOMA BRAZIL

Mgomo wa wafanyakazi hao umesababisha uhaba wa magari ya usafiri
Maafisa wa polisi nchini Brazil wametumia gesi ya kutoa machozi ili kuwatawanya waandamanaji katika siku ya pili ya mgomo wa wafanyikazi wa sekta ya uchukuzi ambao umesababisha uhaba mkubwa wa usafiri wa uma katika mji wa Sao Paulo.
Takriban nusu ya vituo vya treni vilifungwa na kusababisha msongamano mkubwa wa watu katika barabara za mji huo mkubwa ambao unatarajiwa kuandaa michuano ya kombe la dunia kuanzia alhamisi ijayo.
Wafanyakazi hao wa treni wanataka mishahara yao kuongezwa kwa asilimia kumi.
Awamu nyengine ya majadiliano imefeli na wafanyikazi hao wanasema kuwa mgomo huo utaendelea kwa mda usiojulikana. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Na BBC

MWEGANE YEYA WA MBEYA CITY AAHIDI MAKUBWA TAIFA STARS, AMSHUKURU MUNGU KWA KUITWA NA MART NOOIJ


Mwagane-Yeya.pngnnnnnnnnnnnnnnNa Baraka Mpenja, Dar es salaam
MSHAMBULIAJI hatari wa Mbeya City fc, Mwegane Yeya amefurahishwa na kitendo cha kuitwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars chini ya kocha Mholanzi, Mart Nooij.
Akizungumza na mtandao huu, Mwegane amesema kuwa anamshukuru sana Mungu kwa kupata nafasi hiyo kwasababu Tanzania ina wachezaji wengi wenye viwango vya hali ya juu, lakini amechaguliwa yeye.
“Hii ni nafasi nyingine muhimu kwangu. Niliwahi kuitwa katika kikosi cha Young Future Taifa Stars na Kim Poulsen, lakini sikufanya vizuri kwasababu nilikuwa majeruhi. Naamini kwasasa nitaitumia vizuri nafasi hii”. Alisema Mwegane ambaye ni hatari kwa kufunga magoli ya kichwa. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Friday, June 06, 2014

WARIOBA AZISHUKIA UKAWA NA CCM


Katika Bunge hilo, wajumbe wengi wa CCM walimshambulia Warioba na tume yake wakidai kuwa Rasimu ya Pili ya Katiba haikuzingatia maoni ya wananchi na Mabaraza ya Katiba. PICHA|MAKTABA 

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba amewashauri wajumbe wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) na CCM kuacha kuzunguka mikoani kufanya mikutano inayoeleza misimamo yao kuhusu mchakato wa Katiba Mpya kwa kuwa haina tija kwa taifa.
Ameonya kuwa mikutano hiyo inajenga mwelekeo mbaya kwa taifa na kuhatarisha mchakato wa Katiba na kuzitaka pande hizo kumaliza tofauti zao.
Akizungumza katika mahojiano maalumu yaliyofanyika Dar es Salaam jana, Warioba alisema: “Kwa mustakabali mwema wa taifa, ni muhimu makundi haya ‘ya-resolve’ (yamalize), matatizo yaliyopo kabla ya Agosti, ili Bunge Maalumu la Katiba likirejea, wote washiriki na kukamilisha mchakato wa kupata Katiba Mpya. Hili ni kwa masilahi ya taifa.”
Kauli ya Waziri Mkuu huyo mstaafu ambaye pia aliwahi kuwa Mwanasheria Mkuu, imekuja huku makundi ya Ukawa linaloundwa na wabunge wengi wa upinzani na viongozi wa CCM wakiendelea kung’ang’ania misimamo yao kuhusu Rasimu ya Katiba Mpya iliyowasilishwa kwenye Bunge Maalumu la Katiba.
Wakati CCM ikipinga mapendekezo ya kuwapo kwa mfumo wa serikali tatu uliomo kwenye Rasimu, Ukawa unaunga mkono mapendekezo hayo. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...