Malumbano
makali ya maneno na hoja yamezuka baina ya Kiongozi wa Kanisa Katoliki
duniani, Papa Francis na Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu
kuhusu lugha gani aliyotumia Yesu Krtisto miaka 2,000 iliyopita.
Viongozi hao Jumatatu mchana wakati wa ziara ya
siku tatu ya Papa aliyoifanya katika eneo la Mashariki ya Kati ikiwa ni
ziara yake ya kwanza tangu atwae wadhifa huo. “Yesu aliishi hapa katika
ardhi ya nchi hii. Alizungumzia Kiebrania,” alianza Netanyahu wakati
akimweleza Papa Francis kwenye mkutano wa hadhara mjini Yerusalemu.
Netanyahu, pia akaeleza kuwa upo uhusiano wa karibu baina ya mahali alikozaliwa Yesu na Ukristo. Naye Papa Francis akasikiliza kwa muda, kisha akajibu: “Yesu alizungumza lugha ya Kiaramaiki.”
“Ndiyo, nimesema alizungumza Kiaramaiki, lakini pia alijua Kiebrania,” akaingilia kati Netanyahu.
Hata hivyo, mjadala huo umepokewa kwa hisia
tofauti na watu wengi ambao wamekuwa wakifuatilia ziara ya siku tatu ya
Papa Francis katika nchi takatifu. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz