Mbunge wa viti maalumu kwa tiketi ya
CUF, Amina Abdallah Amour amemjia juu katibu wa itikadi na uenezi wa
CCM, Nape Nnauye kwa kuufananisha Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) na
kundi la Boko Haramu na kutaka alaaniwe.
Ukawa iliundwa wakati wa Bunge Maalumu la Katiba na unahusisha wajumbe kutoka vyama vya NCCR-Mageuzi, Chadema na CUF.
Akizungumza bungeni mjini Dodoma juzi, mbunge huyo alisema kauli ya Nnauye ni ya uchochezi na inapaswa kulaaniwa.
Mbunge huyo alikuwa akichangia hotuba ya makadirio
ya mapato na matumizi ya Wizara ya Wanawake, Jinsia na Watoto kwa mwaka
2014/2015 iliyowasilishwa na waziri wake, Sophia Simba.
“Gazeti la Uhuru (jana) lilimnukuu Nape Nnauye
akisema Ukawa ni sawa na Boko Haramu… Hii ni kauli chafu na ya
uchochezi. Haikubaliki na ninailaani kwa nguvu zangu zote,” alisema.
Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz
Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz