Mlipuko katika mgodi wa makaa ya
mawe magharibi mwa Uturuki umesababisha vifo vya zaidi ya wachimbaji
migodi 200 na kujeruhi wengine wengi kujeruhiwa kwa mujibu wa maafisa
nchini humo.
Waziri wa kawi, Taner Yildiz, amesema kuwa zaidi
ya wafanyikazi 780 walikuwa katika mgodi huo pale kuliposikika mlipuko
katika kitengo cha kusambazia umeme.Waokoaji wanajaribu kila mbinu kuwafikia mamia ya wachimba migodi.
Inahofiwa kuwa wachimbaji mgodi wengine wengi bado wamefukiwa chini ya mgodi huo.
Inakadiriwa kuwa wakati mlipuko huo ulipotokea wafanyikazi 780 walikuwa ndani ya mgodi huo japo inaaminika wengi waliweza kukimbilia usalama wao .
Bado idadi ya walionaswa ndani ya mgodi huo haijabainika.
Mgodi huo uko katika mji wa Soma, mkoani Manisa , takriban kilomita 250 kusini mwa Istanbul. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz
Waziri wa nishati Taner Yildiz ameimabia televisheni ya Uturuki kuwa huenda wengi wamekufa kutokana na sumu ya gesi aina ya carbon monoxide.
Amesema moto huo umesababishwa na hitilafu ya umeme.
Picha za televisheni zinaonyesha maafisa wa uokoaji wakiokoa wafanyikazi wa mgodi huo, huku nyuso zao zao zikiwa zimejaa vumbi.
Baadhi yao wanaweza kutembea na wengine wanabebwa na kupelekwa ndani ya magari ya kubebea wagonjwa yaliyoegezwa karibu na eneo la tukio. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz