Saturday, March 15, 2014
Wednesday, March 12, 2014
JK ATANGAZA KIAMA CHA MAJANGILI
Wawakilishi
wa Chama cha Uhifadhi wa Wanyama cha Frankfurt (FZS), wakikabidhi
magari zaidi ya 11 kwa Rais Jakaya Kikwete Ikulu Dar es Salaam jana, kwa
ajili ya kusaidia vita dhidi ya ujangili wa wanyamapori katika hifadhi
na mbuga za taifa.Picha na Ikulu
Rais Jakaya Kikwete amesema Serikali
imenuia kumaliza kabisa ujangili nchini, ikiwa ni hatua ya kunusuru
wanyama walio hatarini kutoweka katika hifadhi za taifa.Hakusita kusisitiza kwamba, nia ya dhati ya Serikali ni kuhakikisha mkakati huo unakamilika, japokuwa kumekuwa na changamoto zinazotokana na ukubwa wa hifadhi hizo na uhaba wa vitendea kazi pamoja na askari wa wanyamapori.
Akizungumza wakati wa kupokea magari 11 ya kisasa kwa ajili ya kusaidia operesheni ya kupambana na ujangili kutoka kwa Shirika la Frankfurt Zoological Society (FZS) la Ujerumani, Kikwete alisema tatizo hilo limekuwa la muda mrefu, lakini juhudi za kulikomesha zinafanyika.
Alisema, pamoja na ukubwa wa tatizo hilo, bado kuna tatizo la uhaba mkubwa wa wafanyakazi wanaotakiwa kudhibiti majangili, ambapo kwa sasa kuna wafanyakazi 1,155 sawa na asilimia 24 tu ya mahitaji halisi ya wafanyakazi 4,000 wanaohitajika.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz
HII NDIO VIDEO YA AJALI YA NDEGE KUMGONGA MTU, MAAJABU...!!!
Hii
imetokea Florida Marekani ambapo mtu mmoja alikua anaruka akiwa na
Parachuti lakini akakutana na ndege hii ndogo ambayo baada ya kumgonga
walianguka chini wote huku ndege ikiangukia pua.
Pamoja na ajali hii, hakuna mtu aliepoteza maisha ila wote walipata
majeraha madogomadogo baada ya kuanguka kwenye umbali wa futi 75 na
wakapelekwa hospitali ambapo mwenye Parachuti John Frost (49)
aliruhusiwa kuondoka.
Hili tukio limenaswa jinsi lilivyotokea kwa sababu kulikua na mpiga
picha aliekua na camera karibu na alikua anashuhudia kila kitu.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz
KURA BADO KITENDAWILI BUNGE LA KATIBA
Wakati wajumbe wa Bunge Maalumu la
Katiba wakipitisha Rasimu ya Kanuni za kuendesha Bunge hilo, suala la
aina ya kura kwa ajili ya kuamua masuala mbalimbali, limekwama na
litaamuliwa na wabunge baada ya kuanza kwa vikao rasmi vya Bunge hilo.
Hatua hiyo imekuja baada ya kuwapo kwa
mvutano wa takriban wiki nne kuhusu rasimu, hasa kifungu cha 37 na 38
kinachoeleza aina ya kura kati ya wazi na ya siri.
Hata hivyo, wajumbe wawili wa Bunge
hilo, Mchungaji Christopher Mtikila wa DP na Felix Mkosamali wa NCCR-
Mageuzi walisusia kupitisha azimio la kukubali Kanuni za Bunge hilo,
wakidai kusalitiwa katika uamuzi huo na wenzao walioko kwenye Umoja wa
Katiba ya Wananchi (Ukawa).
Wajumbe na viongozi mbalimbali wa
vyama vyenye ushawishi bungeni, kwa pamoja waliridhia na kulegeza
misimamo yao ili upatikane mwafaka wa kutengeneza Katiba Mpya ndani ya
wakati. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz
RIDHIWANI, "SIKUSHINIKIZWA KUGOMBEA"
MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ridhiwani Kikwete ameahidi kuwa atajitahidi kutatua kero za maji, umeme na ajira kwa vijana. Alisema hayo jana baada ya kuchukua fomu katika ofisi za Msimamizi wa Uchaguzi wa Wilaya ya Bagamoyo, Shija Andrew.
Leo anatarajia kurudisha fomu hiyo. Ridhiwani alipokuwa akienda kuchukua fomu hiyo, alisindikizwa na mamia ya wanachama wa CCM wa majimbo ya Chalinze na Bagamoyo, wakiwa wanaimba na kucheza kumshangilia mgombea huyo.
Baada ya
kuchukua fomu kutoka kwa Ridhiwani alimhakikishia ofisa huyo kuwa
atazingatia taratibu zote za uchaguzi na kutoendesha kampeni za matusi
na vurugu.
Baada ya
kuchukua fomu hiyo na nakala nyingine muhimu za uchaguzi, aliongozana
tena na mamia ya wafuasi wake, kuelekea kwenye ofisi za CCM Wilaya ya
Bagamoyo, ambapo alizungumza na waandishi wa habari.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz
WAZIRI MKUU WA LIBYA AZUIWAKUSAFIRI
Kiongozi wa mashtaka Nchini Libya Abdel-al-Qader Radwan amemzuia Waziri mkuu wa taifa hilo aliyevuliwa madaraka, Ali Zeidan, kusafiri nje ya taifa hilo hadi pale uchunguzi dhidi yake utakapokamilika.
Anatuhumiwa kwa madai ya ubathirifu wa pesa za umma.
Bwana
Zeidan amesimamishwa kazi mapema siku ya Jumanne na Bunge la taifa
hilo, baada ya Wabunge kudai kuwa meli ya mzigo ya Korea Kaskazini
iliyokuwa imezuiliwa baada ya kunaswa ikibeba mafuta ghafi toka bandari
moja linalokaliwa na waasi huko Libya, ilivunja nanga na kusafiri
baharini.
Kura ya kutokuwa na imani na Bwana
Zeidan iliitishwa baada ya meli hiyo iliyokuwa na bendera ya Korea
Kaskazini kuabiri na kufikia maji makuu ya mipaka ya kimataifa baharini.Mafuta hayo yalikuwa yamenunuliwa kutoka kwa waasi wanaodhibiti bandari ya Al- Sidra.
Wabunge hawana imani na Waziri Mkuu
Bunge la Libya limemuachisha kazi Waziri huyo mkuu, baada ya kupitisha agizo la kutokuwa na imani naye.Hilo limeafikiwa baada ya meli ya Korea Kaskazini kuingia katika bandari ya taifa hilo na kuondoka na mafuta ghafi bila idhini ya serikali.
Makundi ya wapiganaji yamekuwa yakidhibiti baadhi ya bandari ya taifa hilo mashariki mwa taifa, tangu Julai mwaka jana na kuuza mafuta nje ya taifa.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz
Monday, March 03, 2014
ZITAMBUE CHANGAMOTO SITA (6) KWA KILA UCHUMBA/ NDOA...!!!
Ukweli
ni kuwa watu wawili wanapoamua kwa dhati
kuwa katika mahusiano ni kwamba wanakuwa tayari katika akili zao wamejenga
matarajio au matumaini ya kunufaika na uhusiano husika, hata kama hawawezi
ambiana moja kwa moja kuwa “ aisee, mie kuwa na wewe nataraji moja , mbili,
tatu….”.
Kunapokuwepo
na upendo, basi pia kunaleta majukumu, ambapo bila ya kutimizwa kwa majukumu
yanayotarajiwa kutimizwa, maana halisi ya mahusiano bora inapotea.
Hii
si tuu kwa mahusiano ya kimapenzi, bali hata dini zinatufundisha kuwa Mungu
anatupenda, na katika hilo, tunajukumu la kutii amri zake, na kwamba tusipotii
amri zake, tunakuwa tumeharibu maana nzima ya upendo wake, kwani tutajikuta
tumeingia motoni/jehanamu (Kinyume cha upendo).
Hata
katika familia, tumesikia mzazi pamoja na upendo alioonyesha kwa mtoto wake
toka yupo tumboni mpaka mtoto ameweza kujitegemea, endapo mtoto husika
akashindwa kumjali ( hili ndio jukumu linalokuja na upendo wa mzazi), basi
unaweza sikia mzazi huyo akitoa ‘laana’ au ‘akamwachia radhi’ mtoto wake
mwenyewe wa kumzaa.
Ni
wazi kuwa mara nyingi majukumu yanayoletwa na upendo huwa hayaelezwi wazi wazi,
hata hivyo katika mahusiano, mambo yafuatayo yanaweza kuwa sehemu ya matarajio
ambayo wapenzi wanaweza kuwa makini ili
waweze kuwapendeza wenzao. Kwa maana nyingine ni kuwa yafuatayo, ndio maeneo
ambayo mtu aliye kwenye mahusiano ni muhimu ‘acheze’ vema ili kulinda
mahusiano/penzi:-
Fedha: Katika swala la fedha, jambo kubwa
linalojitokeza ni namna ya kufanya maamuzi kuhusu matumizi ya fedha. Ni muhimu kuweka mikakati ya pamoja kwa mambo
ya msingi kimaisha , na kila mmoja kutilia maanani mipango hiyo, kabla ya kuamua
kutumia kipato chake kwa mambo ambayo pengine hayapo nje ya mipango ya kifedha
ya wawili nyie kama wapenzi. Bila shaka,
kuendana na aina yenu ya kipato, aina yenu ya maisha, kama wapenzi mtakuwa na
kiwango fulani cha fedha ambacho si busara mmoja wenu kuamua kutumia bila
kumtaarifu mwenzake , hata kama matumizi husika ni muhimu sana, na haijalishi
nani kazitafuta fedha husika.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz
Friday, February 28, 2014
MASIKINI YA MUNGU MTOTO HUYUUU...!!! KICHWA NA MWILI VYAUNGANA BAADA YA KUUNGUA MOTO
MTOTO Adolotea Njavike(1.4) ambae Kichwa na Kiwiliwili vimeungana baada ya kupata na ajali ya Moto akiwa na mama yake Mzazi. |
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz
BENKI YA DUNIA YAISIMAMISHIA UGANDA MISAADA
Hatua hiyo ya benki ya dunia
haikutarajiwa na wengi kwani taasisi hiyo mara nyingi hujiepusha
kuingilia masuala ya ndani ya kisiasa ya nchi wanachama au kuhusiana na
masuala kama haki za mashoga, kuepuka kuzishurutisha nchi wanachame wake
188.
Hata hivyo msemaji wa benki hiyo David
Theis amesema katika barua pepe kuwa wamesitisha mradi huo wa kuboresha
sekta ya afya ya Uganda hadi watakapoufanyia tathmini na kuhakikisha
malengo yake ya maendeleo hayataathiriwa na sheria hiyo mpya ya
kuharamisha ushoga.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz
AJALI, BASI LAGONGA TRENI, WANNE WAFARIKI
Basi la Bunda Express lililokuwa likitokea Dodoma kwenda Mwanza asubuhi ya leo limegonga Treni Eneo la Manyoni mkoani Singida. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz
Basi la Bunda Express lililokuwa likitokea Dodoma kwenda Mwanza asubuhi ya leo limegonga Treni Eneo la Manyoni mkoani Singida.
Kwa mujibu wa chanzo cha habari kutoka eneo la tukio kinasema kuwa watu wanne wamefariki dunia na kadhaa kujeruhiwa.
Majeruhi Tayari wamepelekwa kwenye Hospitali ya Wilaya ya Manyoni.
Majeruhi Tayari wamepelekwa kwenye Hospitali ya Wilaya ya Manyoni.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz
Chanzo: networkedblogs
Wednesday, February 26, 2014
HIKI NDICHO KINACHOENDELEA MSIBANI KWA DADA YAKE LADY JAY DEE...!!!
Msanii mkongwa wa Bongo Flava Lady Jay Dee amefiwa na dada yake Aitwaye Lucy Lameck Isambwa Mbibo
Lady Jay Dee Ameshare Taarifa Hizo za msiba wa dada yake kupitia mitandao yake ya kijamii
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz
SERIKALI YATANGAZA TAREHE YA USAILI KWA WAOMBAJI WA NAFASI ZA KAZI ZA KILIMO NA MIFUGO
Serikali
inapenda kuwaarifu waombaji wa nafasi za kazi kwa tangazo la tarehe 27
Novemba, 2013 wa kada za Kilimo, Mifugo, Uvuvi na Udereva kuwa usaili
utaanza tarehe 4 Machi, 2014 takriban katika mikoa yote Tanzania Bara na
Zanzibar.
Katibu
wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma Bw. Xavier Daudi
amesema hayo leo ofisini kwake wakati akiongea na baadhi ya wadau
waliomtembelea kwa lengo la kufahamu masuala mbalimbali ya uendeshaji wa
mchakato wa ajira serikalini.
Amesema
usaili huo unaoanza tarehe 4 Machi katika mikoa takribani yote nchini
utahusisha jumla ya wasailiwa 6,087 wa fani za Kilimo, Mifugo, Uvuvi na
udereva kwa kada ambazo sio za Maofisa. Amefafanua kuwa vigezo vya
kupanga mikoa ya usaili vimetokana na anwani ambazo waombaji
waliwasilisha katika barua zao za maombi husika ya kazi.
Daudi
alibainisha kuwa kila mwombaji aliyekidhi vigezo na kuchaguliwa kwa
ajili ya usaili anapaswa kwenda kufanyia usaili katika mkoa aliopangiwa
kama anwani yake inavyoonyesha katika tangazo kwenye tovuti ya
Sekretarieti ya Ajira, isipokuwa kwa waombaji wa mkoa wa Katavi wao
wataenda kufanyia usaili mkoa wa Rukwa na waombaji waliotumia anwani za
mkoa wa Singida wao watafanyia usaili mkoa wa Manyara kutokana na sababu
zisizozuilika.
Aliongeza
kuwa kwa mwombaji ambae hatazingatia anwani, siku na muda aliopangiwa
na kuamua kwenda mkoa mwingine tofauti na utaratibu uliopangwa ajue wazi
hatasailiwa kwa kuwa ratiba na idadi ya majopo ilishapangwa kwa kila
mkoa na haitabadilishwa ili kuweza kurahisisha kazi hiyo kukamilika kwa
ufanisi.
Subscribe to:
Posts (Atom)