Monday, December 30, 2013
Sunday, December 29, 2013
MENEJA WA WEMA SEPETU AHUSISHWA KWENYE UJUMBE WA JACKIE CLIEF ALIOUTUMA MASAA MACHACHE KABLA YA KUNASWA NA MADAWA YA KULEVYA
Yaelekea mwanadada Jackie alikuwa amejipanga kisawa sawa na alijitoa
muhanga na kujua lolote lingeweza kumpata kutokana na kazi aliyo kuwa
akifanya ya kubeba sembe.
Jackie alijipanga na kuamua kumuachia rafiki
yake kipenzi Martin Kadinda maagizo na wosia wake just incase ikatokea
akafariki. Jackie aliweza kuandika ujumbe huo kwenye status yake ya BBM
kama inavyo onekana hapa chini.
Tafadhari Like page yetu click Jambo Tz
Saturday, December 28, 2013
LUMBESA LA VIPODOZI FEKI LAKAMATWA IRINGA
Baadhi ya shehena za vipodozi zilizokamatwa na jeshi la polisi mkoa wa Iringa baada ya kushushwa katika roli katika makao makuu makuu ya jeshi mkoa wa Iringa. |
Kamanda
wa Jeshi la Polisi mkoa wa Iringa ACP Ramadhani Mungi akionyesha
shehena ya vipodozi vilivyokamatwa na jeshi hilo mkoani Iringa katika
makao makuu ya jeshi hilo jana. (Picha na Denis Mlowe) |
Friday, December 27, 2013
HII HAPA NDIO SIRI YA PINDA KUNUSURIKA
*Katibu Umoja wa Wanawake aadhirika kikaoni
*Wabunge 178 waomba kikao na Kinana
KATIKA
hali isiyo ya kawaida, Ijumaa iliyopita Waziri Mkuu Mizengo Pinda
aliponea chupuchupu kung’olewa uenyekiti wa kikao cha wabunge wa Chama
Cha Mapinduzi (CCM).
Kikao hicho (party caucus) kilifanyika baada ya hali ya hewa bungeni kuchafuka baada ya kuwekwa hadharani bungeni ripoti ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira iliyosomwa na Mwenyekiti wake James Lembeli.
Ripoti hiyo ilihusu tathmini ya upungufu kadha wa kadha uliojitokeza wakati wa utekelezaji wa Operesheni Tokomeza Ujangili, upungufu ulioibua mjadala mzito bungeni, na kusababisha mawaziri wanne kujiuzulu.
Mawaziri hao ni Khamis Kagasheki (Maliasili na Utalii), Emmanuel Nchimbi (Mambo ya Ndani), Shamsi Vuai Nahodha (Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa) na David David Mathayo (Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi). Hata hivyo habari zilizopatikana zilisema mawaziri hao waling’olewa kwa amri ya Rais Jakaya Kikwete.
*Wabunge 178 waomba kikao na Kinana
Kikao hicho (party caucus) kilifanyika baada ya hali ya hewa bungeni kuchafuka baada ya kuwekwa hadharani bungeni ripoti ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira iliyosomwa na Mwenyekiti wake James Lembeli.
Ripoti hiyo ilihusu tathmini ya upungufu kadha wa kadha uliojitokeza wakati wa utekelezaji wa Operesheni Tokomeza Ujangili, upungufu ulioibua mjadala mzito bungeni, na kusababisha mawaziri wanne kujiuzulu.
Mawaziri hao ni Khamis Kagasheki (Maliasili na Utalii), Emmanuel Nchimbi (Mambo ya Ndani), Shamsi Vuai Nahodha (Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa) na David David Mathayo (Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi). Hata hivyo habari zilizopatikana zilisema mawaziri hao waling’olewa kwa amri ya Rais Jakaya Kikwete.
Thursday, December 26, 2013
RATIBA YA LIGI KUU YA UINGEREZA LEO ALHAMISI
15:45 Hull City Vs Manchester United
18:00 Aston Villa Vs Crystal Palace
18:00 Cardiff City Vs Southampton
18:00 Chelsea Vs Swansea City
18:00 Everton Vs Sunderland
18:00 Newcastle United Vs Stoke City
18:00 Norwich City Vs Fulham
18:00 Tottenham Hotspur Vs West Bromwich Albion
18:00 West Ham United Vs Arsenal
20:30 Manchester City Vs Liverpool
18:00 Aston Villa Vs Crystal Palace
18:00 Cardiff City Vs Southampton
18:00 Chelsea Vs Swansea City
18:00 Everton Vs Sunderland
18:00 Newcastle United Vs Stoke City
18:00 Norwich City Vs Fulham
18:00 Tottenham Hotspur Vs West Bromwich Albion
18:00 West Ham United Vs Arsenal
20:30 Manchester City Vs Liverpool
Tafadhari Like page yetu click Jambo Tz
PAPA FRANCIS ATETEA WANYONGE WA VITA
Katika hotuba yake ya mwanzo ya Krismasi, Papa Francis amezungumza mjini Rome juu ya maeneo ya vita duniani.
Alitoa wito kwa pande zote zilizohusika na vita vya Syria ziruhusu msaada kufika kwa wanyonge.
Alisema:
"Maisha mengi yamevunjika katika vita vya Syria na kuchochea chuki na kulipiza kisasi.
Wacha tuendelee kumuomba Mungu
awaepushe wapendwa watu wa Syria na maafa zaidi, na kuziwezesha pande
zilizohusika na vita kumaliza ghasia na kuruhusu msaada ufike kwa wale
wanaouhitaji"
Papa Francis piya alitoa wito kwa
mapigano kusitishwa Sudan Kusini na aliwaomba viongozi wa kimataifa
kushughulikia zaidi yanayotokea Jamhuri ya Afrika ya Kati ambayo alisema
mara nyingi haitiwi maanani.
Akizungumza juu ya mamia ya wakimbizi
kutoka Eritrea waliozama karibu na kisiwa cha Utaliana cha Lampedusa
mwezi Oktoba, alieleza wasiwasi wake kuhusu wale wanaohatarisha kila
kitu ili kutafuta maisha bora.
Piya alizungumzia swala la ukatili majumbani, akitetea wanawake wanaopigwa.
Tafadhari Like page yetu click Jambo Tz
DIAMOND AMTAMBULISHA TENA WEMA, HIKI NDICHO ALICHOKISEMA....!!!
Tukio hilo lilitokea jana pale Leaders club kwenye show ya Diamond ambapo Wema Sepetu alipanda kwenye stage na kuongea na mashabiki waliofika kwenye show hiyo.
Kwenye hiyo show Diamond aliuliza,”Mnataka kumjua mchumba wangu”?
Show ilivyoendelea Diamond alitaka kuimba wimbo wa ukimwona akasema, “Nasikia ninayetaka kumuimbia wimbo huu yupo humuhumu ndani”.
Wema Sepetu akapanda kwenye stage wakaimba na kucheza wote.
Wednesday, December 25, 2013
HILI NDILO BARAZA LA MAWAZIRI LINALOTAKIWA
********
Baada ya kizaazaa cha wiki iliyopita ambapo mawaziri wanne
walipoteza kazi zao kutokana na kuwajibishwa kwa vitendo vya ukatili na
mauaji vilivyotokea wakati watendaji katika wizara zao walipokuwa
wakiendesha ‘Operesheni Tokomeza Ujangili’ nchi nzima, kinachosubiriwa
na wananchi hivi sasa ni Rais Jakaya Kikwete kuunda Baraza jipya la
Mawaziri.
Kutokana na udhaifu mkubwa katika utendaji ambao
kwa muda mrefu umeonyeshwa na mawaziri wengi katika Baraza la Mawaziri,
hatudhani kama kuna mwananchi hata mmoja anayemtarajia Rais Kikwete
kujaza tu nafasi za mawaziri aliowafukuza wiki iliyopita.
Nderemo na vifijo vilivyotokana na furaha ya
wananchi katika kila kona ya nchi baada ya mawaziri hao kuondolewa
katika nyadhifa zao ni ishara tosha kwamba hawamtarajii Rais Kikwete
kuishia hapo, isipokuwa kuwaondoa mawaziri wengine wengi ambao tayari
wamethibitika na hata kutajwa na chama chao cha CCM kuwa ni ‘mawaziri
mizigo’.
KHERI YA X-MASS NA MWAKA MPYA KWA WADAU WOTE WA JAMBO TZ
Tunapenda kuwatakia kheri ya Chistmas na Mwaka mpya wapenzi wasomaji wa blog hii na page yetu ya facebook.
WaTanzania hatuna budi kulinda amani ya nchi yetu na upendo miongoni mwetu
kwa gharama yeyote ile na bila kuyumbishwa au kutetereka ili tuweze
kuachia vizazi vyetu vijavyo Urithi ulio mwema kuliko wowote Ule.
TANZANIA yenye Amani, Upendo na Utulivu.
"MUNGU IBARIKI TANZANIA"
Subscribe to:
Posts (Atom)