Israel imekanusha madai hayo na Waziri
Mkuu wake Benjamin Netanyahu leo hii anatarajiwa kuendeleza kampeni
yake dhidi ya kufikia makubaliano ya nyuklia na Iran wakati
atakapokutana na Rais Vladimir Putin wa Urusi mjini Moscow.
Sunday, November 24, 2013
MAMA YAKE ZITTO KABWE AELEZEA SAKATA LA MWANAYE
Siku moja baada ya Kamati Kuu ya Chadema kumvua uongozi
aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu Taifa wa chama hicho, Zitto Kabwe, mama yake
mzazi, Shida Salum ametoa ya moyoni akieleza kuwa kilichomkuta mwanaye
kimefunika mabaya mengi yaliyopangwa afanyiwe.
“Kwa upande wangu naona kama ni ushindi kwa Zitto
kutokana na jinsi ninavyojua hali ilivyo, mambo yalikuwa ni mengi mno na
nikwambie tu, Zitto kuvuliwa uongozi kumefunika hayo yaliyokuwa
yamekusudiwa kufanywa dhidi yake. Nilikuwa naomba Mungu kila siku ili
afukuzwe Chadema,” alisema mama huyo wakati akizungumza na gazeti hili
nyumbani kwake Tabata, Dar es Salaam.
Shida Salum alisema kuwa Mungu amemnusuru mwanaye
na kusisitiza, “Watu walikaa na kutengeneza ripoti ya siri kuhusu Zitto
na kuiweka kwenye mtandao kisha kuituma kwa wanachama wa Chadema
wanaowafahamu.
Mpaka wanafikia hatua hiyo maana yake ni kwamba wamejaribu njia zote za kummaliza, lakini wameshindwa.”
Mpaka wanafikia hatua hiyo maana yake ni kwamba wamejaribu njia zote za kummaliza, lakini wameshindwa.”
Alisema kutokana na hali ilivyo hivi sasa
amemnyang’anya mwanaye kwa muda simu zake zote za mkononi, kompyuta
mpakato (Laptop) pamoja na iPad ili asiwasiliane na watu, kwa maelezo
kuwa wapo wenye nia mbaya wanaomsaka kumpa pole za kinafiki. “Kwa sasa
nataka mwanangu atulize akili.”
Shida Salum, mbali na kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya
Chadema, pia ni mwasisi wa Shirikisho la Vyama vya Watu Wenye Ulemavu
(Shivyawata) na Mwenyekiti wa Chama cha Watu Wenye Ulemavu wa Viungo
(Chawata)
SOMA KWA MAKINI ILE TAARIFA MAALUM YA CHADEMA KWA WATANZANIA JUU YA UAMUZI WA KAMATI KUU
Ndugu Wananchi, wanachama na viongozi wa CHADEMA,
Kamati
Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) iliyokutana Ubungo
Plaza, Dar es Salaam kuanzia asubuhi ya siku ya Jumatano ya tarehe 20
Novemba, 2013 hadi alfajiri ya leo Ijumaa tarehe 22 Novemba, 2013
imetafakari na kujadili kwa kina taarifa mbali mbali juu ya hali ya
kisiasa ndani na nje ya Chama chetu ambayo kwa muda mrefu imegubikwa na
tuhuma kubwa na nzito dhidi ya Chama chetu na viongozi wake wakuu, yaani
Mwenyekiti wa Taifa, Mheshimiwa Freeman Aikaeli Mbowe (MB), na Katibu
Mkuu, Dk. Wilbrod Peter Slaa. Tuhuma hizi zilikuwa na malengo na athari
ya kuwapaka matope na kuwachafua viongozi wakuu wa Chama na Chama
chenyewe, kutengeneza mtandao wa siri ndani na nje ya Chama ambao
hatimaye ungefanikisha sio tu lengo la kufanya mapinduzi nje ya
utaratibu wa kikatiba wa Chama, bali pia ungekipasua Chama vipande
vipande na hivyo kuua matumaini ya Watanzania juu ya uwezekano wa
kufanya mabadiliko ya kisiasa na kiuchumi na kijamii katika nchi yetu
kwa kukiondoa madarakani Chama cha Mapinduzi (CCM).
Ndugu Wananchi, wanachama na viongozi wa CHADEMA, Uchunguzi
wa Kamati Kuu umebaini kuwepo kwa mkakati mkubwa wa kutimiza malengo
hayo ambao umeandikwa katika waraka unaoitwa ‘Mkakati wa Mabadiliko
2013.’ Mkakati huu uliandaliwa na kikundi kinachojiita ‘Mtandao wa
Ushindi’ ambacho vinara wake wakuu ni wanne, yaani Naibu Katibu Mkuu na
Naibu Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Mheshimiwa Zitto
Zuberi Kabwe ambaye kwenye waraka huo anajulikana pia kama ‘MM’ au
‘Mhusika Mkuu’; mjumbe wa Kamati Kuu na mwanazuoni kutoka Chuo Kikuu cha
Dar es Salaam, Dk. Kitilla Mkumbo ambaye kwenye waraka anajulikana pia
kama M1; Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Arusha ambaye kwa sasa
amesimamishwa uongozi, Bwana Samson Mwigamba na ambaye kwenye waraka
anaitwa M3; na mtu mwingine ambaye hadi sasa jina lake halijajulikana
lakini kwenye waraka anajulikana kama M2 na anatajwa kuwa yuko ‘ukingoni
kupigwa nje’ katika mageuzi ya kiutendaji yanayoendelea katika
Sekretariat ya Chama hapa Makao Makuu.
Kwa
mujibu wa waraka wenyewe, “Mkakati huu umeandaliwa kwa pamoja na M2 na
M3 na kupitiwa na kurekebishwa na M1 ili upelekwe kwa MM kwa maoni ya
mwisho na kuanza utekelezaji.” Mbele ya Kamati Kuu, Dk. Mkumbo alikiri
kwamba MM au Mhusika Mkuu ni Naibu Katibu Mkuu Zitto Kabwe; M1 ni yeye
mwenyewe Dk. Mkumbo na M3 ni Bwana Mwigamba. Dk. Mkumbo alikataa kata
kata kumfahamu M2. Aidha, Dk. Mkumbo alikiri mbele ya Kamati Kuu kwamba
yote yaliyoandikwa katika ‘Mkakati wa Mabadiliko 2013’ yametoka kwenye
‘Mtandao wa Ushindi’ na hayajabadilishwa.
Thursday, November 21, 2013
HOFU YATANDA KAMATI KUU YA CHADEMA, KIKAO CHAFANYIKA CHINI YA ULINZI MKALI WA BLUE GUARD
********
Hali ya wasiwasi iligubika eneo kinapofanyika kikao cha Kamati
Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kilichoanza Dar es
Salaam jana.
Ulinzi mkali wa walinzi wa Chadema (Blue Guard),
uliimarishwa katika ukumbi wa Ubungo Plaza kinapofanyika kikao hicho
ambacho kinatarajiwa kumalizika leo, huku kukiwa na maagizo
yaliyoashiria kuwapo kwa mambo mazito.
Maazimio ya kikao hicho yanasubiriwa kwa hamu na
wafuatiliaji wa mambo ya siasa nchini kwani kinafanyika katika kipindi
ambacho chama hicho kikuu cha upinzani nchini kinapita katika misukosuko
na hasa ya malumbano baina ya makamanda wake wa juu.
MAZUNGUMZO YA NYUKLIA YA IRAN YAANZA
Catherine Ashton Mkuu wa Sera za Kigeni wa Umoja (kushoto) na Waziri wa mambo ya nje wa Iran Mohammad Javad Zarif wakiwa katika mkutano na waandishi wa habari mjini Geneva baada ya kushindwa kufikiwa kwa makubaliano. (10.11.2013).
Mazungumzo magumu yanaanza leo kati ya Iran na mataifa makubwa kutafuta makubaliano kwa mpango wa nyuklia wa Iran ambayo pia yatawaridhisha wanasiasa wa msimamo mkali huko Marekani, Israel na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Mazungumzo hayo yanafanyika Geneva wakati kukiwa na hali ya mvutano inayoongezeka Mashariki ya Kati ambapo waziri wa mambo ya nje wa Iran akiishutumu Israel kwa kujaribu kuvuruga mchakato huo kufuatia mirupuko miwili ya mabomu iliouwa takriban watu 23 nje ya ubalozi wa Iran mjini Beirut hapo jana.Wizara ya mambo ya nje ya Iran imeilaumu Israel na mamluki wake kwa kuhusika na miripuko hiyo.
WAZIRI NCHIMBI, MWAKYEMBE WAFANYA KIKAO NA WATENDAJI WAKUU WA WIZARA ZAO JIJINI DAR
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk
Emmanuel Nchimbi (kushoto-meza kuu) akizungumza na Watendaji Wakuu wa
wizara yake pamoja na wa Wizara ya Uchukuzi katika Kikao cha utendaji
kazi cha kuimarisha uhusiano kati ya wizara hizo kilichofanyika katika
Ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi jijini Dar es
Salaam. Kulia (meza kuu) ni Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe.
Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison
Mwakyembe (kulia-meza kuu) akizungumza na Watendaji Wakuu wa wizara yake
pamoja na wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi katika Kikao cha utendaji
kazi cha kuimarisha uhusiano kati ya wizara hizo kilichofanyika katika
Ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi jijini Dar es
Salaam. Kushoto (meza kuu) ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk
Emmanuel Nchimbi. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk
Emmanuel Nchimbi akizungumza na Watendaji Wakuu wa wizara yake pamoja na
wa Wizara ya Uchukuzi (hawapo pichani) katika Kikao cha utendaji kazi
cha kuimarisha uhusiano kati ya wizara hizo kilichofanyika katika Ukumbi
wa Mikutano wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi jijini Dar es Salaam.
Kulia ni Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe. Picha zote na Felix
Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
Wednesday, November 20, 2013
EMMANUEL ADEBAYOR AONESHA UTAJIRI WAKE, JUMBA LA KIFAHARI, MAGARI NA NDEGE
Mchezaji wa Tottenham Hotspur Emmanuel Adebayor ni mmoja kati ya wachezaji matajiri sana Africa na anamiliki nyumba kwao Togo,Ghana,UK na Marekani.
Adebayor mwenye miaka 29 ametoa picha zake zikionyesha magari yake ya kifahari, private jet na vitu vingine vingine.
Enjoy picha 15 kutoka kwa Adebayor ambaye siku chache zilizopita alikuwa kwenye harusi ya Peter wa P Square pamoja na Diamond Platnums.
WATU ZAIDI YA 50 WAFUKIWA BAADA YA JENGO KUPOROMOKA AFRIKA KUSINI
Watu
wawili wamefariki na wengine takriban watu 50 kukwama kwenye vifusi
baada ya paa ya jumba la maduka lililokuwa linajengwa kuporomoka nchini
Afrika Kusini.
Inaarifiwa watu 29 wameweza kuokolewa.
Taarifa zinazohusianaAfrika Kusini
Madaktari kutoka kampuni ya kibinafsi ya Netcare 911 walifika kutoa huduma ya kwanza katika eneo hilo la Tongaat Kaskazini mwa mji wa Durban.
Madaktari kutoka kampuni ya kibinafsi ya Netcare 911 walifika kutoa huduma ya kwanza katika eneo hilo la Tongaat Kaskazini mwa mji wa Durban.
"Shughuli hii itachukua mda mrefu. Itatuchukua muda kuwafikia wale waliokwama," alisema msemaji wa kampuni hiyo.
Hata hivyo ni mapema mno kujua sababu ya kuporomoka kwa jengo hilo.
Inaarifiwa watu wengine 26 wamepelekwa hospitalini wakiwa na majereha mabaya.
CHANZO BBC SWAHILI
LIST YA WASANII WALIOLIPWA PESA NYINGI DUNIANI 2012 - 2013
List mpya kutoka Forbes inahusisha wasanii waliolipwa pesa nyingi
duniani kwa kipindi cha June 2012 hadi June 2013 ambapo pesa hizo
zinatokana na mauzo ya album, show(tour) na vitu vingine.
Wakongwe bado wapo kwenye list na Justin Bieber pamoja na umri wake mdogo lakini bado ameendelea kubaki kwenye top 10 ya list hii. List kamili hii hapa.....
1. Madonna – $125 million
2. Lady Gaga - $80 million
3. Bon Jovi – $79 million
4. Toby Keith – $65 million
5. Coldplay – $64 million.
6. Justin Bieber – $58 million
7. Taylor Swift – $55 million
8. Elton John – $54 million
9. Kenny Chesney – $53 million
9. Beyonce – $53 million (tie)
11. Sean “Diddy” Combs – $50 million
12. Sir Paul McCartney – $47 million
13. Calvin Harris – $46 million
14. Jennifer Lopez – $45 million
15. Roger Waters – $44 million
16. Muse – $43 million (tie)
16. Rihanna – $43 million (tie)
18. Jay Z – $42 million
18. One Direction – $42 million (tie)
20. Dr. Dre – $40 million
20. Red Hot Chili Peppers ($40 million, tie)
22. Rolling Stones – $39 million (tie)
22. Katy Perry – $39 million (tie)
24. Tim McGraw – $33 million (tie)
25. Pink – $32 million (tie)
25. Tiësto – $32 million (tie)
MSIMU WA SIKUKUU UMEWADIA TANGAZA BIASHARA YAKO NASI KWA BEI NAFUU
Kuza biashara yako msimu huu wa sikuu, kwa kutangaza na http://jambotz8.blogspot.com/
Piga simu no:- 0687 221198/ 0715 221198/ 0766 221198
Piga simu no:- 0687 221198/ 0715 221198/ 0766 221198
UFARANSA YAIPIGA UKRAINE 3-0 NA KUFUZU KOMBE LA DUNIA.
Ufaransa imefanikiwa kufuzu kucheza
Kombe la Dunia baada ya kuigeuzia kibao Ukraine na kuichapa mabao
3-0. Awali Ukraine ilishinda kwa mabao 2-0 ikiwa nyumbani na kuweka
matumaini ya juu kusonga mbele katika mechi hiyo ya marudiano
ugenini.
Lakini leo kwa mabao ya Mamadou Sakho aliyefunga mawili na
Karim Benzema, Ufaransa imetinga fainali ya Kombe la Dunia. Ilionekana
ni vigumu kwa Wafaransa kusonga mbele baada ya kufungwa mabao 2-0 katika
mechi ya kwanza
Tuesday, November 19, 2013
KIWANDA CHA KUTENGENEZA VIYWAJI VIKALI CHAFUNGWA SHINYANGA
Kiwanda cha kutengeneza vinywaji cha Trully African kilichopo Mtanda Manispaa ya Shinyanga kimefungwa na Halmashauri ya mji huo kwa kutokidhi
viwango vya ubora.... mengi kuhusu sakata hili endelea kusikiliza radio Faraja Fm na kutembelea mtanda huu wa jambotz8.blogspot.com.
Story na Steve Kanyeph na Isaac Edward Kisesa
Story na Steve Kanyeph na Isaac Edward Kisesa
Subscribe to:
Posts (Atom)