Thursday, November 21, 2013

HOFU YATANDA KAMATI KUU YA CHADEMA, KIKAO CHAFANYIKA CHINI YA ULINZI MKALI WA BLUE GUARD

 

Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe (katikati) akiwa na walinzi wake akiwasili katika Jengo la Ubungo Plaza, Dar es Salaam, jana kushiriki kikao cha Kamati Kuu ya chama hicho. Picha na Michael Jamson 

********

Hali ya wasiwasi iligubika eneo  kinapofanyika kikao cha Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kilichoanza Dar es Salaam jana.


Ulinzi mkali wa walinzi wa Chadema (Blue Guard), uliimarishwa katika ukumbi wa Ubungo Plaza kinapofanyika kikao hicho ambacho kinatarajiwa kumalizika leo, huku kukiwa na maagizo yaliyoashiria kuwapo kwa mambo mazito.




Maazimio ya kikao hicho yanasubiriwa kwa hamu na wafuatiliaji wa mambo ya siasa nchini kwani kinafanyika katika kipindi ambacho chama hicho kikuu cha upinzani nchini kinapita katika misukosuko na hasa ya malumbano baina ya makamanda wake wa juu.


Maelekezo ya ulinzi


Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe aliwasili ukumbini hapo saa 5.20 asubuhi na baada ya kuingia, wapiga picha waliruhusiwa kuingia kuchukua kumbukumbu ya tukio hilo kwa dakika moja tu.


Waandishi wa habari hawakutakiwa kuingia na badala yake walielezwa kuwa wangepewa taarifa baadaye.


Wakati wapiga picha wakiwa ndani, mmoja wa wajumbe wa mkutano huo alitoka na kutoa maelekezo kwa walinzi wa Chadema akiwataka kuwa makini kutekeleza kazi yao watakapopewa amri ya kumwondoa mjumbe yeyote mkutanoni.


“Kama mkipewa amri ya kuondoa mtu ingieni na mtekeleze amri hiyo mara moja,” alisisitiza mjumbe huyo na kuingia ndani haraka. Walinzi hao zaidi ya 10, walipokea maelekezo hayo kwa kutikisa kichwa kuashiria kukubaliana na amri hiyo.


Kikao kufunguliwa


Kikao hicho ambacho kilifunguliwa dakika nane baada ya Mbowe kuwasili, kilipangwa kujadili mambo matatu jana.


Mmoja wa wajumbe wa mkutano huo ambaye hakutaka kutajwa jina lake alisema kingepitia taarifa za vikao viwili vya Kamati Kuu vilivyopita.


Suala jingine ambalo lilipangwa kujadiliwa jana ni ushiriki wa Chadema katika uchaguzi mdogo wa Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi Jimbo la Kiembesamaki, Zanzibar na kupitia taarifa ya fedha

MWANANCHI

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...