Mshikamano wa vyama vya upinzani katika kupinga Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba wa 2013 umehamia nje ya Bunge na sasa vyama hivyo vimetangaza kuanza kampeni ya kuuhamasisha umma kudai maridhiano kabla ya kuendelea na mchakato wa Katiba Mpya.
Jana
wenyeviti wa vyama hivyo; James Mbatia (NCCR-Mageuzi), Freeman Mbowe
(Chadema) na Profesa Ibrahim Lipumba (CUF) walikutana na waandishi wa
habari na kumtaka Rais Jakaya Kikwete kutosaini muswada huo kuwa sheria,
hadi pale kutakapokuwa na maridhiano ya pande zote husika.
Walisema
muungano wao ni mwanzo wa kuunganisha umma wa Watanzania kufanya uamuzi
wa kunusuru walichokiita "utekaji madaraka na mamlaka ya nchi kutoka kwa
wananchi" hivyo wanaitaka Serikali kurekebisha kasoro zinazojitokeza
katika mchakato huo.
Akitoa
tamko la pamoja kwa niaba ya viongozi wenzake, Profesa Lipumba alisema
wanachopigania ni kuurejesha mchakato wa Katiba Mpya mikononi mwa umma,
kwa maelezo kwamba suala hilo kwa sasa limehodhiwa na CCM.
"Rais
Kikwete asisaini muswada huu, aurejeshe bungeni ufanyiwe marekebisho
yenye kujenga kuaminiana na mwafaka wa kitaifa kwenye mchakato wa
mabadiliko ya Katiba. Hatutakwenda kumwona ila aurejeshe
bungeni,"alisema Lipumba na kuongeza: