Tabia mbaya! Staa wa Bongo Fleva, Nasibu
Abdul ‘Diamond’ amenaswa na msanii mwenzake, Esterlina Sanga ‘Linah’
wakiwa kwenye mapozi ya kimahaba ambayo yametafsiriwa vibaya.
Katika
tukio hilo lililojiri juzikati kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini
Tabora ndani ya Tamasha la Serengeti Fiesta, Diamond alishuhudiwa akiwa
amempakata Linah ndani ya basi huku mikono ya jamaa huyo ikishika
maeneo nyeti.
Mara baada ya kutimba uwanjani hapo wakitokea hotelini
tayari kwa kufanya shoo, Diamond na Linah walibaki kwenye basi wakiwa
wamepakatana na hata msichana huyo alipomaliza shoo yake kali mishale ya
saa 3: 00 usiku, alirejea mikononi mwa Diamond ambaye alimpachika
mapajani.