Uamuzi na msimamo wa Japan umetangazwa
jana jijini Dar es Salaam na Waziri wa Uchumi, Biashara na Viwanda wa
nchi hiyo, Toshimistu Motegi alipokutana na kufanya mazungumzo na Rais
Jakaya Kikwete, Ikulu.
Taarifa ya Ikulu iliyosambazwa na
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, ilimnukuu Motegi akisema: "Kwa kuanzia
kampuni mbili za Honda na Panasonic zimekubali kujenga viwanda nchini,
kimoja kwa ajili ya kutengeneza pikipiki za Honda na kingine kwa ajili
ya kutengeneza vifaa vya umeme."
Akaweka msisitizo: "Huu ni mwanzo tu
Mheshimiwa Rais (Kikwete) kwa sababu kama nilivyosema kuwa tunataka
Tanzania kuwa nchi ya mfano ya uwekezaji wa Japan katika eneo hili la
dunia, na namna hiyo kwa pamoja tutakuwa tumeshirikiana katika kuongeza
ajira kwa wananchi wa Tanzania."
Sunday, August 11, 2013
SERIKALI YADAIWA KUMGEUKA DR ULIMBOKA YADAI AMEFICHA USHAHIDI WA KUTEKWA KWAKE
SIKU chache baada ya Mahakama ya Kisutu kumwachia mtu aliyedaiwa kumteka na kumtesa kiongozi wa Jumuiya ya Madaktari nchini, Dk. Steven Ulimboka, serikali imemshukia daktari huyo na kudai ndiye chanzo cha kukwama kwa dola kukamata watu waliomteka.
Jana Mwendesha Mashitaka Mkuu wa Serikali (DPP), Eliazer Feleshi, alidai kuwa vyombo vya dola vimeshindwa hadi sasa kuwakamata waliohusika katika shambulio hilo kutokana na Dk. Ulimboka kukwepa kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi.
Feleshi ambaye jana aliambatana na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Said Mwema, katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, alidai lawama zinazosukumwa kwa Jeshi la Polisi kwa madai ya kushindwa kuwakamata waliomtendea unyama daktari huyo hazina msingi, kwa kuwa mhusika mwenyewe hajafika polisi, licha ya kuitwa mara nyingi kutoa maelezo.
Alisema kama Dk. Ulimboka angetoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi kungekuwa na mafanikio makubwa katika kuwasaka na hata kuwatia mbaroni waliohusika katika unyama huo.
“Kila mara mmekuwa mkilaumu polisi wanashindwa kukamata wahalifu lakini tutakamataje kama wenye ushahidi hawataki kutoa ushirikiano?
Kwa mfano mdogo tu ni ‘ishu’ (suala) ya Dk. Ulimboka, hadi leo hajatoa taarifa lakini polisi wanaendelea kusakamwa na kutukanwa tu,” alisema.
Hata hivyo, wakati Feleshi akitoa kauli hiyo, Dk. Ulimboka katika andiko lake alilolitoa mara tu baada ya kurejea nchini kutoka Afrika Kusini alikopelekwa kwa ajili ya matibabu, alimtaja mtu anayeaminika kuwa mfanyakazi wa Idara ya Usalama wa Taifa, Ramadhani Ighondu, kuwa ndiye aliyemteka na kumtesa.
Ulimboka akimtumia Wakili Nyaronyo Kicheere alisema Ighondu na wenzake ni mhusika mkuu katika unyama aliofanyiwa, kauli ambayo imekanushwa mara kadhaa na serikali.
Mapema wiki hii, raia wa Kenya, Joshua Mulundi, aliyekuwa akikabiliwa na tuhuma za kumteka na kumtesa Dk. Ulimboka aliachiwa na Mahakama ya Kisutu baada ya DPP Feleshi kumfutia shitaka. Hata hivyo Mulundi alikamatwa tena na sasa amefunguliwa mashitaka ya kutoa maelezo ya uongo kwa polisi.
KUTOKA KWENYE MTANDAO WA DAILYMAIL UINGEREZA:SHEIK PONDA AHUSISHWA NA KESI YA MABINTI WA UINGEREZA WALIOMWAGIWA TINDIKALI
Sheikh Ponda Issa who is suspected of inciting the attack on Kirstie Trup and Katie Gee was shot by police in Tanzania's capital last night
A radical Muslim preacher wanted in
connection with an acid attack on two British teenagers in Zanzibar has
been shot by police, it was reported.
Sheikh
Issa Ponda Issa was hit in the shoulder with a tear gas canister as he
tried to escape from officers after being cornered near Tanzania's
capital Dar es Salaam, The Sunday Mirror said.
JAPAN KUJENGA KIWANDA CHA PIKIPIKI TANZANIA
WAINGEREZA WALIOMWAGIWA TINDIKALI WAITESA SERIKALI
Siku tano baada ya raia wawili wa Uingereza kumwagiwa tindikali visiwani Zanzibar, Serikali kupitia vyombo vyake vya uchunguzi imeibuka na kueleza kuwa bila wananchi kutoa taarifa za ushahidi wa uhalifu wa aina mbalimbali, ni vigumu kuwabaini wahusika. (HM)
Kauli hiyo ilitolewa kwa pamoja jana
na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Said Mwema, Mkemia Mkuu wa
Serikali, Profesa Samwel Manyele na Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali
(DPP) Eliezer Feleshi, katika mkutano wao na waandishi wa habari,
uliolenga kueleza mikakati ya kupambana na matumizi yasiyo sahihi ya
tindikali nchini.
Katika ufafanuzi wao walisema, "Kutoa taarifa ya uhalifu wa jambo lolote siyo hiari, ni jukumu la kisheria na kikatiba," huku Feleshi akitolea mfano jinsi Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari nchini, Dk Steven Ulimboka alivyoshindwa kutoa ushahidi wa tukio lililomkuta la kutekwa, kupigwa na kisha kutupwa katika Msitu wa Mabwepande, hivyo kufanya uchunguzi kuwa mgumu.
Katika ufafanuzi wao walisema, "Kutoa taarifa ya uhalifu wa jambo lolote siyo hiari, ni jukumu la kisheria na kikatiba," huku Feleshi akitolea mfano jinsi Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari nchini, Dk Steven Ulimboka alivyoshindwa kutoa ushahidi wa tukio lililomkuta la kutekwa, kupigwa na kisha kutupwa katika Msitu wa Mabwepande, hivyo kufanya uchunguzi kuwa mgumu.
Saturday, August 10, 2013
NDEGE YA KIJESHI YALIPUKA NA KUTEKETEA KWA MOTO WAKATI IKITUA KWA DHARURA.
Ndege hiyo ilikuwa ya jeshi la Ethiopia.MOJA YA NDEGE ZA NCHI YA SOMALIA.PICHA YA NDEGE ZA JESHI YA MAKTABA SIO YA SOMALIA.
NDEGE ya kijeshi imelipuka na kuteketea nchini
Somalia baada ya kutua kwa dharura katika uwanja wa kimataifa wa ndege
mjini Mogadishu.
Inasemekana kuwa ndege hiyo ilikuwa ya jeshi la Ethiopia.
Kuna ripoti kuwa ndege ilikuwa imebeba zana za kivita.
Wafanyakazi katika uwanja huo wa ndege waliel
ezea kusikia milipuko kadhaa huku moto ukienea kwa ndege hiyo.
JESHI LA POLISI LATANGAZA DAU LA MILIONI 10 KWA MTU ATAKAYEWATAJA WATU WALIOWAMWAGIA TINDIKALI WAZUNGU
Zanzibar, Tanzania — Kamanda wa Polisi, Kamishna Musa
Ali Musa amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeahidi kutoa Shilingi
milioni 10/= kwa mtu yeyote atakayetoa taarifa zitakazofanikisha kukamatwa kwa
watu waliowashambulia mabinti wawili kutoka Londona, Uingereza, Kirstie Trup na
Katie Gee.
Mabinti hao walishambuliwa kwa tindikali usoni, kifuani na mikononi siku ya Jumatano walipokuwa njiani kuelekea kwenye chakula cha jioni.
Mabinti hao walishambuliwa kwa tindikali usoni, kifuani na mikononi siku ya Jumatano walipokuwa njiani kuelekea kwenye chakula cha jioni.
Friday, August 09, 2013
JAJI MUTUNGI AANZA KUTUMA SALAMU ZA UTENDAJI KAZI WAKE ....!!!
********
Dodoma. Msajili mteule wa Vyama vya Siasa
nchini, Jaji Francis Mutungi amewataka Watanzania kutulia na kusubiri
utendaji wake atakapokabidhiwa rasmi jukumu hilo jipya alilopewa na Rais
Jakaya Kikwete.
Mutungi aliteuliwa kushika wadhifa wa msajili wa
vyama vya siasa kuchukua nafasi ya John Tendwa ambaye amestaafu. Tendwa
aliiongoza taasisi hiyo kwa miaka 13.
Mutungi alisema: “Ninafahamu nina majukumu mazito
mbele yangu, lakini siwezi kusema chochote kwa kuwa sijakabidhiwa rasmi
ofisi. Ninachotaka kusema ni kwamba nitakuwa mtumishi wa kila mmoja.”
MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL ASHIRIKI SWALA YA SIKUKUU YA IDDI KITAIFA MKOANI TABORA
SIMBA KUADHIMISHA SIMBA DAY KESHO TEREHE 10.
KESHO, Jumamosi tarehe 10 Agosti mwaka 2013, klabu ya soka
ya Simba itaadhimisha kile kinachoitwa Siku ya Simba (SIMBA DAY) katika Uwanja
wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Utaratibu wa kuwa na Simba Day ulianzishwa na klabu kwa
lengo la kuwa na siku ambapo wapenzi, wanachama, viongozi, wachezaji wa zamani
na wa sasa pamoja na watu wengine mashuhuri, hukutana kwa pamoja na
kusherehekea klabu ambayo imewafanya wawe wamoja pamoja na tofauti nyingi
walizonazo.
Mwaka huu, shughuli hiyo itafanyika katika Uwanja wa Taifa
jijini Dar es Salaam. Pamoja na mambo mengine, Simba SC inatarajiwa kucheza
mechi ya kirafiki na klabu ya soka ya Sports Club Villa kutoka nchini Uganda.
Katika kusherehesha tukio hilo, wasanii maarufu kama vile
Juma Nature, Tunda Man na Snura maarufu kwa jina la ‘Mama Majanga’ watatumbuiza
uwanjani hapo.
MUME WA JOYCE KIRIA, HENRY KILEWO AWALIZA WATU KWENYE MKUTANO MABIBO SAHARA
kiukweli inasikitisha, lakini bado alisisitiza kwa kusema 'hakuna dhambi kubwa hapa duniani kama uoga' na ' watatupiga kwa mabomu na watatu ua kwa risasi lakini na wao watakufa kwa presha ya dhambi
WANYARWANDA 520 WATII AGIZO LA RAIS KIKWETE LA KUONDOKA NCHINI
Zikiwa zimesalia saa 48 kabla ya kumalizika kwa muda uliotolewa na Rais Jakaya Kikwete kwa wahamiaji haramu kuondoka nchini au kuhalalisha ukaazi wao na wenye silaha kuzisalimisha, makundi ya wahamiaji hao, yameanza kuondoka kwa hiari.
Wastani wa wahamiaji haramu 150 wanaendelea kujiandikisha kuvuka mpaka katika Kituo cha Rusumo, Ngara mkoani Kagera kutekeleza agizo hilo.
Ofisa Uhamiaji wa Kituo cha Rusumo, Samweli Mahirane alisema mpaka sasa Wanyarwanda 520 wameshaondoka katika maeneo mbalimbali ndani na nje ya Ngara na kurejea makwao huku Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Fabian Massawe akisema silaha 17 za aina mbalimbali zimesalimishwa.
Mahirane
alisema wahamiaji hao wanatokea katika vijiji vya Wilaya za Ngara,
Karagwe, Kyerwa, Biharamulo na Geita pamoja na Runzewe na wamekuwa
wakiishi katika maeneo hayo bila vibali halali. (HM)
Aliwahakikishia wahamiaji hao usalama katika mataifa yao kwani hivi karibuni Serikali ya Rwanda ilikubali kuwapokea hata walio na mifugo kwa masharti kuwa ndani ya kipindi kifupi wataipunguza kwa kuiuza na kuboresha maisha yao.
"Rwanda wanahitaji mifugo michache, hivyo walio na mingi wanatakiwa kuipunguza kwa kuuza na kujenga makazi bora ikiwa ni pamoja na kuhifadhi ama kulinda mazingira ya nchi hiyo," alisema Mahirane. Chanzo: mwananchi
MOURINHO: HATUTAKATA TAMAA MPANGO WA KUMSAJILI ROONEY...!!!
Chelsea tayari walishatuma ofa mbili ambazo zimekataliwa na Manchester United, ofa ya mwisho inayotajwa kuwa ni zaidi ya paundi million 25 ilitumwa jumapili. Lakini Mourinho alisema: "Hatuna kizuizi cha muda kwenye suala hili.
'Tumemuona Rooney kama ni mchezaji ambaye tungependa kuwa nae. Tumefanya kila kitu katika utaratibu unaopaswa na tutafanya hivyo mpaka siku ya mwisho ya usajili. Tunafnya kila kitu tukizingatia sheria, kutoa ofa rasmi kwa klabu moja kwa moja.
'Hakujawahi kuwepo kwa mawasiliano na mchezaji, hakijatokea kitu kama hicho. Tusubiri tuone kama mambo yatabadilika.'
Rooney inaaminika kwamba amemwambia kocha wake David Moyes kwamba anataka kuondoka, lakini United imekuwa ikisisitiza kwamba hauzwi. Chanzo: shaffihdauda
Thursday, August 08, 2013
WAPINZANI WACHEZEA KICHAPO KIKALI KIBONDO....!!!
Katika hali inayothibitisha ule usemi wa mwanamuziki Chameleon wa Uganda kuwa "fitina yako bahati yangu" wapinzani wamechezea kichapo cha mwaka kwenye Halmashauri ya wilaya ya Kibondo baada ya CCM kushinda kwenye nafasi zote za kuongoza Halmashauri hiyo, ushindi uliowaacha midomi wazi wapinzani waliokuwa wakisubiri kufaidi kwenye ugomvi wa madiwani wa CCM wilayani hapo.
Diwani wa CCM Ndugu Emily Msanya kuibuka Mwenyekiti wa Halmashauri baada ya kupata kura 14 kati ya 17 zilizopigwa na Makamu Mwenyekiti ni Apronary Mazinda ambaye pia alishinda kwa kura 14 kati ya 17.
Kuchaguliwa kwa madiwani hao na ushindi huo wa CCM kwenye ngome ya upinzani ambapo Mbunge wa jimbo hilo ni Ndg. Mkosamali wa NCCR-Mageuzi ni uthibitisho dhahiri kuwa CCM ina mkakati mkubwa wa kuzidhibiti ngome zote za upinzani nchini kuelekea uchaguzi wa 2014 na 2015.
MUME WA PILI WA WASTARA AIBUKA, ADAI WASTARA NI MKEWE....!!!
Na Issa Mnally
MIEZI nane baada ya kufariki dunia mumewe Juma Kilowoko ‘Sajuki’, ...
hatimaye mume wa pili wa staa wa filamu za Kibongo, Wastara Juma aitwaye Ahmed Kushi ameibuka na kudai kwamba anatambua kwamba staa huyo bado ni mkewe na anataka ampatie mwanaye aliyezaa naye.
Kwa muda mrefu kulikuwa na taarifa kuwa Wastara aliachana na mwanaume huyo kwa talaka kabla ya kuolewa na Sajuki lakini kuibuka kwake na madai kuwa bado mwanadada huyo ni mkewe kumezua mshangao mkubwa.
MADAI YA KUSHI
Akizungumza na gazeti hili hivi karibuni, Kushi alifunguka kwa mara ya kwanza kuwa yeye na Wastara walifunga ndoa ya Kiislamu mwaka 2000 na kujaliwa kupata mtoto mmoja wa kiume aitwaye Fares.
Alisema: “Kisheria bado ni mke wangu kwa kuwa nilikuwa nimempa talaka moja tu wala hazikufika tatu,” alisema Kushi na kudai kwamba ndoa yake na staa huyo ilidumu kwa mwaka mmoja na nusu na kuvunjika kutokana na kutawaliwa na migororo.
MIEZI nane baada ya kufariki dunia mumewe Juma Kilowoko ‘Sajuki’, ...
hatimaye mume wa pili wa staa wa filamu za Kibongo, Wastara Juma aitwaye Ahmed Kushi ameibuka na kudai kwamba anatambua kwamba staa huyo bado ni mkewe na anataka ampatie mwanaye aliyezaa naye.
Kwa muda mrefu kulikuwa na taarifa kuwa Wastara aliachana na mwanaume huyo kwa talaka kabla ya kuolewa na Sajuki lakini kuibuka kwake na madai kuwa bado mwanadada huyo ni mkewe kumezua mshangao mkubwa.
MADAI YA KUSHI
Akizungumza na gazeti hili hivi karibuni, Kushi alifunguka kwa mara ya kwanza kuwa yeye na Wastara walifunga ndoa ya Kiislamu mwaka 2000 na kujaliwa kupata mtoto mmoja wa kiume aitwaye Fares.
Alisema: “Kisheria bado ni mke wangu kwa kuwa nilikuwa nimempa talaka moja tu wala hazikufika tatu,” alisema Kushi na kudai kwamba ndoa yake na staa huyo ilidumu kwa mwaka mmoja na nusu na kuvunjika kutokana na kutawaliwa na migororo.
Subscribe to:
Posts (Atom)