UPANDE
wa Jamhuri katika kesi ya jengo refu la ghorofa 18 lililojengwa jirani
na Ikulu bila kufuata utaratibu unatarajia kuita mashahidi 13 na
vielelezo 20 kuthibitisha mashtaka dhidi ya vigogo walioruhusu ujenzi
huo.
Hayo yalielezwa jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na Wakili wa Serikali kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, Leonard Swai.
Hayo yalielezwa jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na Wakili wa Serikali kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, Leonard Swai.
Alikuwa akisoma maelezo ya awali ya kesi hiyo mbele ya Hakimu Mkazi Sundi fimbo.
Swai alisema kesi hiyo itaanza kusikilizwa Agosti 7 mwaka kwa ajili ya mashahidi wa upande wa mashtaka kutoa ushahidi wao.
Washitakiwa katika kesi hiyo ni Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Makumba Kimweri na Msanifu Mkuu wake Richard Maliyaga.