Askari
saba wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), waliouawa
katika jimbo la Darfur nchini Sudan, wanatarajiwa kuagwa leo kwenye
viwanja vya makao makuu ya jeshi hilo.
Miili
ya wanajeshi hao iliwasili nchini juzi kwa ndege maalumu katika Uwanja
wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu J. K Nyerere, Terminal One na kwenda
kuhifadhiwa kwenye Hospitali ya Rufaa ya Lugalo jijini Dar es Salaam.
Wanajeshi
waliouawa ni Sajenti Shaibu Othuman, Koplo Oswald Chaula, Koplo Mohamed
Juma, Koplo Mohamed Chikilizo, Rodney Ndunguru, Peter Werema na
Fortunatus Msofe.
Taarifa
kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana na Kurugenzi ya Habari na
Uhusiano, Makao Makuu ya JWTZ, ilieleza kuwa askari hao wataagwa leo na
shughuli hiyo itahudhuriwa na familia, makamanda wa jeshi na viongozi wa
Serikali.