Friday, July 19, 2013

SERIKALI YASISITIZA KUWA "KODI YA LINE ZA SIMU" IKO PALE PALE...!!!


Waziri wa Fedha, William Mgimwa, amesisitiza uamuzi wa Serikali kuendelea kutoza Sh 1,000 kwa kila mwezi kwa laini ya simu, licha ya kampuni za simu na wanasiasa kupinga.

Akizungumza na mwandishi juzi, Mgimwa alikumbusha wanaolalamikia kodi hiyo, kwamba suala la ulipaji kodi kwa taasisi au watu binafsi, ni la kisheria kulingana na mapato yao na hali halisi iliyopo.

Pia alieleza kushangazwa na matangazo ya baadhi ya kampuni kuhusu utozwaji kodi wananchi akisema wananchi ndio wanataka barabara, maji na umeme vijijini na kodi hizo zinakwenda kutumika huko.

Kwa mujibu wa Mgimwa, kodi ya laini za simu na ya intaneti, imetengwa ikatumike kusaidia maji na uwezo wa Serikali kupeleka elimu vijijini jambo ambalo ni la maendeleo.

MAGAZETI YA LEO IJUMAA JULAI 19, 2013

MASISTER BANDIA WAKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA ...!!!

Wanawake watatu wamekamatwa kwa madai ya kujaribu kusafirisha dawa za kulevya kupitia uwanja wa ndege wakiwa wamevalia kama masista.
 
Wasafirishaji hao walisimamishwa wakati wakiwasili kwenye kituo maarufu cha mapumziko nchini Colombia, sababu polisi walifikiri kwamba mavazi yao hayakuwa yakionekana halisia.
Maofisa waligundua kwamba kila mwanamke kati yao alikuwa na zaidi ya kilo 4 za cocaine zikiwa zimefungwa katika miguu yake.

Wakiwaongezea fedheha katika mashitaka, wasafirishaji hao walipangwa mstari mbele ya waandishi wakiwa bado wamevalia mavazi yao ya kituko kuficha ukweli.

LOWASSA AMCHAMBUA RAIS KIKWETE...!!!


Na Swahili TV
Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa  Edward Lowassa, amemsifia Rais  Jakaya Kikwete kuwa ameweza kuifanya Tanzania kupata heshima  katika ulingo wa kimataifa, aliyasema hayo wakati akihojiwa na Swahili TV jijini Washington DC.

“Ni hivi karibuni  tu  Rais Xi Jinping wa China, Rais Obama na Rais mstaafu wa Marekani  George W.Bush  walikuwa nchini Tanzania, hii inaonyesha kuwa Tanzania iko juu katika medani za kimataifa” alisema Mheshimiwa Lowassa.

TAARIFA MAALUM YA TFDA KWA UMMA KUHUSU UTHABITII WA DAWA AINA YA 'DICLOFENAC' ILIYODAIWA KUWA NA MDHARA MWILINI..!

1.Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) ina jukumu la kulinda na kudumisha afya ya jamii kwa kuhakiki ubora, usalama na ufanisi wa vyakula, dawa, vipodozi na vifaa tiba.

2. Hivi karibuni, TFDA imepokea taarifa ya kuwepo kwa hofu juu ya usalama wa dawa aina ya Diclofenac kupitia mitandao ya simu na vyombo vya habari. Kufuatia taarifa hiyo, TFDA inapenda kutoa ufafanuzi kama ifuatavyo:
a. Diclofenac ni dawa iliyoko kwenye kundi la dawa zinazojulikana kitaalam kama “Non – Steroidal Anti-inflammatory Drugs”(NSAIDs). Dawa hizi hutumika kutuliza maumivu na kuondoa uvimbe unaosababishwa na



magonjwa mbalimbali. Magonjwa hayo ni pamoja na magonjwa ya viungo, mifupa, uvimbe wa fizi na maumivu ya kichwa.

b. Mamlaka imesajili dawa ya Diclofenac kutoka makampuni mbalimbali ndani na nje ya nchi baada ya kutathmini ubora, usalama na ufanisi wake. Hata hivyo Diclofenac, kama ilivyo kwa dawa nyingine, ina madhara yanayofahamika. Kwa baadhi ya wagonjwa Diclofenac inaweza kusababisha vidonda vya tumbo, kuumwa kichwa, kuharisha, kutapika na kuwashwa mwili.



c. Pamoja na madhara yaliyoainishwa hapo juu, hivi karibuni imetolewa taarifa na Mamlaka ya udhibiti wa dawa ya nchi za Umoja wa Ulaya (European Medicines Agency) kwamba watu wenye matatizo ya moyo na shinikizo la damu, kisukari, waliowahi kupata kiharusi, wenye lehemu (cholesterol) nyingi kwenye damu, mshituko wa moyo na wanaovuta sigara wanaweza kupata matatizo kwenye moyo na mfumo wa damu ikiwa watatumia Diclofenac kwa kiwango kikubwa na kwa muda mrefu.

Thursday, July 18, 2013

HUYU NDIYE STAA WA FILAMU BONGO ANUSURIKA KUFA KATIKA AJALI YA GARI...!!!

STAA wa filamu Bongo, Jacqueline Pentzel amesema amenusurika kifo baada ya kupata ajali ya gari hivi karibuni.

Akizungumza na mwandishi wetu, Jacqueline alisema ajali hiyo ilitokea maeneo ya Mbezi alipokuwa akielekea nyumbani kwa mama yake, Mbezi jijini Dar akiwa kwenye gari lake dogo, aliligonga kwa nyuma gari aina ya DCM.

“Ni ajali ya ajabu kweli niliipata, maana DCM limefunga breki za ghafla mbele yangu na mimi nilikuwa nimejisahau nikalivaa ila namshukuru Mungu kwa kuwa sijaumia ila gari langu tu ndiyo limeharibika vibaya kwenye shoo ya mbele,” alisema Jacqueline.

WASTARA JUMA "NAHITAJI MUME NA SI MWANAUME WA KUPITA"

 
 
STAA wa filamu za Kibongo, Wastara Juma amesema hana haraka ya kuolewa kwani anahitaji mume na si mwanaume  wa kupita

Akizungumza na mwandishi wetu hivi karibuni, Wastara alisema kwa sasa yupo huru kutoka na mtu yeyote ampendaye kutokana na sheria na dini inavyosema ila kwa sasa shughuli za kuigiza zimembana.
 
‘Nahitaji mume na si mwanaume  wa kupita,  awe mvumilivu, mchapakazi pia awe na hofu ya Mungu. Kwa sasa nafanya filamu zangu kama kumuenzi marehemu mume wangu,” alisema Wastara. 
Na GPL

UJUE UKWELI WA DAWA ZA KULEVYA WALIZOKAMATWA NAZO MASOGANGE NA MWENZAKE, ADHABU YAO MIAKA 20 AU KIFUNGO CHA MAISHA


 
 Mellis Edward kushoto na Agness Masogange kulia waliokamatwa  na madawa ya kulevya nchini Afrika kusini
****
BAADA ya kukamatwa na dawa za kulevya nchini Afrika Kusini, msanii anayeshiriki katika video za wasanii wa muziki wa bongo fleva, Agnes Jerald 'Masogange' na mwenzake Melisa Edward, ukweli umeibainika kwamba dawa walizokamatwa nazo ni za kutengenezea dawa za kulevya, ambazo hazipatikani nchini na hazina matumizi yoyote.
Kupitia taarifa rasmi zilionesha kuwa, Chemical bashirifu ndiyo aina ya dawa walizokamatwa nazo nchini humo, ambapo wasanii hao walikamatwa nchini Afrika Kusini wakitokea Tanzania.
Akizungumza ofisini kwake Dar es Salaam leo Kamishina wa Tume ya Kuratibu na Kuthibiti Dawa za Kulevya nchini, Christopher Shekiondo alisema kwamba kwa mujibu wa sheria za nchi, dawa walizo kamatwanazo wasichana hao zinatumika kutengenezea dawa za kulevya, ambapo adhabu yao ni sawa na mtu aliyekamatwa na dawa za kulevya.

MAGAZETI YA LEO ALHAMIS JULAI 18, 2013 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

.
.

AZAM YAZIPA YANGA, SIMBA SHILINGI MIL 280





Mwenyekiti wa Simba, Aden Rage.
Na Saleh Ally
UONGOZI wa kampuni ya Bakhresa inayomiliki klabu ya Azam umemwaga dola milioni moja (zaidi ya Sh bilioni 1.6) ili kupata haki ya udhamini wa Ligi Kuu Bara kama warushaji wa matangazo ya televisheni.

Kutokana na kumwaga fedha hizo, kampuni hiyo kupitia kituo chake kipya cha televisheni yake ya Azam TV, kitakachoanza kurusha matangazo hivi karibuni, kitapewa haki ya kuonyesha mechi zote za Ligi Kuu Bara. 
Kampuni hiyo iliyokuwa inapambana na Supersport ya Afrika Kusini iliyokuwa tayari kutoa dola 500,000 imeihakikishia bodi ya ligi hiyo kuwa iko tayari kutoa fedha hizo na kila klabu zikiwemo Yanga na Simba zitapata Sh milioni 140 kila moja kwa msimu.

CHADEMA YATUPA KOMBORA JIPYA TENA....!!!

 

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimefanikiwa kunasa siri za mipango ya hujuma zilizokuwa zimeandaliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi mdogo wa udiwani katika kata nne za Jiji la Arusha, Tanzania Daima Jumatano limebaini.

Habari kutoka vyanzo mbalimbali vya kuaminika, zimebainisha kuwa CHADEMA katika uchaguzi huo kilifanikiwa kushinda kata hizo baada ya kuvunja ngome ya CCM iliyok
uwa ikiongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Mwigulu Nchemba.

Kwa mujibu wa habari hizo, mipango karibu yote iliyokuwa ikifanywa na CCM, ikiwemo halali na haramu, ilivuja na kufika mikononi mwa wapinzani wao ndani ya muda mfupi hata kabla ya utekelezaji.

Imedaiwa kwamba baadhi ya watu waliokuwa katika kambi ya CCM, waliamua kwa siri kufichua mipango hiyo na kuifikisha kwa mahasimu wao kutokana na kile kilichodaiwa kuchoshwa kushiriki katika mambo ya kidhalimu.

Habari zinasema maofisa kadhaa wa CCM ambao wamekuwa wakiratibu na kusimamia mipango karibu yote miovu dhidi ya wapinzani, waliamua kwenda kinyume na makubaliano hayo, na kwa njia ya siri wakafanikiwa kutoa mpango mzima hadharani.

KAULI YA BAN K-MOON JUU YA MAUAJI YA ASKARI WA JWTZ DARFUR


Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UNO), Ban K-Moon(pichani chini), amesema amesikitishwa na kuhuzunishwa na mauaji ya askari saba wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), lililofanywa na waasi wa Sudan Julai 13, mwaka huu.

Askari hao wa JWTZ waliokuwa Darfur, Sudan ya Kusini kulinda amani kwa mujibu wa UNO, walishambuliwa na waasi hao karibu na kambi ya Manawashi eneo la Khor Abeche, mji wa Darfur Jimbo la Nyala ambapo pia askari wengine 17 walijeruhiwa baadhi yao vibaya.

Katika salamu zake hizo kupitia kwa Msemaji wake, Katibu Mkuu huyo wa Uno, ameelezea masikitiko yake kuhusiana na vifo hivyo na kutoa pole kwa familia za marehemu waliokuwa wakilinda amani, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Vikosi vya Umoja wa Afrika kwa Umoja wa Mataifa vya Kulinda Amani (Unamid).

Ban K-Moon amelaani shambulio hilo dhidi ya Unamid na kuelezea matumaini yake kwamba Serikali ya Sudan itachukua hatua zinazofaa kuhakikisha kwamba wahusika wanafikishwa mbele ya sheria.

CHADEMA: TENDWA ALIBARIKI KUANZISHWA ‘RED BRIGADE’

Photo: Chadema: Tendwa alibariki kuanzishwa ‘Red Brigade’

Dar es Salaam. Chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema) kimesema Msajili wa Vyama vya Siasa, John Tendwa alibariki kuundwa kwa makundi ya vijana ndani ya chama hicho, yanayoitwa ‘Red Brigade’.

Hatua hiyo ya Chadema imekuja baada ya Tendwa kutishia kuifuta Chadema, iwapo wataendelea na mpango wao wa kuanzisha kambi za mafunzo ya kujilinda kwa vijana wake nchini.

Katika taarifa yake, aliyoitoa kwa vyombo vya habari jana, na kusainiwa na Naibu Msajili, Rajab Juma kwa niaba yake, Tendwa alieleza kushangazwa na kusikitishwa na hatua hiyo ya Chadema kwa kuwa walishakatazwa mpango huo tangu mwaka 2004.

“Msajili anavikumbusha vyama vyote vya siasa hasa Chadema kuwa, kifungu cha 19 cha Sheria ya vyama vya siasa kinampa uwezo wa kufuta usajili wa chama chochote kinachokiuka masharti ya usajili au kifungu chochote cha sheria ya vyama vya siasa. Kifungu cha 20 cha sheria ya vyama vya siasa kinasema uamuzi wa msajili ni wa mwisho na hauwezi kukatiwa rufaa mahakamani,” alisema Msajili.

Hata hivyo, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Chadema ambaye pia ni Mbunge wa Ubungo, John Mnyika alisema: “Tendwa alikuwepo kwenye mkutano wa Chadema wa Agosti 13, 2006 uliopitisha katiba mpya ya chama hicho.

“Katika katiba mpya tuliweka kifungu kinachosema, Chadema itakuwa na chombo cha kulinda

uongozi na mali za chama kikiitwa Red Brigade...Tendwa katika mkutano aliipongeza Chadema kwa mabadiliko hayo ya katiba.

“Katiba ya Chadema ilisajiliwa katika ofisi yake kwa mujibu wa sheria mwaka 2006 na kusema Chadema imekidhi matakwa yote,”

Kuhusu madai ya Chadema kwamba CCM kina kambi ya namna hiyo, Tendwa alisema hayana msingi, badala yake amekitaka kuwasilisha ushahidi katika taasisi husika ikiwamo ofisi yake unaoonyesha kambi za mafunzo za vijana wa CCM, ili suala hilo liweze kushughulikiwa kisheria.

“Kwa kuwa hivi sasa sheria zinakataza suala hili, hazijabadilika na viongozi wa Chadema ni walewale waliositisha kutekeleza mpango huo mwaka 2004, haieleweki nia yao sasa ni nini.

Kama ni kupima matokeo iwapo watatekeleza mpango huo, utakuwa si uamuzi wa busara kwa uhai wa chama chao,’’ alisisitiza msajili.

Alisema kuwa mwaka huo 2004 hata Chama cha Wananchi(CUF)kupitia kwa aliyekuwa Katibu Mkuu wa chama hicho, Wilfred Lwakatare kiliwahi kuomba ufafanuzi kwa msajili kuhusu nia yao ya kutaka kuanzisha mafunzo ya ukakamavu wa kujilinda kwa vijana wake kila wilaya, ambapo walikataliwa kwa kuwa ni kinyume cha sheria.

Msajili pia alitumia fursa hiyo kuviasa vyama vyote vya siasa kutumia muda wao kufanya shughuli za siasa,ili kuchangia maendeleo ya nchi, badala ya kutumia uwezo wao na muda kubuni mambo yanayoleta mtafaruku na kuhatarisha amani na utulivu nchini.

 

Dar es Salaam. Chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema) kimesema Msajili wa Vyama vya Siasa, John Tendwa alibariki kuundwa kwa makundi ya vijana ndani ya chama hicho, yanayoitwa ‘Red Brigade’.


Hatua hiyo ya Chadema imekuja baada ya Tendwa kutishia kuifuta Chadema, iwapo wataendelea na mpango wao wa kuanzisha kambi za mafunzo ya kujilinda kwa vijana wake nchini.

Katika taarifa yake, aliyoitoa kwa vyombo vya habari jana, na kusainiwa na Naibu Msajili, Rajab Juma kwa niaba yake, Tendwa alieleza kushangazwa na kusikitishwa na hatua hiyo ya Chadema kwa kuwa walishakatazwa mpango huo tangu mwaka 2004.

“Msajili anavikumbusha vyama vyote vya siasa hasa Chadema kuwa, kifungu cha 19 cha Sheria ya vyama vya siasa kinampa uwezo wa kufuta usajili wa chama chochote kinachokiuka masharti ya usajili au kifungu chochote cha sheria ya vyama vya siasa. Kifungu cha 20 cha sheria ya vyama vya siasa kinasema uamuzi wa msajili ni wa mwisho na hauwezi kukatiwa rufaa mahakamani,” alisema Msajili.

Wednesday, July 17, 2013

TAARIFA TOKA IKULU JUU YA RAI YA RAIS KIKWETE KWA RAIS BASHIR WA SUDAN


 Rais Jakaya Kikwete
--

 

Rais Jakaya Mrisho Kikwete amefanya mazungumzo kwa njia ya simu na Rais wa Sudan Mheshimiwa Omar Bashir kufuatia kuuawa na kujeruhiwa kwa askari wa Tanzania, walioko katika ulinzi wa kimataifa wa amani katika jimbo la Darfur na kumtaka Rais Bashir kuchukua hatua za haraka kuwasaka na kuwakamata waliohusika na kitendo hicho kiovu na kuwafikisha mbele ya sheria haraka iwezekanavyo.

Katika mazungumzo yao, Rais Omar Bashir amekubaliana na Rais Kikwete na kumuahidi kuwasaka  hadi kuwakamata wale wote waliohusika na kuwachukulia hatua za kisheria.


Rais Bashir amemueleza Rais Kikwete kuwa binafsi anaamini kuwa waliohusika ni wahalifu na hivyo kuahidi kuwa lazima 
watasakwa hadi kukamatwa kwa ajili ya kuchukuliwa hatua.

MAMA BAGHDAD AMUOMBEA MSAMAHA MWANAE KWA CHID BENZ... AOMBA WAKUTANE PAMOJA NA NAY WA MITEGO


Baada ya jana Chidi Benz kuweka wazi kuwa hategemei kumsamehe Baghdad kwa ‘blunder’ aliyoifanya ya kuwashirikisha yeye na Nay wa Mitego bila kuwaambia, mama mzazi wa Baghdad amekuja hadharani na kumuombea msamaha mwanae.

Mama huyo ameongea leo kwenye segment ya 255 kwenye kipindi cha XXL cha Clouds FM kuhusu nia yake ya kutaka kumaliza tofauti zilizopo kati ya mwanae na Chidi.

Mama Baghdad amekiri kuwa mwanae hakutumia akili kuchukua uamuzi huo wa kuwashirikisha wasanii wanaofahamika kuwa na uadui mkubwa kimuziki bila kufikiria madhara yake.

Amesema mwanae hakufanya jambo la busara na ndio maana ameamua kumpigia magoti Chidi ili ampe ‘second chance’ mwanae ambaye amejaribu kuomba msamaha bila mafanikio.

255 pia imezungumza na Chidi Benz aliyepo nchini Kenya kwa sasa ambaye amesema hawezi kukataa wito wa mama yake na Baghdad kwakuwa ni kama mama yake pia na amekubali kuja kukutana naye akirejea nchini.

Jana wakati akihojiwa kwenye kipindi cha Mambo Mseto cha Radio Citizen ya Kenya, Chidi alisema kamwe hatokuja kumsamehe Baghdad.

Source:Mambo Mseto {Radio Citizen},Kenya

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...