Friday, June 14, 2013
Thursday, June 13, 2013
KAULI YA BALOZI WA TANZANIA KUHUSU MSICHANA ANAYEDAIWA KUTAKA KUNYONGWA BAADA YA KUKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA EGYPT
Baada ya watu wengi kuzipata habari na bila kujua imekuaje kwa Mtanzania anaedaiwa kukamatwa na dawa za kulevya nchini Egypt na kwamba alikua anakaribia kunyongwa, balozi Mohamed Haji wa Tanzania nchini Egypt ameongea Exclusive na millardayo.com na kueleza yote anayoyafahamu kuhusu hii ishu. Namkariri akizungumza 1. Ni kweli kuna raia wawili Watanzania wamekamatwa na dawa za kulevya ambao ni Mbarak Abdallah Salim (28) na Sharifa Mahmud (27) wakazi wa Magomeni Kagera Dar es salaam, wanaundugu wa mtoto wa shangazi na mjomba. 2. Walikamatwa tarehe 16 May 2013 wakati wakiingia Misri, kwa mujibu wa maelezo safari yao ilianzia Dar es salaam kwenda Mombasa, Nairobi mpaka Misri. |
.
PICHA ZA KALA JEREMIAH AKIAMKABIDHI MAMA MZAZI WA MANGWAIR TUZO YAKE
MH: ZITO KESHO KUWA MGENI RASMI SHOW YA MWANA FA, HUKU SUGU AKIWA KWA JIDE
Ile the Big Square 1, show za magwiji wa
muziki Tanzania mwana FA ‘The Finest’ na Lady Jay Dee ‘Miaka 13 ya Lady
Jay Dee’ zitapigwa kesho June 14, huku presha ikiwa inaongezeka hasa kwa
fans wanaotamani kuhudhuria show walioichagua na kuona ukubwa wa show
kama walivyotarajia.
Show hizi kubwa zina nguvu sana kutokana
na ukubwa wa majina ya wasanii husika. Kwa mujibu wa lady Jay Dee timu
anaconda kesho itaungwa mkono na mheshimiwa Joseph Mbilinyi a.k.a Sugu.
Jide ambae hivi karibuni ameachia wimbo
mpya unaopatikana kwenye album yake ‘Nothing but the truth’ inayoitwa
Yahaya, amepost kupitia kupitia ukurasa wake wa facebook na pia katika
akaunti yake ya Twitter kuonesha list ya wasanii watakaopanda jukwaani,
na pia uwepo wa Sugu.
” Miaka 13 ya Lady JayDee, Ijumaa ya kesho shughuli inaanza rasmi saa 3:00 usiku...Ukiskia paaaa ujue show imeisha
1. Prof Jay 2. Juma Nature 3. Grace Matata 4. Hamza Kalala 5. Wakazi na ugeni wa Mh. Joseph Mbilinyi a.k.a SUGU
Nyimbo zote unazozipenda zitalia tar 14 June, pale Nyumbani Lounge sababu yaaaaa sababu yaaaaaa ?????????”
Kwa upande wa Mwana FA ambae atapiga show
yake na Live band akiwa na kundi kubwa na maarufu kwa upigaji wa Live
Band ‘Wananjenje’, yeye amepewa full sapoti na mbunge wa Kigoma
Kaskazini Zitto kabwe.
Zitto ameweka wazi kupitia akaunti yake ya twitter kuwa anamsapoti sana msanii huyo.
“You have my full support “@MwanaFA”
"BABY MADAHA ASITAKE KUPATA UMAARUFU KUPITIA JINA LANGU TENA ANIKOME" ...... JACK WOLPER
MWANADADA anayefanya vizuri katika tasnia ya filamu Jaqueline Massawe
‘Wolper Gambe’ amesema anamshangaa sana msanii wa muziki ambaye pia ni
mwigizaji Baby Madaha kutumia vyombo vya habari kutengeneza ugomvi
wakati hana mawasiliano naye yoyote na wala si rafiki yake au mtu
aliyekaribu naye na hana mazoea naye.
“Nimelizika na umaarufu nilio nao sihitaji
kujipeleka katika magazeti na kuongelea vitu ambavyo havina faida katika
jamii, mimi sina urafiki na Baby Madaha, namshanga anavyotapatapa
kuniandika vibaya kwa jambo lisilo nihusu, mambo hayo niliyafanya nikiwa
Chipukizi”
“Nakumbuka mimi nilipigiwa simu na rafiki yake
akiniomba namba mwenye nyumba lakini ghafla nikapiwa simu na mwandishi
wa habari mara Polisi nikashangaa huyo mtu hata namba ya mwenye nyumba
sijamtumia nasumbuliwa na watu utafikiri mimi ndio mtuhumiwa, lakini
jambo ninalomshangaa mimi ni dalali?,” alihoji Wolper.
Hivi karibuni yalizuka maneno yakiwahusisha wasanii hawa wawili
ikisemekana walikuwa wakigombea nyumba ya kupanga, huku Baby Madaha
kuigizwa mjini na mwenye nyumba kwa kupangishwa nyumba hewa, Wolper
amedai kuwa kwa sasa yeye amekuwa makini halipii nyumba kienyeji bali
ulipia kwa mwanasheria wake tena kwa kufuata taratibu kwa kukwepa
utapeli.
MUME WA MTU ANASWA GEST AKIWA NA SHOGA WAKIFANYA UCHAFU WAO
Tukio
hilo lililoshuhudiwa na watu kibao, lilijiri Juni 10, mwaka huu katika
nyumba moja ya kulala wageni iliyopo Kinondoni jijini Dar.
Kunaswa
kwa wanaume hao ambao ilidaiwa walikuwa kwenye harakati za kufanya
Usodoma na Ugomora, kulifuatia mke wa mmoja wao kunasa meseji za
kimapenzi walizokuwa wakitumiana wawili hao.
Mama
huyo alipobaini meseji hizo chafu, wawili hao wakisisitiziana kukutana
kwenye gesti hiyo usiku wa siku hiyo, alimpigia simu mmoja wa waandishi
na kumpa mkasa mzima ambapo walikubaliana saa moja zoezi la
kuwanasa litaanza..
Ilipofika saa 1:30 usiku, timu yetu, mama huyo, wapambe wake na polisi walikuwa wanafanya doria nje ya gesti hiyo.
Saa
5:30 usiku, mume wa mwanamke huyo akiwa na mwanaume anayedaiwa kuwa
shoga walifika gesti hiyo bila kujua kama waliwekewa mtego wa kunaswa na
kwenda kuchukua chumba namba 2.
Wakiwa
ndani, mke alimpigia simu mumewe na kuhoji alipokuwa akajibiwa alikuwa
mitaa ya nyumbani kwao Manseze, Dar akipiga stori na rafiki zake.
Wawili
hao wakiwa wanajiandaa na mchezo wao usiofaa, polisi aligonga mlango
akijifanya mhudumu aliyetaka kumpatia taulo, jamaa bila kujua alifungua
ndipo walipofumaniwa na kuibua varangati zito.
Kufuatia
timbwili hilo, waliwekwa chini ya ulinzi na kutolewa pale gesti tayari
kupelekwa kituoni ndipo mwanaume anayedaiwa kuwa shoga akatimua mbio
mithili ya mwanariadha wa kimataifa, Usain Bolt wa Jamaika na wanandoa
hao waliendelea kuzozana huku mke akimlalamikia mumewe na kumwambia
wakifika nyumbani ampe talaka yake.
Hata
hivyo, mwanamke huyo aliomba sakata hilo lisipelekwe polisi kwa madai
alichotaka ni kumfumania mumewe na kwamba alikuwa na ushahidi wote.
GPL
RAIS JACOB ZUMA ASEMA KUWA AFYA YA NELSON MANDELA YAANZA KUIMARIKA
Rais wa zamani wa Afrika Kusini Nelson Mandela kulia na rais wa sasa Jacob Zuma
Rais
wa Afrika Kusini Jacob Zuma amesema kuwa afya ya rais wa zamani wa
taifa hilo Nelson Mandela imeanza kuimarika kidogo kutokana na matibabu
anayopewa na Madaktari wake jijini Pretoria.
Zuma
amewaambia wabunge kuwa Mandela anayefahamika kwa jina maarufu kama
Madiba ameanza kuimarika na ni habari njema kwa raia wa nchi hiyo ambao
wamekuwa wakikumbwa na wasiwasi kutokana na afya yake kuendelea
kudorora.
Rais
huyo ameongeza kuwa kila mmoja anakumbuka mchango wa Mandela ambaye
alifungwa jela miaka 27 akiwa katika harakati za kupinga ubaguzi wa
rangi nchini humo na baadaye kufanikiwa kuwa kiongozi wa kwanza mweusi
nchini humo mwaka 1994.
Kiongozi
huyo wa Afrika Kusini amewataka raia wa nchi hiyo na dunia nzima
kuendelea kumwombea Mandela ili apate nafuu haraka na kuruhisiwa kurudi
nyumbani.
Familia
ya Mandela imesema kuwa imeguswa mno na salamu za heri njema
zinazotumwa na watu mbalimbali duniani kumtakia kiongozi huyo wa zamani
nafuu ya haraka.
Mandela
mwenye umri wa miaka 94 alilazwa hospitalini Jumamosi iliyopita baada
ya kuanza kusumbuliwa na mapafu tatizo ambalo limemsumbua kwa muda
mrefu.
MWANA FA AFUNGUKA KUHUSU BIFU LAKE NA LADY JAYDEE
Baada
ya kutibuana na Lady Jaydee, Mwana FA ameamua kuvunja ukimya
na kuwataka mashabiki wachukulie poa maana ni hali ya kawaida
tu katika maisha ya kibinadamu.....
Ugomvi
wa wasanii hawa ulianza baada ya Mwana FA ku re -tweet post
moja ya shabiki wake ambayo ilikuwa ikiiponda show ya Lady
Jaydee...
Lady
jaydee alijaribu kumuonya mara kadhaa lakini FA hakusikia na
badala yake aliretweet post ya shabiki mwingine ikimponda Lady
Jaydee....
Uvumilivu ulimshinda Lady Jaydee na kuamua kujibu mashambulizi kwa kumuita Mwana Fatuma na na mengine mengi.....
Wasikilize hapo chini wakifunguka
RAIS KAGAME AMGOMEA JK
RAIS
wa Rwanda, Paul Kagame, amemshambulia kwa maneno makali Rais Jakaya
Kikwete, akijibu ushauri alioutoa kwa serikali yake wa kukaa katika meza
ya mazungumzo na waasi wa kikundi cha Democratic Force for the Liberation of Rwanda (FDLR),
ili kumaliza mapigano. Shirika la Habari la Rwanda, linalojulikana kwa
jina la News of Rwanda, jana lilimkariri Rais Kagame akitoa maneno ya
kejeli na yenye mwelekeo wa kupuuza ushauri wa Rais Kikwete.
Kauli hiyo ya Rais Kagame, ambayo pia imesambazwa katika mitandao mbalimbali ya habari, inaonyesha kukerwa na ushauri wa Rais Kikwete ambao ameuita upumbavu uliojazwa ujinga.
Hii ni mara ya kwanza kwa Rais Kagame kutoa kauli hiyo tangu Rais Kikwete alipotoa ushauri huo, wakati akizungumza katika kikao cha Mkutano wa Umoja wa Afrika uliofanyika mapema mwaka huu, mjini Addis Ababa, Ethiopia.
Waasi wa FDLR ambao jamii yao ni Watutsi, walikimbilia nchini Kongo baada ya mapigano ya kimbari ya mwaka 1994, yaliyosababisha maelfu ya watu kupoteza maisha na wamekuwa wakiendesha chokochoko dhidi ya Serikali ya Rais Kagame.
Akizungumza katika sherehe ya kuhitimu mafunzo ya kijeshi maofisa 45 wa jeshi lake, Rais Kagame alisema ushauri wa kufanya mazungumzo na waasi wa FDLR ni ujinga na haupo katika historia ya Wanyarwanda.
Wednesday, June 12, 2013
KIFO CHA KASHI...YALIYOTABIRIWA NA MCHUNGAJI YAMETIMIA
Marehemu Jaji Hamisi ‘Kashi’.
KIFO
cha msanii wa siku nyingi katika tasnia ya filamu za Kibongo, Jaji
Hamisi ‘Kashi’ kilichotokea Jumatatu katika Hospitali ya Taifa ya
Muhimbili kimehitimisha maono ya mchungaji aliyetabiri kuwa mastaa
wawili mmoja wa Bongo Fleva na mwingine wa Bongo Movie watafariki dunia
ndani ya mwaka huu.
Marehemu Albert Mangwea.
TAARIFA ZA KIFO
Saa
5 asubuhi taarifa za kifo zilitua katika chumba chetu cha habari na
haraka waandishi wetu wakafika nyumbani kwa baba mzazi wa msanii huyo
Kinondoni Mkwajuni jijini Dar es Salaam na kuwashuhudia waombolezaji
wakiangua vilio kufuatia kifo cha mpendwa wao huyo.
Akizungumza
na paparazi wetu rafiki wa marehemu aliyejitambulisha kwa jina la
Mwamtoro Mzura alisema wiki mbili kabla ya kifo hicho, Kashi akiwa
anaendesha gari maeneo ya Karume, Ilala jijini Dar alikosea njia na
kwenda kujikita kwenye ukingo wa barabara na kuumia miguu.
“Baada
ya kupata ajali hiyo alikimbizwa Hospitali ya Amana na kupatiwa
matibabu, kisha akaruhusiwa kurudi nyumbani, kuanzia siku hiyo hali yake
ilianza kudhoofu,” alisema.
Mwamtoro
alisema kuwa Ijumaa iliyopita hali yake ilibadilika na kuwa mbaya,
hivyo akakimbizwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kupatiwa matibabu hadi
Jumatatu iliyopita alipoaga dunia.
MASTAA WAFURIKA NYUMBANI KWAKE
Jacqueline Pentzel ‘Jack wa Chuz’, Sabrina Rupia ‘Cathy’, Mayasa Mrisho ‘Maya’, Seif Mbembe, Herieth Chumila, Happy Nyatawa ambaye alikuwa na marehemu katika Kundi la Shirikisho la Msanii Afrika.
Mastaa hao walinaswa na mapaparazi wetu nyumbani kwa baba mzazi wa Kashi.
Jacqueline Pentzel ‘Jack wa Chuz’, Sabrina Rupia ‘Cathy’, Mayasa Mrisho ‘Maya’, Seif Mbembe, Herieth Chumila, Happy Nyatawa ambaye alikuwa na marehemu katika Kundi la Shirikisho la Msanii Afrika.
Mastaa hao walinaswa na mapaparazi wetu nyumbani kwa baba mzazi wa Kashi.
TANGAZO LA MAFUNZO YA UALIMU DARAJA 'A' NA STASHAHADA MWAKA 2013/2014
Nafasi za Mafunzo ya Ualimu Ngazi ya Cheti Daraja A na Stashahada kwa mwaka wa masomo 2013/2014.
Katibu
Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi anawatangazia Wahitimu wa
Kidato cha Nne mwaka 2012 na Kidato cha Sita mwaka 2013 kuwa muda wa
kupokea maombi kwa ajili ya mafunzo ya Ualimu ngazi ya Cheti na
Stashahada mwaka wa masomo 2013/2014 umeongezwa mpaka tarehe 28/06/2013.
Sifa za mwombaji ni kama zilivyoainishwa katika tangazo la Wizara lililopo katika tovuti ya Wizara www.moe.go.tz linalohusu “Nafasi za Mafunzo ya Ualimu Ngazi ya Cheti Daraja A na Stashahada kwa mwaka wa masomo 2013/2014”.Bofya hapa
Aidha, wahitimu wa kidato cha Sita kuanzia mwaka 2008 hadi mwaka 2013 wanahimizwa kutuma maombi yao.
Barua
za maombi zioneshe Jina na anuani kamili ya mwombaji na kuambatisha
nakala ya matokeo yake ya mtihani (wahitimu wa Kidato cha Nne 2012 na
Kidato cha Sita 2013 waambatishe ukurasa wenye matokeo yao kutoka Baraza
la Mitihani la Tanzania Au kuonesha namba yake ya mtihani)
Maombi yatumwe kwa:-
Katibu Mkuu,
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi,
S.L.P.9121,
DAR ES SALAAM
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
SUGU AFUNGUKA KUHUSU WAUZA UNGA WANAVYO WATUMIA WANAMUZIKI KUBEBA UNGA
USHUHUDA WA SUGU
Ukweli
wa jinsi matajiri wauza unga wanavyowatumia wanamuziki wa Kitanzania
kama punda, unapewa nguvu na ushuhuda aliowahi kuutoa Mbunge wa Mbeya
Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi ‘Sugu’. Mbunge huyo ambaye anapewa
heshima kwamba ni mmoja wa waasisi wa Bongo Fleva, alimweleza mwandishi
wetu kuwa kabla hajawa memba wa jumba hilo la kutunga sheria, aliwahi
kufuatwa na wauza unga kumshawishi awe anabeba mzigo kwenda nao nje ya
nchi.
“Jamaa waliniambia kwa sababu mimi nasafiri safiri sana, passport
(hati ya kusafiria) yangu itakuwa imeshagongwagongwa sana, kwa hiyo ni
rahisi kwenda nchi tofautitofauti kwa urahisi, kwa hiyo wakataka niwe
nabeba unga. “Kigezo cha pili waliona kwa sababu mimi ni mwanamuziki,
kwa
hiyo ni rahisi watu kuamini ziara zangu ni za kimuziki. Nilikataa,
niliwaambia siwezi kufanya biashara hiyo kabisa,” alisema Sugu.
Mwaka
2011, mbunge huyo aliwahi kugusia hilo, wakati akitoa hoja kuchangia
bajeti ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kuwa serikali
ni lazima iwasaidie wanamuziki wa Kitanzania kwa sababu wanaibiwa sana,
hivyo kuwafanya vijana kuona kimbilio rahisi la kutajirika ni kuuza
madawa ya kulevya. “Mheshimiwa spika, serikali isifanye ili kijana wa
Kitanzania afanikiwe lazima auze unga, madawa ya kulevya,” alisema Sugu
na kueleza mfano huo wa jinsi alivyofuatwa kushawishiwa na matajiri wa
unga ili naye awe punda.
WASTARA AKIRI KUTOKEWA NA MZIMU WA SAJUKI KITANDANI...!!
SIKU
chache baada ya staa wa sinema za Kibongo, Wastara Juma kumaliza eda
na kurejea Bongo akitokea Uarubuni ameanza kuona maruweruwe ndani ya
chumba alichokuwa akilala na mumewe marehemu, Sadick Juma Kiwoloko
‘Sajuki’, Risasi Mchanganyiko lina habari za uhakika.
Kwa mujibu wa Wastara siku hiyo akiwa amelala chumbani humo, usiku wa manane alihisi uwepo wa Sajuki kitandani kwake.
“Niliongea naye kwa kweli siwezi kukumbuka haswa ni nini tulichoongea lakini tulikuwa katika hali ya furaha sana,” alisema Wastara.
Pia, Wastara alisema kuwa wakiwa katika maongezi yao, aliuchukua mkono wake na kuuweka juu ya mwili wa Sajuki katika hali ya mapenzi na akapitiwa na usingizi.
“Asubuhi nilipoamka nilihisi kama nilikuwa na Sajuki pale kitandani, kuangalia vizuri, mkono wangu ulikuwa juu ya shuka badala ya mwili wa Sajuki,” aliongeza.
Hata hivyo, Wastara alisema kuwa alihisi ni ndoto lakini alipochunguza alihisi kama kulikuwa na mtu aliyekuwa amelala naye pale kitandani.
“Sijui kama ni maruweruwe, ndoto au Sajuki alikuja kweli kitandani kwangu, kikubwa ninachokiamini ni kwamba mapenzi kwa marehemu mume wangu ndiyo yamepelekea hali hiyo,” alisema
Wastara Juma akiwa na mumewe Sadick Juma Kiwoloko ‘Sajuki’ enzi za uhai wake.
“Niliongea naye kwa kweli siwezi kukumbuka haswa ni nini tulichoongea lakini tulikuwa katika hali ya furaha sana,” alisema Wastara.
Pia, Wastara alisema kuwa wakiwa katika maongezi yao, aliuchukua mkono wake na kuuweka juu ya mwili wa Sajuki katika hali ya mapenzi na akapitiwa na usingizi.
“Asubuhi nilipoamka nilihisi kama nilikuwa na Sajuki pale kitandani, kuangalia vizuri, mkono wangu ulikuwa juu ya shuka badala ya mwili wa Sajuki,” aliongeza.
Hata hivyo, Wastara alisema kuwa alihisi ni ndoto lakini alipochunguza alihisi kama kulikuwa na mtu aliyekuwa amelala naye pale kitandani.
“Sijui kama ni maruweruwe, ndoto au Sajuki alikuja kweli kitandani kwangu, kikubwa ninachokiamini ni kwamba mapenzi kwa marehemu mume wangu ndiyo yamepelekea hali hiyo,” alisema
FAMILIA YAMKATAA MTOTO WA NGWEA....!!!
SIKU chache baada ya aliyekuwa mkali wa Hip Hop Bongo, Albert Kenneth Mangweha ‘Ngwea’ kupumzishwa kaburini kufuatia kifo cha usingizini nchini Afrika Kusini kilichotokea Mei 28, mwaka huu, mambo kibao yanazidi kuibuka.
Habari
zinadai kuwa familia ya marehemu Ngwea imemkataa mtoto aliyeletwa na
mama yake makaburini akidaiwa kuwa ni mtoto wa Ngwea.
MTOTO WA NGWEA
Juni 6, mwaka huu wakati wa mazishi, mwanamke aliyejitambulisha kwa jina la Paulina Jeremiah, mkazi wa Kigamboni, Dodoma alitimba akiwa na mtoto huyo wa kike aitwaye Neema Albert na kudai kuwa alimzaa na Ngwea mwaka 2001, wakati msanii huyo akisoma Sekondari ya Mazengo.
MTOTO WA NGWEA
Juni 6, mwaka huu wakati wa mazishi, mwanamke aliyejitambulisha kwa jina la Paulina Jeremiah, mkazi wa Kigamboni, Dodoma alitimba akiwa na mtoto huyo wa kike aitwaye Neema Albert na kudai kuwa alimzaa na Ngwea mwaka 2001, wakati msanii huyo akisoma Sekondari ya Mazengo.
Wakati akijieleza, ndugu wa Ngwea, Anthony Mangweha alikuwa akimsikiliza ambapo aliwataja wanandugu wa marehemu waliokuwa wakijua suala hilo.
Waliotajwa kujua kuwa mtoto huyo alikuwa wa Ngwea ni Frank, Jotam na Amani ambao waliwahi kutumwa na marehemu kwenda kumwangalia mkoani Dodoma.
Hata hivyo, ndugu huyo aliyekuwa akimsikiliza alimtaka mama Neema kupoa, hadi familia ikae kikao.
.
FAMILIA YAKAA KWA SAA 7, YATOA UAMUZI MZITO!
“Kweli wikiendi iliyopita familia ilikaa kikao kwa zaidi ya saa 7, pamoja na mambo mengine lakini wanadaiwa kufikia uamuzi mzito wa kumkataa mtoto huyo hadi mama Neema apeleke vigezo vya uthibitisho,” kilisema chanzo chetu ndani ya kikao hicho.
Akizungumzia suala hilo kwa sharti la kutotajwa gazetini, mmoja wa dada zake Ngwea alisema: “Ni kweli yule mtoto aliondoka na mama yake lakini kama akileta uthibitisho tutampokea.”
“Kweli wikiendi iliyopita familia ilikaa kikao kwa zaidi ya saa 7, pamoja na mambo mengine lakini wanadaiwa kufikia uamuzi mzito wa kumkataa mtoto huyo hadi mama Neema apeleke vigezo vya uthibitisho,” kilisema chanzo chetu ndani ya kikao hicho.
Akizungumzia suala hilo kwa sharti la kutotajwa gazetini, mmoja wa dada zake Ngwea alisema: “Ni kweli yule mtoto aliondoka na mama yake lakini kama akileta uthibitisho tutampokea.”
Subscribe to:
Posts (Atom)