Habari Habari za uhakika zilieleza kuwa Wema na timu ya wafanyakazi
katika kampuni yake ya Endless Fame Production, alikodisha ndege ya
kifahari kutoka Dar kwenda Arusha kwa ajili ya mapumziko tangu Aprili 18
hadi 20, mwaka huu.
Ilifahamika kuwa
ndani ya ndege hiyo ambayo kuikodisha ni mkwanja mrefu, aliongozana na
kampani yake tu.
CHANZO
CHA YOTE NI DIAMOND
Ilibumburuka kuwa
timu yake hiyo ilikuwa takriban watu watano ambao walimsindikiza kwenda
kwenye mapumziko kutokana na ‘stresi’ alizokuwa nazo.
Ilielezwa kuwa stresi alizokuwa nazo
zilitokana na ile ishu ya kudaiwa kurekodiwa akibembeleza penzi kwa
aliyekuwa mwandani wake, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ usiku mkali
huku jamaa akiwa amelala na mpenziwe wa sasa, Penniel Mungilwa ‘Penny’.
Baada ya kutokea
kwa ishu hiyo ndipo Wema alipoamua kwenda kujichimbia Arusha kupoteza
mawazo.
“Unajua ile ishu ilimchanganya sana bidada maana
hakutegemea kama Diamond anaweza kufanya kitu kama kile so (kwa hiyo)
alikwenda kutuliza akili na kweli sasa hivi walau yupo fresh (vizuri),”
alisema sosi wa karibu wa Wema.
AINGIA ARUSHA KWA ULINZI MKALI
Walipoingia jijini Arusha, staa huyo wa Filamu ya The
Super Star alipokelewa kwa ulinzi mkali hadi katika hoteli ya bei mbaya
aliyokuwa ameweka oda kwa ajili yake na watu wake.
“Unaambiwa kuanzia Arusha Airport (uwanja wa ndege)
hadi hotelini ilikuwa ni full ulinzi wa kufa mtu,” kilisema chanzo
chetu,




















Kwa mujibu wa mtandao wake wa kijamii wa Instagram, Lulu
alitupia picha akiwa ‘location’ kuashiria kwamba amerudi kazini baada
ya kusimama kuigiza kwa muda mrefu.




