Kumekuwa na uvumi kuhusu wasanii wanaoliunda
kundi la muziki la PSquare kutengana kiasi cha mashabiki wao kubaki
wameduwaa. Hata hivyo Peter na Paul Okoye wameweka wazi kuwa huwa wanaingia kwenye mitafaruku hadi kufikia hatua ya kupigana makonde huku kila mmoja akitishia kutengana lakini wakadai kwamba kama ni kutengana ambae angeweza kuwatenganisha ni mama yao pekee. Wawili hao wamesema kuwa mama yao aliwalea na kuwaonyesha upendo na mapenzi na kama ingetokea kuwa siku moja itatokea PSquare watatengana basi yatakuwa ni maamuzi ya wazi na kama mmoja wao ataamua kustaafu muziki basi haimaanishi kuwa wataacha kusaidiana. |
Tuesday, March 26, 2013
HABARI KUHUSU KUVUNJIKA KWA KUNDI LA P. SQUARE...!!!
Tanzania yaahidiwa misaada bila masharti
Rais Xi Jinping wa China ameahidi
kuendelea kuipiga jeki Afrika ili kukabiliana na changamoto za
kimaendeleo, huku akisema kuwa suala la utoaji misaada yenye masharti
magumu siyo ajenda ya Serikali yake. Jinping akitumia jukwaa la Tanzania
kutambulisha sera yake kwa nchi za Afrika alisema kwamba bara hilo
limepiga hatua kubwa kimaendeleo na kwamba nchi yake itaimarisha
uhusiano uliopo kwa manufaa ya pande zote mbili.
Alisisitiza kwamba ushirikiano wenye tija ni ule
unaozingatia “majadiliano na maridhiano” na kwamba Serikali yake
imetenga kiasi cha Dola za Marekani 20 bilioni kufadhilia miradi
mbalimbali ya maendeleo Afrika.
“China haitakuwa tayari kutoa masharti kwa
taifa lolote… Tunataka kutoa fursa zinazofanana,” alisema Rais, ambaye
alishika rasmi wadhifa huo Machi 14, mwaka huu. Alisema China
haitaingilia masuala ya ndani ya nchi, huku akisisitiza kwamba shabaha
ya nchi yake ni kuendelea kupalilia ushirikiano mwema uliodumu kwa
miongo kadhaa na siyo kujihusisha na migogoro.
Baadhi
ya wachunguzi wa mambo wanadai kuwa, kauli ya kiongozi hiyo ni kama
ujumbe wa onyo kwa baadhi ya nchi za Magharibi ambazo zinalalamikiwa
kuendesha sera zinazominya ustawi wa Afrika.
Mhadhiri katika
Chuo cha Diplomasia na Uhusiano wa Kimataifa (CFR), Dk Ahmed Mtengwa
alisema: “Ni hotuba inayofungua njia kwa Afrika..., amezungumzia
ushirikiano unaolingana yaani `win win situation’ (kila upande
ufaidike), hivyo kwangu ninayaona matumaini.”Rais Jinping,
aliyekuwa katika ziara ya siku mbili nchini na juzi usiku alisaini
mikataba 17 inayohusu sekta za kilimo, afya na miundombinu.
Mkataba
wa ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo mkoani Pwani ni kati ya miradi mikubwa
iliyomo kwenye makubaliano hayo na ujenzi wake utafanywa na Kampuni ya
Merchants Holding ya China na utakwenda sanjari na ujenzi wa barabara
inayounganisha bandari hiyo.
Pia katika
bandari hiyo itaunganishwa na Reli ya Kati na na ile ya Mamlaka ya Reli
ya Tanzania na Zambia (Tazara) ili kurahisisha usafiri wa mizigo ndani
na nje ya nchi. Mikataba mingine itahusiana na uboreshaji wa sekta ya
viwanda, kilimo hasa kile cha tumbaku ikiwamo kuwatafutia soko wakulima
kutoka Mikoa ya Tabora na Ruvuma ili waweze kuuza zao hilo katika soko
la China pamoja na kulipatia Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) zana
za kufanyia kazi.
Rais huyo, ambaye Tanzania ndiyo nchi
ya kwanza barani Afrika kuitembelea, alizindua na kukabidhi rasmi Kituo
cha Mikutano cha Kimataifa cha Mwalimu Julius Nyerere kilichoko jijini
Dar es Salaam ambalo ni jengo la ghorofa tatu na lenye kumbi nne za
mikutano zenye uwezo wa kuchukua watu 1,800 kwa wakati mmoja.
Ujenzi wa kituo
hicho uligharimu Dola za Marekani 29.7 milioni zilizotolewa na Serikali
ya China kwa lengo la kumuenzi Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.
Rais huyo
alisifu ushirikiano wa muda mrefu baina ya taifa lake na Tanzania na
kusisitiza kuwa nchi hizo zitaendelea kusaidiana kama sehemu ya kuenzi
misingi iliyowekwa na waasisi wa mataifa haya mawili, Mwalimu Julius
Nyerere na Mao Tse Tung.
Rais
Jinping aliondoka jana jioni kwenda Afrika Kusini kuhudhuria mkutano wa
tano wa Wakuu wa Nchi zinazokua kwa kasi kiuchumi ikiwamo Brazil, Urusi,
India, China na Afrika ya Kusini (BRICS).
Chanzo -
Mwananchi
NGUMI ZITAPIGWA BUNGENI: NDESAMBURO
MBUNGE wa
Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo, (CHADEMA), amewataka Watanzania
watarajie mapanbano makubwa zaidi bungeni, hata ikibidi ngumi kupigwa,
ili kuleta ustaarabu na kutetea haki ya kidemokrasia katika chombo hicho
cha kutunga sheria.
Ndesamburo
ambaye amekuwa bungeni tangu mwaka 2000, alisema hayo jana katika
mahojiano mafupi na gazeti hili, ofisini kwake Moshi Mjini.
Alisema
nyakati zimebadilika na wabunge wa mwaka 2013 si sawa na wa mwaka 2000;
kwani hawa wa sasa hawako tayari kuona kanuni zinavunjwa waziwazi.
Ndesamburo
alikuwa akizungumzia kauli ya Spika wa Bunge, Anna Makinda, na Naibu
wake, Job Ndugai, ambao wanadai kuwa baadhi ya wabunge wa CHADEMA ni
vinara wa fujo bungeni.
Alisema
siasa za sasa ni za vijana, si za wazee kama ilivyokuwa huko nyuma na
kwamba wazee wanapaswa kuelewa kuwa nyakati zimebadilika.
Alisema
kwamba katika siasa za kuelekea mwaka 2015, CHADEMA ina nafasi kubwa ya
kushinda ili kuwaletea Watanzania maendeleo waliyokosa kwa miaka zaidi
ya 50.
“Kwa hiyo
watu wajifunze kwenda na wakati. Zamani Bunge lilikuwa limetawaliwa na
wazee. Sasa kuna vijana. Vijana ni tofauti na wazee. Lazima wazee waanze
kujua vijana wanataka nini. Sheria na kanuni zinazoendesha Bunge,
vijana wanazijua, zinapovunjwa ni rahisi kuelewa. Zamani hakuna
aliyekuwa anajali hilo.
“Hizi fujo
ni demokrasia. Bunge linashika hamasa, limekuwa zuri. Wala wasione haya.
Hii ni mwanzo tu, tutaona mengi hata ngumi zitapigwa mle ndani. Ndiyo
ustaarabu, hilo ndilo Bunge. Unaponyimwa haki yako, unataka mtu
afanyeje?”
Katika
Bunge la Februari, Bunge lilitawaliwa na fujo, baada ya Spika wa Bunge,
Anna Makinda, na Naibu Spika, Job Ndugai, kuliendesha Bunge kinyume cha
kanuni na kusababisha kuzomewa na wabunge wa upinzani waliodai Spika na
naibu wake wanapinda kanuni.
Mjadala
mkali ulianza wakati wa kujadili hoja binafsi za mbunge wa Ubungo, John
Mnyika, mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari, na Mbunge wa
Kuteuliwa na Rais, James Mbatia. Uongozi wa Bunge uliahirisha shughuli
za Bunge mara kadhaa baada ya hali ya kutoelewana na ubishi mkali
kutokea ndani ya Bunge.
Akizungumzia
hali hiyo, Makinda alinukuliwa akisema, “Hata hivyo, imelazimu
kuahirisha mijadala ya hoja binafsi kutokana na tabia iliyojitokeza ya
utovu wa nidhamu kwa baadhi ya wabunge na hivyo kuamua kwa makusudi
kuanzisha vurugu na hivyo kulifanya Bunge lianze kupoteza heshima yake
ya kibunge.”
Alisema
hoja binafsi za wabunge zinaongozwa na kanuni za Bunge kuanzia kanuni ya
53 hadi 58, na kanuni za majadiliano zinaongozwa na kanuni kuanzia 59
hadi 71 ambazo kwa ujumla wake zikifuatwa kama inavyotakiwa vurugu
haiwezi kutokea bungeni.
Makinda
ambaye alionekana kuzungumza kwa jazba, alisema katika mkutano huu
imeonyesha waziwazi baadhi ya wabunge kwa makusudi na kwa nia ya
kupotosha wananchi wanatumia vibaya kanuni hizo na wakati mwingine
kuwadanganya wananchi ambao kwa bahati mbaya kanuni hizi hawazifahamu.
Ubabe huo
wa Spika na naibu wake ulisababisha kwa mara ya kwanza tangu kumalizika
kwa uchaguzi mkuu wa 2010, wabunge wa vyama vya upinzani kuungana
kumsusa Spika na Naibu Spika, wakipinga hatua yake ya kupindisha hoja
mbalimbali zilizowasilishwa na wabunge wa upinzani.
Wabunge wa
vyama vya upinzani waliotoka kupinga ubabe wa Spika kinyume cha kanuni
ni wa vyama vya CHADEMA, CUF, UDP, TLP na NCCR-Mageuzi ambao waliungana
kwa kutoka nje ya ukumbi wa Bunge, kupinga hatua ya Ndugai kuwaburuza
katika kupitisha hoja ya Mbatia.
Hoja hiyo
binafsi iliyoainisha udhaifu katika mfumo wa elimu nchini, iliwasilishwa
na kuibua mjadala mzito bungeni, huku kambi ya upinzani ikikubali hoja
ya Mbatia kutaka kuunda kamati teule wakati wabunge wa CCM wakipinga,
hoja iliyosababisha hadi sasa Wazairi Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania kuunda tume inayotafuja tatizo la kufeli kwa wanafunzi wa mwaka
2012.
SOURCE
TANZANIA DAIMA
Mahakama yaamuru matokeo ya urais Kenya yachunguzwe
Nairobi.
Mahakama ya Juu (Supreme Court) ya nchini Kenya imeagiza kuchunguzwa kwa
fomu 34 za matokeo ya uchaguzi wa rais kutoka katika vituo vyote
34,400, vilivyotumika kupigia kura katika Uchaguzi Mkuu wa nchi hiyo
uliofanyika Machi 4, mwaka huu.
Kadhalika mahakama hiyo jana iliagiza
kuhesabiwa upya kwa kura za urais katika vituo vya kupigia kura 22 kati
ya elfu 33 vilivyolalamikiwa na aliyekuwa mgombea urais wa Muungano wa
Cord, Raila Odinga.
Katika malalamiko yake yaliyowasilishwa
katika mahakama hiyo kupinga Uhuru Kenyatta kutangazwa mshindi wa urais
katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Machi 4, Odinga alidai kuwa vituo hivyo
22 kura zilizopigwa zinazidi idadi ya wapigakura walioandikishwa.
Akisoma uamuzi huo kwa niaba ya majaji
wenzake watano, Jaji Smokin Wanjala alisema kwamba uhesabuji kura wa
vituo hivyo utafanyika leo kuanzia saa 2.00 asubuhi kwa lengo la kubaini
ukweli kuhusu madai hayo.
“Matokeo ya kura zitakazohesabiwa katika
vituo hivyo 22 yawasilishwe katika mahakama hii Jumatano, saa 10.00
jioni,” alisema Jaji Wanjala.
Kikao hicho, ambacho Jaji Mkuu wa
Tanzania, Mohamed Othman Chande amealikwa kama mwangalizi, ni cha awali
kabla ya kesi hiyo kuanza kusikilizwa rasmi keshokutwa (Alhamisi) na
kuendelea kwa mfululizo hadi kufikia uamuzi ikiwa madhumuni yake.
Lengo ni kupitia madai yaliyowasilishwa
mahakamani hapo na pande zote zinazohusika na kuamua mwenendo wa kesi
utakavyofanyika.
Ukiachilia mbali kesi iliyofunguliwa na
Odinga kupinga Kenyatta kutangazwa mshindi wa uchaguzi huo wa tano tangu
kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi hapa Kenya, kuna kesi nyingine
ambayo imefunguliwa na muungano wa mashirika yasio ya kiserikali, `The
African Centre for Open Governance’ (Africog).
Katika kesi hiyo inayorushwa moja kwa
moja na vituo kadhaa vya televisheni nchini Kenya, Africog inahoji
uhalali wa uchaguzi huo.
“Kesi yetu haihusiani na nani ameshinda
au kushindwa bali jinsi umma ulivyoshindwa, tumepoteza ahadi ya uchaguzi
uliowazi,” alisema Gladwell Otieno, Mkurugenzi Mtendaji wa Africog.
Kesi ya tatu ambayo imefunguliwa na
wajumbe wa timu ya kampeni ya Kenyatta, mwanaharakati katika mitandao ya
kijamii Dennis Itumbi na Moses Kuria wanaopinga uamuzi wa Tume Huru ya
uchaguzi na Mipaka (IEBC) ya kujumuisha kura zilizoharibika wakati wa
kujumlisha kura za wagombea urais.
Katika uamuzi wake, mahakama iliamua
kwamba kesi zote tatu zitaunganishwa kuwa moja, huku ile iliyowasilishwa
na Odinga ikiwa ndiyo kinara wa kesi zote.
Pia mahakama iliamuru Muungano wa Vyama
vya Siasa wa Cord na Jubilee kuteua mawakala 10 kila mmoja ambao
watakula kiapo mahakamani hapo kabla ya kuanza kuhesabu upya kura hizo.
Katika uamuzi wake jana jioni, mahakama
hiyo ilikubali ombi la Mwanasheria Mkuu wa Kenya, kushiriki katika kesi
hiyo kama rafiki wa mahakama na siyo mdaiwa kama ilivyokuwa awali.
Wakili wa Cord, George Oraro alikubali uamuzi huo licha ya kuupinga
awali.
Chadema Arusha yatangaza mgogoro tena na RC, OCD
Arusha. Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema) Kanda ya Kaskazini, kimetangaza mgogoro na Mkuu wa Mkoa wa
Arusha, Magessa Mulongo na Kamanda wa Polisi Wilaya ya Arusha (OCD),
Gilles Bilabaye .
Hatua hiyo inatokana na kile kinachodai
walitumia lugha na kauli za matusi dhidi ya wanachama na wafuasi wa
chama hicho, kwenye harakati za kuzuia maandamano yaliyoitishwa
kumshinikiza Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa
ajiuzulu.
Akisoma tamko la chama hicho kwa
waandishi wa habari jana, Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema alisema
viongozi hao waliwaita vijana wafuasi wa Chadema kuwa ni wahuni, wavuta
bangi na wanywa viroba.
Pia, wanadaiwa kuwaita wafuasi hao kuwa
hawana kazi za maana, ndiyo maana wanakubali kushiriki maandamano
yanayoitishwa na chama hicho.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, viongozi hao
wanadaiwa kutoa kauli hizo Jumamosi na Jumapili iliyopita wakiwa katika
harakati za kukabiliana na tishio la maandamano yaliyotangazwa na
Chadema, kabla ya kuahirishwa baada ya makubaliano kati ya Mwenyekiti wa
chama hicho, Freeman Mbowe na Mkuu wa Polisi nchini, Said Mwema.
Wakati Magessa akisema alitimiza wajibu
na majukumu yake ya kazi kuhakikisha maandamano hayo hayafanyiki, OCD
aligoma kuzungumzia tuhuma dhidi yake akisema mwenye mamlaka ya suala
lolote linalohusu polisi ni Kamanda wa Polisi Mkoa (RPC).
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha,
Lebaratus Sabas alisema hawezi kuzungumzia tuhuma dhidi ya OCD wake, kwa
sababu hakusikiza maneno hayo yakitamkwa.
Januari 5, 2011 Chadema waliandaa
maandamano kupinga uchaguzi uliomweka madarakani Meya wa Arusha,
Gaudence Lyimo matokeo yake watu watatu waliuawa na polisi.
MBUNGE SHAROBARO WA KENYA SONKO AWAPA TIMU YA KENYA SHILINGI MILIONI MOJA BAADA YA KUTOKA SARE NA NIGERIA
Nairobi County
Senator Miko Mbuvi alias Sonko has promised to award the Kenya National
football side one million cash prize after they held Nigerian to a
famous 1-1 draw at Calabar on Saturday evening,
Sonko will also top up a 100, 000 Shillings for Francis
Kahata’s sublime free kick that nearly won the game for Kenya.
The National Alliance (TNA) chairman Johnson Sakaja and
Sonko’s close ally tweeted via his handle@SakajaJohnson Tweeted : Sonko
says he'll still give the 1m. #HarambeeStars are winners!!
Prime Minister Raila Odinga has also promised to host the
team for dinner and award team members and the technical bench.
FKF chairman Sam Nyamweya will also part with a cool one
million as a token of appreciation for job well done.
Kenya has two points from three games in a group that also
includes of Namibia and Malawi.
Monday, March 25, 2013
Wema atoa sababu za kutoa milioni 13 za faini ya Kajala
Mrembo Wema Sepetu leo amemake headline baada ya kutoa mfukoni mwake shilingi milioni 13 kulipa faini aliyopigwa muigizaji mwenzie Kajala Masanja aliyehukumiwa leo kwenda jela miaka mitano ama kulipa kiasi hicho cha fedha.
Kajala
na Wema wakikumbatiana
Akizungumza exclusively na Bongo5, Wema amesema hakufikiria mara
mbili kutoa kiasi hicho cha fedha.“Kusema kweli wanasemaga kwamba kutoa ni moyo so naamini what I did is best, nimetoa kwasababu I had to do it and sikuthink twice kuhusu kufanya hivyo,” amesema Wema.
Wema akwa na
Kajala
“Nimefanya kama namsaidia rafiki yangu kama namsaidia ndugu yangu na
sidhani kama ingekuwa ni kitu kizuri kumuona mwenzako anaingia kwenye
dhahama, kwenye tabu, kwenye mateso na wakati nina uwezo wa kumsaidia
kwahiyo I just did what I had to do.”Kuachiwa kwa Kajala kumepokelewa kwa furaha kubwa na mastaa mbalimbali nchini.
Cpwaa
So I hear Kajala is out! Good news..Hongereni sana wana BOngoMovies! Bongoflava tujipangeni..tutaendelea kupigwa bao kila siku while we are sitting on a Multi-Billion Industry, it’s time to stop fantasizing posing in front of camera poppin bottles of Champagne,Rented Fancy cars,Cheap Wardrobe n ( No..The Ladies are fine,I love them too sitaki ubaguzi)… Tufikirie kibiashara zaidi na sio sifa tu.
Rio Pol
It’s a blessed Monday I say this because finally someone stood up and did something right and righteous. I’ve worked in the entertainment industry for the past seven years and no star or their glam team or entourage would do what Miss Wema Abraham Sepetu did. Thank you god both my girls Elizabeth Michael and Kajala Masanja are free. God bless you wema.
Kajala
akikumbatiana na Zamaradi
Mboni MasimbaKAJALA outtttttttttt# Mungu mkubwa # WEMA mwokozi wa KAJALA # Mwenyez Mungu akuzdishie na akupe ulipo pungukiwa. Una moyo wa pekee. Lov u always my Dogo
Ben Pol
Nimemvulia kofia Wema, ameni-inspire …moyo kama huo anao mtu mmoja Kati ya Milioni moja, watu hujifanya wakisikitika humu twitter tu…
Elizabeth Michael aka Lulu
Welcome back kay wangu…….Kajala wangu….mamy wangu
Na Bongo5
KAJALA AKILIA KWA FURAHA MARA BAADA YA WEMA SEPETU KULIPA FAINI YA MILIONI 13 MAHAKAMANI LEO
Msanii wa bongo movie Kajala (kushoto) akilia
kwa furaha mara baada ya mahakama ya hakimu mkazi kisutu kutoa hukumu ya
kesi yake kwa kwenda jela miaka 5 au kulipa faini ya Shilingi za
Kitanzania Milioni 13 ambazo zililipwa na Msanii mwenzake Katika tasnia
hiyo Wema Abraham Sepetu ili kumnusuru Kajala kwenda jela Miaka Mitano.
Pembeni yake aliyemshika ndie Msanii Wema Abraham Sepetu aliyemlipia
Faini ya Shilingi Milioni 13 za Kitanzania
Rais Kikwete apokea ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa julius Nyerere toka kwa Rais wa China Xi Jinping
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete
akipokea ufunguo kutoka kwa Rais Wa Jamhuri ya Watu wa China Mhe.Xi
Jinping wakati wa makabidhiano ya Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa
Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo.Ukumbi huo umejengwa
kwa ushirikiano kati ya Seriklai ya China na Tanzania.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na
Rais Xi Jinping wa China wakishangilia
jambo wakati wa makabidhiano ya Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa
Julius Nyerere leo jijini Dar es Salaam.
jambo wakati wa makabidhiano ya Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa
Julius Nyerere leo jijini Dar es Salaam.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete
akihutubia wageni waliohudhuria sherehe za makabidhiano ya Ukumbi wa
Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere leo jijini Dar es Salaam.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete
na Rais wa China Mhe.Xi Jinping wakiangalia picha za matukio
mbalimbali yanayohusu historia ya ushirikiano kati ya China na Tanzania
katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere leo wakati wa
sherehe za makabidhiano ya ukumbi huo jijini Dar es Salaam leo. Picha
na Freddy Maro - Ikulu. LOVENESS LOVE ''DIVA'' AJUTA KUGAWA PENZI KWA MO RACKA
Diva alhamisi iliyopita alifunguka kuhusu kosa kubwa alilolifanya katika maisha yake tangu azaliwe. Na alichosema kajuta ni kua na uhusiano wa kimapenzi na msanii Mo Racka. Hiki ndicho alichokiandika Twitter jana usiku |
WEMA SEPETU AWAFANYIA SHOPPING YA ZAIDI YA TSH. MIL. 6.5 MBWA WAKE WAWILI
Staa wa bongo movie na mmilikiwa kampuni ya Endless love film
anayejulikana kama Wema Isaac Sepetu hivi karibuni amefanya kufuru kwa
mbwa wake wawili baada ya ‘shopping’ iliyogharimu dola 4,000 za
Kimarekani (zaidi ya TSh. milioni 6.5)
Wema aliteketeza kiasi hicho cha fedha kwa
kuwanunulia mbwa hao pafyumu, viatu na nguo, alivyoagiza kutoka nchini
China, lengo likiwa ni kuhakikisha wanaishi katika mazingira mazuri.
Baada yay eye kuulizwa alikuwa na haya ya kusema
“Najua watu wanaweza kushangazwa na kitendo cha
mimi kutumia kiasi hicho cha fedha lakini sioni kama ni tatizo kwani ni
kitu ambacho kinanipa furaha katika maisha yangu.”
Mbwa hao wa Wema Sepetu aliowapa majina ya Van na
Gucc wamekuwa ni gumzo kutokana na jinsi anavyowahudumia huku akiajiri
watu maalumu wa kuhakikisha wanavaa, kula na kulala pazuri.
KAJALA AHUKUMIWA MIAKA 5, MUMEWE MIAKA 7
HUKUMU ya kesi iliyokuwa
inamkabili staa wa filamu za Kibongo, Kajala Masanja na mumewe
imetolewa leo na Hakimu Sundi Fimbo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi
Kisutu, jijini Dar. Katika hukumu hiyo Kajala amehukumiwa kwenda jela
miaka mitano au kulipa faini ya shilingi milioni 13 na mumewe kwenda
jela miaka saba au kulipa faini ya shilingi milioni 200.
Kajala alikuwa anakabiliwa na kesi ya kuuza nyumba iliyowekwa kizuizini na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) baada ya mumewe, Faraji Agustino kukumbwa na msala wa kutakatisha fedha haramu.
Wasanii wa Bongo movie wanazichanga hapahapa kuzilipa ila zimepngua kidogo,Wema na Zamaradi wanakimbia ATM KUZICHUKUA ZINGINE.leo leo Kajala anafika nyumbani kwao
ISHA MASHAUZI NAYE BINGWA WA MADAWA YA KULEVYA AKILI MWENYEWE.......!!!
STAA wa muziki wa taarab na mkurugenzi wa Mashauzi Classic, Aisha Ramadhan ‘Isha Mashauzi’ ameibua gumzo na kushangaza mashabiki baada ya kukiri kuwa yeye ni mtumiaji wa pombe kali na madawa ya kulevya aina ya mirungi
Ishu hiyo ilijiri Alhamisi ya wiki iliyopita wakati akihojiwa na mtangazaji wa Redio Times FM, Hadija Shaibu ‘Dida’ kupitia kipindi chake cha Mitikisiko ya Pwani ambapo alisema mirungi na pombe kali ndiyo starehe yake kwani inampa stimu kabla hajapanda jukwaani na katika maisha yake ya kawaida nje ya usanii.
Mashauzi alifunguka hayo baada ya Dida kumtaka atoe ufafanuzi juu ya skendo ya kuvuta bangi inayomkabili ambapo alisema siyo kweli kwamba anavuta bangi ila akakiri kuwa anakula sana mirungi na kugida ulabu. Aliongeza kwamba kwa kuwa hana mume, mtoto wala hataki kuwa na familia, mirungi na pombe ndiyo vitu vinavyompa furaha maishani mwake.
UKWELI KUHUSU ELIMU YA NAIBU WAZIRI WA MH. MLUGO HUU HAPA
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo anadaiwa kutumia ujanja katika wasifu na elimu yake ambapo katika maisha yake ya kielimu ametumia majina manne tofauti.
Philipo Augustine Mulugo ndiyo jina lake halisi ambalo alilisomea mpaka alipohitimu darasa la saba kwa mara ya kwanza 1988, lakini kutokana na kwamba hakufaulu kwenda sekondari alirudia darasa hilo.
Uchunguzi uliofanywa na Mwananchi kwa takriban miezi mitatu sasa umebaini kuwa 1989, Mulugo alirudia darasa la saba katika Shule ya Msingi Rukwa ya mkoani Mbeya akitumia jina la Hamimu Hassan.
Imebainika kuwa kabla ya kuhitimu darasa la saba kwa mara ya pili, alibadili jina hilo (kutoka Hamimu Hassan) na kuwa Hamimu Augustino ambalo aliendelea nalo wakati akisoma elimu ya sekondari katika Shule ya Sekondari kutwa ya Mbeya (Mbeya Day) mwaka 1990.
Hata hivyo, Mulugo mwenyewe akizungumza na gazeti hili jijini Dar es Salaam alipuuza tuhuma hizo kwa kusema kuwa ni njama za kisiasa zinazofanywa na maadui zake. Mulugo anasema madai hayo yamekuwa yakitolewa mara kwa mara na amekuwa akiyajibu kwa kuwaonyesha vyeti vyake halali vya shule.
“Hayo madai ni ya muda mrefu, wewe sijui utakuwa mtu wa 20 kuuliza swali kama hilo. Mimi vyeti ninavyo na hata ukitaka ushahidi nitakuonyesha,” alisema Waziri Mulugo na kuongeza:
“Haya mambo kabla hata sijachaguliwa kuwa Mbunge, tulivyokuwa bado kwenye mchujo wa ndani, usiku wa manane watu walisambaza huu uvumi na nilivyoenda kwenye kikao nikatoa vyeti vyangu, wakaviona.”
Waliomfundisha
Baadhi ya walimu waliomfundisha Mulugo, watu waliofanya kazi naye pamoja na wakazi wa Kijiji cha Udinde alikozaliwa, maelezo yao yanathibitisha mabadiliko ya majina ya Mulugo kwa nyakati tofauti pia ngazi mbalimbali za kielimu.
Uchunguzi unabainisha kuwa baada ya kuhitimu kidato cha nne, alifaulu kwenda Shule ya Sekondari ya Wavulana, Songea ambako alisoma kati ya 1994 na 1996 akiendelea kutumia jina la Hamimu Mulugo.
Baada ya kuhitimu kidato cha sita, uchunguzi ulibaini kuwa Mulugo alirejea Mbeya na 1998 alilazimika kubadili tena jina pale alipotumia cheti cha mtu aitwaye Dickson Mulungu, kuombea kazi ya kufundisha katika Shule ya Sekondari ya Southern Highlands.
Habari zinasema Mulugo alichukua hatua hiyo ili kumshawishi mmiliki wa shule hiyo mfanyabiashara, Gulnoor Dossa (sasa ni marehemu), kumpa nafasi ya kufundisha shuleni hapo.
Chanzo: Mwananchi
CHID BENZ AANZA UGOMVI TENA AMPIGA NGWEA CLUB
Chid Benz
Rapper Chid Benz, amempiga Cow Bama
a,k,a Ngwea nje ya Ambassador Lounge ikiyoko Mkapa tower, posta, usiku
wa kuamkia leo.ugomvi huo ulitokea baada ya Chid
kumzingua Dully alipokua akiingia, ambapo
mwisho wake aliamua kuondoka. Alipoondoka Dully Ngwea akamuuliza
inakuaje unamzingua kubwa lao, ndipo Chid alipopaniki na kuanza kutoa
lugha chafu huku akitaka kutokumsikiliza Ngwea, inasemekana Ngwea
aliamua kukaa kimya lakini Chid aliendelea kungea kwa hasira na kusema
"ndio nimemzingua kwani yeye nani" na kumbadilikia Ngwea
Subscribe to:
Posts (Atom)