Saturday, March 16, 2013
BREAKING NEWZZZZZ .... Jeshi la Polisi Lapiga Marufuku Maandamano ya Chadema Leo, Latoa Sababu Za Kupiga Marufuku Maandamano

Kamanda wa Polisi wa kanda hiyo ACP, Charles Kenyela
---
Jeshi
la Polisi mkoani Dar es Salaam kanda ya Kinondoni limekataza
maandamano yaliyokuwa yamepangwa kufanyika tarehe 16 Machi 2013
yaliyokuwa yameiratibiwa na Mbunge wa Ubungo, John Mnyika yaliyolenga
kufika katika Wizara ya Maji ili kufikisha ujumbe kwa Waziri wa Maji,
Prof Maghembe kuhusu kero ya maji katika jimbo hilo ambayo
haijatatuliwa wala kupatiwa ufumbuzi kwa muda mrefu. Kamanda wa Polisi
wa kanda hiyo ACP, Charles Kenyela amesema endapo maandamano hayo
yatafanyika:
1. Upo wasiwasi wa kutokea kwa vurugu pale watakaposhindwa kufikia muafaka kuhusu hoja zao.
2. Amewasiliana na Ofisi ya Waziri husika na kufahamishwa kuwa haina taarifa rasmi za ujio wa maandamano hayo.
3. Barabara yatakakopita maandamano hayo ipo katika ujenzi na hivyo maandamano hayo yatazuia shughuli za mkandarasi kukamilisha kazi yake kwa wakati na kuisababishia Serikali hasara.
Credits: Lukaza Blog
RAIS KIKWETE ATUMA SALAMU KWA PAPA FRANCIS WA KWANZA
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete leo Ijumaa 15 Machi, 2013 mchana amemtumia salamu
za Pongezi Baba Mtakatifu Francis I kwa kuchaguliwa kwake kuwa Papa wa
kanisa Katoliki Duniani na Vatican.
“Kuchaguliwa
kwako ni ushuhuda tosha wa imani na heshima kubwa ambayo kanisa
Katoliki inayo kwako, historia yako na upendo wako wa kujali na
kuwapenda wanyonge, unyenyekevu ni sababu tosha ya kuwapa wakatoliki,
wasio wakatoliki na wasio wakristo pia kusherehekea uteuzi wako” Rais Kikwete amesema kwenye barua yake ya Pongezi kwa Papa Francis I.
Vatican
na Tanzania imekua na uhusiano wa muda mrefu na hivyo Rais Kikwete
amemhakikishia Papa Francis kuwa uhusiano huo utadumu na anatarajia
utaimarika zaidi chini ya uongozi mpya wa Papa Francis I
“Mwisho”
Imetolewa na:
Premi Kibanga
Mwandishi wa Habari wa Rais, Msaidizi,
IKULU
DAR ES SALAAM
15 March, 2013
Waziri Dkt. Mwakyembe abariki uzinduzi wa ‘Showroom’ mpya ya Magari ya Volkswagon ya Kampuni ya Alliance Autos.
Mkurugenzi
Mkuu wa Kampuni ya CFAO Motors Roddy Sharp (kulia) akiongozana
na Waziri wa Nchi Mh. Anne Ruth Herkes wa Wizara ya Uchumi na
Teknolojia ya Ujerumani (kushoto) baada ya kuupokea Ujumbe kutoka nchini
Ujerumani kunakotengenezwa magari aina ya Volks Wagon walipofika
kushuhudia uzinduzi wa showroom mpya ya Kampuni ya Alliance Autos
wauzaji wa magari ya Volkswagon. Kushoto ni Balozi wa Ujerumani nchini
Tanzania Mh. Klaus Peter Brandes aliyeambata na ugeni huo.
Waziri
wa Nchi Mh. Anne Ruth Herkes wa Wizara ya Uchumi na Teknolojia ya
Ujerumani akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika hafla
ya uzinduzi wa Showroom mpya ya magari ya Volkswagon ya Kampuni ya
Alliance Autos iliyopo Pugu/Nyerere road jijini Dar es Salaam. Kushoto
ni Msaidizi wa Mkurugenzi wa CFAO Motors Mama Maria Petro akipokea
wageni waalikwa.
Mgeni
rasmi Waziri wa Uchukuzi Mh. Dkt Harrison Mwakyembe akizungumza na
wageni waalikwa pamoja na ujumbe wa wafanya biashara kutoka Ujerumani
walioongozwa Balozi wa Ujerumani nchini Klaus –Peter Brandes katika
hafla ya kuzindua Showroom ya magari ya kampuni ya Alliance Autos
inayouza magari aina ya Volkswagon ambapo pamoja na mambo mengine
amepongeza hatua hiyo na kusema serikali iko bega kwa bega na wafanya
biashara wabunifu na pia kuuhakikishia ujumbe kutoka Ujerumani kuwa
serikali imeweka mazingira bora ya kuwekeza hivyo wasisite kujitokeza.
Thursday, March 14, 2013
Mchumba wa Bwana Misosi asema na yeye ya Moyoni baada ya Wema Sepetu Kunyoa nywele
MWIGIZAJI wa sinema za Kibongo, Tamrina Poshi ‘Amanda’ amefunguka kuwa katika maisha yake hakuna kitu anachokichukia kama kushikwa nywele.
Akipiga
stori na mwandishi wetu hivi karibuni, Amanda alibainisha kuwa kama
ingekuwa ni hiari yake basi angenyoa hata kipara ili asipate usumbufu wa
kwenda kushikwa nywele saluni.
DIAMOND ATANGAZA KUJENGA MSIKITI
Kwa mujibu wa staa huyo ambaye kwa sasa anaminya kimapenzi na
mtangazaji wa DTV, Penniel Mungilwa ‘Penny’, msikiti huo utakuwa
kumbukumbu yake kwa watakaoutumia kama sehemu ya kurudisha kwa…
SIKU chache baada ya kuwachefua Waislamu wenzake kwa kutimba kwenye Maulid na kuomba dua akiwa amevaa hereni na mkufu, msanii wa Bongo Fleva mpenda totoz, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ametangaza kujenga msikiti jijini Dar es Salaam, kwani ni jambo alilolipanga kwa muda mrefu.
Kwa mujibu wa staa huyo ambaye kwa sasa anaminya kimapenzi na mtangazaji wa DTV, Penniel Mungilwa ‘Penny’, msikiti huo utakuwa kumbukumbu yake kwa watakaoutumia kama sehemu ya kurudisha kwa jamii inayompa sapoti kubwa.
Diamond ambaye amemjengea mama yake, Sanura Kassim ‘Sandra’ nyumba ambayo hadi sasa imegharimu Sh. milioni 260 alifunguka: “Ninajitahidi sana kununua viwanja au vinyumba vidogovidogo maeneo tofauti. Nipo kwenye plan (mpango) ya kujenga msikiti japo sijapanga sehemu hasa hadi nipate eneo la kutosha.
“Nataka iwe kumbukumbu ili hata kesho na keshokutwa nikifa, vizazi vijavyo wawe wanaswali kwenye msikiti uliojengwa na Diamond.
“Kwa kufanya hivyo itanipa baraka kubwa sana na soon tu nina imani mwenyezi Mungu atanisaidia nijenge huo msikiti.”
Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.
Na Sifael Paul Global PublishersSIKU chache baada ya kuwachefua Waislamu wenzake kwa kutimba kwenye Maulid na kuomba dua akiwa amevaa hereni na mkufu, msanii wa Bongo Fleva mpenda totoz, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ametangaza kujenga msikiti jijini Dar es Salaam, kwani ni jambo alilolipanga kwa muda mrefu.
Kwa mujibu wa staa huyo ambaye kwa sasa anaminya kimapenzi na mtangazaji wa DTV, Penniel Mungilwa ‘Penny’, msikiti huo utakuwa kumbukumbu yake kwa watakaoutumia kama sehemu ya kurudisha kwa jamii inayompa sapoti kubwa.
Diamond ambaye amemjengea mama yake, Sanura Kassim ‘Sandra’ nyumba ambayo hadi sasa imegharimu Sh. milioni 260 alifunguka: “Ninajitahidi sana kununua viwanja au vinyumba vidogovidogo maeneo tofauti. Nipo kwenye plan (mpango) ya kujenga msikiti japo sijapanga sehemu hasa hadi nipate eneo la kutosha.
“Nataka iwe kumbukumbu ili hata kesho na keshokutwa nikifa, vizazi vijavyo wawe wanaswali kwenye msikiti uliojengwa na Diamond.
“Kwa kufanya hivyo itanipa baraka kubwa sana na soon tu nina imani mwenyezi Mungu atanisaidia nijenge huo msikiti.”
PAPA MPYA FRANCIS 1 AMEANZA KAZI
Papa mpya Francis Vatican
....akiwa pungia mkono waumini waliofika eneo hilo wakati wa kutangazwa kwake
Kazi ya kuchaguwa wasaidizi…
Papa Francis I (katikati) akiwa na Kardinali Santos Abril wa Hispania (kushoto) na Kardinali Agostino Vallini ambaye pia ni Kasisi Mkuu (Vicar General) wa Roma (kulia) wakiupungia umati leo asubuhi.
Papa Francis I akihutubia kwa mara ya kwanza baada ya kuchaguliwa.
Siku yake ya kwanza ofisini kama Papa mtakatifu wa kanisa Katoliki,
Papa Francis 1 tayari anaanza kazi. Papa anatarajiwa kuwateua
wafanyakazi wakuu watakaohudumu katika Vatican chini ya uongozi wake.
Ameanza siku yake kwa maombi ya kibinafsi katika hekalu ya mtakatifu
Maria Maggiore mjini Rome. Baadaye Papa atafanya misa ya sherehe katika
kanisa la Sistine.
Mwandishi wa BBC anasema kuwa uteuzi atakaofanya Papa Francis,
utatizamiwa kama ishara ya mageuzi katika uongozi uliozongwa na kashfa
nyingi na pia utaonyesha mwelekeo anaonuia kuchukua kwa kanisa hilo.
Baadaye wikendi ijayo, Papa mpya anatarajiwa kukutana na vyombo vya habari vya dunia katika mkutano maalum.
Na Jumapili, ataongoza misa yake ya kwanza kama papa. Hata hivyo yeye
mwenyewe atatawazwa rasmi kuwa Papa Francis 1, siku ya Jumanne.
Chanzo: BBC SWAHILI
Timuatimua yawakera wanafunzi vyuo vikuu
RAIS
Jakaya Kikwete ameombwa kuchukulia kwa uzito vitendo vya timuatimua
wanafunzi katika vyuo vikuu vya umma kutokana na wanafunzi hao kudai
haki wanazopaswa kuzipata wawapo vyuoni.
Msemaji
wa Umoja wa Wanafunzi waliofukuzwa katika Vyuo Vikuu nchini
(UUEST), Philipo Mwakibingwa, alitoa kauli hiyo jana wakati wa
uzinduzi wa umoja huo na kusema kuwa lengo kubwa la umoja huo ni
kutetea wanafunzi waliofukuzwa.
Alisema tangu miaka ya 2000 hadi sasa, suala hilo limezidi kukua
nchini, watawala wa vyuo vikuu ambao ni maprofesa na baadhi ya viongozi
waliopo serikalini kulichukulia kama mila na desturi.
Mwakibingwa
alisema wanafunzi hao wamekuwa wakifukuzwa kutokana na kutoa mawazo
mbadala, kuhoji mambo, kukosoa uovu uliopo na unaondelea kutendeka
ndani ya vyuo, hivyo na kutoa ushauri pale inapobidi kwa masilahi ya
taifa lao.
Akizungumzia
umoja huo, alisema wamefikia hatua ya kuunda umoja huo kutokana na
serikali pamoja na Bunge kushindwa kutatua matatizo yao na kuongeza
kuwa hali hiyo imesababishwa na taarifa potofu zilizotolewa na
watawala wa vyuo vikuu hivyo.
“Kwa
sababu watawala wa vyuo vikuu wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa
kututenganisha na jamii zetu, familia zetu, jamaa, viongozi wetu wa
kidini na asasi kwa taarifa za uongo kupitia vyombo vya habari, tumeona
suluhu ya maisha yetu ni kuungana. Muungano huu umeundwa kwa ajili ya
kutetea maisha yetu,” alisema Mwakibingwa.
CHADEMA yalisulubu Bunge
WANASHERIA
wameunga mkono msimamo wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)
na wale wa NCCR- Mageuzi kupinga hatua ya Ofisi ya Bunge kuliagiza
Jeshi la Polisi kuwakamata wabunge wake ili wakahojiwe.
Wakizungumza
mwanasheria mashuhuri hapa nchini na wakili wa kujitegemea, Mathew
Kakamba, alisema ni kinyume cha sheria na ni matumizi mabaya ya
madaraka kwa Ofisi ya Bunge kutumia polisi kuwakamata wabunge katika
masuala yanayolihusu Bunge.
Wanasheria
hao walitoa maoni yao kuhusiana na mvutano mkubwa wa kisheria
uliozuka baina ya CHADEMA na Ofisi ya Bunge ambayo imeagiza kukamatwa
kwa wabunge kadhaa wa upinzani ili wakahojiwe na Kamati ya Haki, Kinga
na Maadili ya Bunge, ambayo CHADEMA wanadai kuwa haipo.
Wakili
Kakamba katika maoni yake alisema ni makosa kisheria kutumia nguvu za
mhimili mwingine katika kuendesha masuala yanayohusu mhimili wa pili.
“Kuna
mgogoro unaojulikana kwa Watanzania karibu wote kuhusiana na vurugu
zilizotokea katika mkutano wa Bunge lililokwisha, na kuvunjwa kwa
kamati za kudumu za Bunge.
“Pamoja
na kuvunjwa kwa kamati hizo, bado kama sikosei, wajumbe wake
hawajateuliwa na kwa maana hiyo, kisheria utendaji wake haujaanza. Kwa
lugha nyingine, haziwezi kuitwa kamati rasmi kwa sababu hazina
wajumbe,” alisema Wakili Kakamba.
Kauli ya Wakili Kakamba imeungwa mkono na wakili mwingine, Aloyce
Komba, ambaye amekiita kitendo cha Ofisi ya Bunge kutumia polisi
kuwakamata wabunge wao wa upinzani kuwa ni udhalilishaji mkubwa na
uvunjaji wa haki za binadamu.
Komba
anayetoka Kampuni ya Uwakili ya Haki Kwanza, alisema Bunge ni chombo
kinachojitegemea na linazo sheria na kanuni zinazopaswa kutumika
kumlazimisha mbunge kutimiza agizo la wito.
“Masuala
yote ya Bunge yanatakiwa kuendeshwa kibunge bila kutegemea vyombo
vingine vya nje, labda tu ikiwa kuna mwingiliano kutoka katika mhimili
mwingine.
“Si sahihi kwa spika kutumia polisi kuwakamata wabunge wakati wanazo
kanuni na taratibu nzuri tu, na sidhani kama ni utaratibu mzuri na
unaolenga kudumisha demokrasia.
“Mbunge akishindwa kufika, kwani hakuna sheria nyingine hata za
kuzuiwa kuhudhuria vikao kadhaa vya Bunge, hadi leo wanataka kutumia
polisi kuwakamata?” alihoji Komba.
Akizungumzia
uhalali wa kamati hizo, Komba ambaye ni mtaalamu wa sheria katika
mambo ya utawala, alisema kimsingi hazipo, kwa sababu tangu kuvunjwa
kwake na kuundwa nyingine, bado spika hajateua wajumbe wa kamati mpya.
“Hajateua wajumbe wa kamati hizo, na ni sawa kabisa kuwa hazipo. Sasa
wanaitwa kuhojiwa na kamati gani? Mtazamo wa kisheria ni kwamba
hazipo.
Alikwenda
mbali zaidi na kuilaumu Ofisi ya Bunge kwa madai ya kuvunja haki za
msingi kwa sababu aliyetendewa kosa ni spika (kiti), anayelalamika ni
spika, mteuzi wa kamati ni spika na ushahidi mwingi utatoka kwa spika,
hivyo kupingana kabisa na haki za sheria ambazo mlalamikaji hapaswi
tena kuwa mwendesha mashitaka.
Hata hivyo, mawakili hao walikubaliana na kuwataka wabunge wote
waliopata barua za wito kutoka Ofisi ya Bunge kuitikia na si kukaidi.
“Pamoja na kasoro hizo, kama wameitwa na Ofisi ya Bunge, wanatakiwa
kwenda na si kugoma. Huko ndiko mahali pekee wanakotakiwa kuwakosoa hao
wakubwa, na hata wanao uwezo wa kukataa kuzungumza hata kama kamati
yenyewe ingekuwa hai kisheria,” walisema wanasheria hao.
CHADEMA wagoma
Juzi
Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa alimwagiza Mnadhimu wa
Kambi ya Upinzani Bungeni kuiandikia barua Ofisi ya Bunge ya kukataa
wabunge wake kukamatwa na polisi ama kuhojiwa na kamati waliyodai ni
hewa, kwa kuwa zilizokuwapo zilivunjwa na Spika Anne Makinda katika
kikao kilichoisha mwezi uliopita.
Akizungumza
jijini Dar es Salaam jana, Dk. Slaa alisema kisheria, kanuni na
taratibu za Bunge, kamati ambazo zimeshavunjwa haziwezi kufanya kazi
yoyote kwa kuwa ni batili mpaka hapo zitakapoundwa kamati nyingine.
Alilitaka
Bunge kurejea kanuni za kudumu za Bunge namba 113 (7), inayozungumzia
ukomo wa uhai wa kamati za Bunge, uhai wake unaishia Mkutano wa Kumi
wa Bunge ambapo inakuwa ni nusu ya kwanza ya uhai wa Bunge lenyewe.
Dk. Slaa alisema kutokana na kifungu hicho, inaonesha dhahiri kwamba
Spika Anne Makinda na wasaidizi wake wana matumizi mabaya ya sheria,
kutoifahamu vizuri ama kulewa madaraka, hali ambayo CHADEMA
haitakubaliana nao.
Hivyo
alisema Kamati ya Haki, Kinga na Maadili ya Bunge ambayo ilikuwa
chini ya Mbunge wa Mlalo, Brigedia mstaafu Hassan Ngwilizi (CCM),
haitawahoji wabunge wake kwa kuwa imekwisha kumaliza kazi yake tangu
Februari 8, mwaka huu.
Msimamo wa CHADEMA unakuja zikiwa ni siku mbili tangu Ofisi ya Bunge
kupitia Katibu Mkuu, Dk. Thomas Kashililah, itumie Jeshi la Polisi
kuwataarifu baadhi ya wabunge wa chama hicho kuwa wanahitajika jijini
Dar es Salaam kwa ajili ya mahojiano na kamati hiyo.
Katibu
Mkuu huyo alisema kama wabunge wa CHADEMA wanaitiwa kuhusu vurugu
zilizotokea bungeni Februari 4, mwaka huu, tayari zimeshatolewa hukumu
yake kwa kuwataja wahusika kuwa ni Tundu Lissu (Singida Mashariki),
John Mnyika (Ubungo), Paulina Gekul (Viti Maalumu) na Joshua Nassari (
Arumeru Mashariki).
Alisema
katika hukumu hiyo ambayo ilisomwa na Spika Makinda ilikuwa ya upande
mmoja wa kamati yenyewe iliyokaliwa na wabunge wa CCM ambao waliwaona
wabunge wa CHADEMA pekee ndio waliofanya vurugu huku ikishindwa
kuwaita wahusika kwa mahojiano.
Aidha, alisema hata kama kamati ya Brigedia Ngwilizi ingekuwa hai,
wabunge wake wasingeitii, kwa kuwa tayari imekwisha kuwahukumu.
Hata hivyo Dk. Slaa alitumia nafasi hiyo kumtaka Spika Makinda kwenda
kozi kwa ajili ya kujifunza sheria za kuongoza Bunge kutokana na
kushindwa kwake katika kipindi chote alichokalia kiti hicho.
“Nasikia Spika Makinda huwa anasema kuwa niwafundishe wabunge wangu
sheria, kanuni na taratibu za Bunge kwa kuwa nazifahamu vizuri, kwani
yeye na wanasheria wake wanafanya nini? Kupoka kwake sheria na
taratibu za bungeni ndizo zinazosababisha vurugu?” alihoji Dk. Slaa na
kuongeza:
“Nataka nimwambie kwamba wakati nipo bungeni, maspika waliokuwa
wakiongoza Bunge akiwamo Samuel Sitta walikuwa wakijua kuongoza, kwa
kufuata sheria na kanuni zake na ndiyo maana hakuna vurugu zilizokuwa
zikitokea na si yeye.”
Aidha, alisema maspika hao walikuwa wanajua kwamba mabunge yote ya
Afrika na yale ambayo Tanzania inaiga kutoka kwao yana sheria na
taratibu zinazowaruhusu kushangilia hata kuzomea kwa kutaja chama chao
na si hivi ambavyo Spika Makinda anavyofanya.
Lissu anena
Akizungumza
kwa niaba ya wenzake, Lissu alisema kwa mujibu wa sheria na kanuni za
Kamati ya Haki, Kinga na Maadili ya Bunge, zinamtaka Katibu Mkuu wa
Bunge Dk. Kashililah kuandika barua hizo kwa niaba ya Spika Makinda
lakini hakufanya hivyo.
Lakini pia Lissua alisema hata barua ya polisi (police message)
waliyopewa si taarifa tosha ya kujipeleka wao kuhojiwa bali walipaswa
kupelekewa taarifa ya kuitwa kwa ajili ya mahojiano na Bunge.
Kutokana na maelezo hayo Lissu alisema hakuna jambo lililofuatwa
kisheria, hivyo hakuna watakayemwona, na alidai kuwa tayari hukumu yao
ilishatolewa na Mwenyekiti wa kamati hiyo, Brigedia Ngwilizi Februari
8, mwaka huu.
WANYARWANDA WAKOMALIA NDOA YA UWOYA
KATIKA kile kilichoonekana ni kuikomalia ndoa ya msanii wa filamu Bongo
Irene Uwoya, baadhi ya wadau nchini Rwanda wameendelea kutambua kuwa
yeye ni mke halali wa msakata kabumbu, Hamad Ndikumana ‘Kataut’.
Hayo yalibainika hivi karibuni baada ya Uwoya, Vincent Kigosi ‘Ray’, Steven Jacob ‘JB’ na Amri Athuman ‘King Majuto’ kutua nchini humo kuhudhuria utoaji wa tuzo za filamu zilizopewa jina la Rwanda Movies Awards.
Wakiwa Rwanda, matangazo yaliyokuwa yakirushwa kupitia redio na televisheni yaliainisha kuwa Uwoya ni mke wa Ndikumana, kitendo kilichowashangaza wasanii hao.
Akizungumza na Amani hivi karibuni, mmoja wa wasanii aliyeomba hifadhi ya jina lake alisema, inavyoonekana Wanyarwanda wengi hawataki kuamini kuwa ndoa ya Uwoya na Ndiku haipo na ndiyo maana wameikomalia.
“Katika matangazo yaliyokuwa yakisikika katika redio na televisheni, jina lililokuwa linatajwa ni Oprah umugore wa Kataut, wakimaanisha Oprah mke wa Kataut.
“Jina la Oprah kwa Uwoya limekuwa maarufu nchini Rwanda kufuatia filamu ya Oprah on Sunday iliyowashirikisha yeye, Ray na marehemu Kanumba,” kilieleza chanzo hicho.
Chanzo Global Publishers
Hayo yalibainika hivi karibuni baada ya Uwoya, Vincent Kigosi ‘Ray’, Steven Jacob ‘JB’ na Amri Athuman ‘King Majuto’ kutua nchini humo kuhudhuria utoaji wa tuzo za filamu zilizopewa jina la Rwanda Movies Awards.
Wakiwa Rwanda, matangazo yaliyokuwa yakirushwa kupitia redio na televisheni yaliainisha kuwa Uwoya ni mke wa Ndikumana, kitendo kilichowashangaza wasanii hao.
Akizungumza na Amani hivi karibuni, mmoja wa wasanii aliyeomba hifadhi ya jina lake alisema, inavyoonekana Wanyarwanda wengi hawataki kuamini kuwa ndoa ya Uwoya na Ndiku haipo na ndiyo maana wameikomalia.
“Katika matangazo yaliyokuwa yakisikika katika redio na televisheni, jina lililokuwa linatajwa ni Oprah umugore wa Kataut, wakimaanisha Oprah mke wa Kataut.
“Jina la Oprah kwa Uwoya limekuwa maarufu nchini Rwanda kufuatia filamu ya Oprah on Sunday iliyowashirikisha yeye, Ray na marehemu Kanumba,” kilieleza chanzo hicho.
Chanzo Global Publishers
ADAIWA KUMCHINJA MPENZI WAKE KAMA KUKU
Na GlobalpublishersVILIO vilitawala Kata ya Nyahanga wilayani hapa wakati wa kuuaga mwili wa binti Jessica Elialinga (19) aliyeuawa kinyama kwa kuchinjwa kama kuku na mpenzi wake, Musa Petro (27) mkazi wa Shunu kwa sababu zinazodaiwa ni wivu wa kimapenzi.
Tukio hilo lililoibua simanzi kubwa kutokana na marehemu kuhitimu Kidato cha Nne katika Shule ya Sekondari ya Kata ya Nyihogo, Kahama mwaka jana, lilijiri saa 12:45 Februari 6, mwaka huu.
Kitendo hicho kilifanyika katika banda la mbuzi lililopo nyumbani kwa kijana huyo ambaye baada ya kutekeleza mauaji na yeye alifanya jaribio la kutaka kujitoa roho kwa kisu.
Akisimulia juu ya tukio hilo, rafiki wa karibu wa Musa ambaye aliomba hifadhi ya jina lake kwa ajili ya usalama, alisema wiki moja kabla ya tukio hilo, mtuhumiwa huyo alikuwa akiwatangazia jamaa zake kwamba ana dhamira ya kumuua binti huyo kufuatia kubaini kuwa anamsaliti kimapenzi.
“Unajua Musa anafanya kazi ya kuchuna ngozi za wanyama machinjio ya Wilaya ya Kahama, alitutangazia dhamira yake hiyo, lakini tulichukulia kauli yake kama mzaha.
“Alisema anataka kufanya hivyo kwa sababu amekuwa akitumia gharama kubwa kwa mpenzi wake huyo tangu walipoanza uhusiano, msichana akiwa kidato cha pili, lakini anatoka kimapenzi na mwanaume mwingine,” alisema rafiki huyo.
Hata hivyo, inadaiwa baada ya mtafaruku wa usaliti, wawili hao walipatana na kuendelea na mapenzi, lakini baada ya mwanafunzi huyo kuhitimu kidato cha nne alibadilika ambapo mwanaume alisikia kuwa tayari ana mwanaume mwingine kutoka jijini Mwanza ambaye walikubaliana kufunga pingu za maisha baada ya kumaliza masomo.
Inadaiwa siku chache kabla ya mauaji hayo, rafiki mmoja wa karibu wa mtuhumiwa alikutana na marehemu njiani na kumsimamisha kwa lengo la kumweleza kauli zenye kutishia maisha yake anazozitoa mpenzi wake, lakini binti huyo hakusimama kumsikiliza.
Baada ya Musa kudaiwa kufaulu kumchinja mpenzi wake huyo na yeye kujikata koromeo na kuanguka akiwa ameishiwa nguvu, kijana mchunga mbuzi ambaye wengi katika eneo hilo humchukulia kama kaka yake Jessica, ndiye aliyekuwa wa kwanza kumshuhudia Musa akiwa katika hali hiyo.
Alipomhoji kulikoni, hakupata jibu zaidi ya kushuhudia jitihada za mtuhumiwa huyo kufungua mlango wa chumbani mwake zikishindikana.
Kijana huyo alitoa taarifa kwa watu ambao walifika na kumchukua Musa na kumkimbiza hospitali ya wilaya kuokoa uhai wake.
Watu waliobaki nyumbani walifuatilia michirizi ya damu hadi kwenye zizi la mbuzi ambako walimkuta Jessica ameshafariki dunia baada ya kuchinjwa.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Everest Mangala alithibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo alisema mtuhumiwa anashikiliwa na Jeshi la Polisi wilayani Kahama katika Hospitali ya wilaya hiyo anakoendelea kupatiwa matibabu.
HII NDIO HISTORIA FUPI YA PAPA FRANCIS 1: JORGE MARIO BERGOGLIO
Francis (/ˈfrænsɨs/, /ˈfrɑːnsɨs/; Latin: Franciscus [franˈtʃiskus]; born Jorge Mario Bergoglio; 17 December 1936) is current pope of the Catholic Church. He serves as the 266th pope,
having been elected on 13 March 2013. In that role, he is both the
leader of the Catholic Church and sovereign ruler of the Vatican City
State.
A native of Buenos Aires, Bergoglio was ordained as a priest in 1969. From 1998 until 2013, he served as the Archbishop of Buenos Aires, and Pope John Paul II made him a cardinal in 2001. Elected as pope in 2013 following his predecessor Pope Benedict XVI's resignation, Bergoglio chose "Francis" as his name. This marked the first time in papal history that this name had been used, and along with Pope John Paul I is one of only two times since Pope Lando's brief 913 reign that a serving pope held a name unused by a predecessor. Francis is both the first Jesuit priest and the first native of the Americas to be elected Pope. He is also the first non-European pope since Syrian-born Pope Gregory III, who died in 741.
Jorge Mario Bergoglio was born in Buenos Aires, Argentina, one of the five children of Italian immigrants Mario José Bergoglio, a railway worker, and his wife, Regina María Sívori, a housewife. As a teenager Bergoglio had a lung removed as a result of an infection. He studied and received a master's degree in chemistry at the University of Buenos Aires before he decided to pursue an ecclesiastical career . According to another reference, he graduated from a technical school as a chemical technician, and at the age of 21 decided to become a priest.
Bergoglio entered the Society of Jesus on 11 March 1958 and studied to become a priest at the Jesuit seminary in Villa Devoto. In 1960 Bergoglio obtained a licentiate in philosophy from the Colegio Máximo San José in San Miguel; in 1964 and 1965 he taught literature and psychology at the Colegio de la Inmaculada, a high school in the province of Santa Fe, Argentina, and in 1966 he taught the same courses at the Colegio del Salvador in Buenos Aires.
In 1967, Bergoglio finished his theological studies and was ordained to the priesthood on 13 December 1969, by Archbishop Ramón José Castellano. He attended the Facultades de Filosofía y Teología de San Miguel (Philosophical and Theological Faculty of San Miguel), a seminary in San Miguel, Buenos Aires. Bergoglio attained the position of novice master there and became professor of theology.
The Society of Jesus promoted Bergoglio and he served as provincial for Argentina from 1973 to 1979. He was transferred in 1980 to become the rector of the seminary in San Miguel, and served in that capacity until 1986. He returned to Argentina to serve as confessor and spiritual director in Córdoba.
Kwa Kusoma Zaidi Juu ya Historia Fupi ya Papa Mpya Jorge Mario Bergoglio BOFYA HAPA
TGNP yashinda kesi ya Jengo Mahakama Kuu
Jengo lenyewe la TGNP
Usu Mallya
Mtandao
wa Jinsia Tanzania (TGNP),
walinunua jengo la ofisi hii kutoka kwa
Mfilisi wa iliyokuwa Tanzania Sewing Thread Manufacturers Limited (TSTML) yaani
Benki ya Rasilimali ya Tanzania mnamo tarehe 15th June, 1997.
Wapangaji wasiohalali walikwenda mahakamani
wakiwashitaki Benki ya Rasilimali ya Tanzania pamoja na TGNP na kesi
ilifunguliwa tarehe 16th July 1997 kesi ilipewa Na. 215/1997. Madai
ya washitaki yalikuwa yafutayo:
a)
TGNP ilipendelewa katika mchakato mzima wa tenda ya
manunuzi ya jengo hili na kwamba TGNP hawakuwa wazawa.
b)
Utoaji wa tenda kwa upande wa Beki ya Rasilimali
Tanzania ulikuwa batili kwa sababu haukufuata/haukuzingatia sheria ya nchi ya
manunuzi na hivyo kukiuka haki za kimsimgi (failure to observe the law, public
policy and the rules of natural justices)
TGNP kama washitakiwa
walishinda kesi hiyo ya madai namba
215/1997 iliyofunguliwa na waliokuwa wapangaji. Jengo lenye kesi ni jengo la
gorofa moja zilipo Ofisi za Makao Makuu ya Shirika Mabibo Dar es salaam.
Chini ya Mhe. Jaji T.B.
Mihayo, 15 Oktoba 2009, TGNP Ilishinda kesi hiyo na walalamikaji walidai kuwa
TGNP imependelewa. Oktoba 19, 2009, walifungua rufaa katika makahakama kuu ya
Rufaa ya Tanzania, wakiipinga hukumu ya kesi ya msngi namba 215/1997 na kukawa
na kesi ya rufaa namba 129/2009 ili pia waendelee kukaa kwenye jesngo hilo.
TGNP iliiomba mahakama
kufuta ombi la walalamikaji la kuendelea kuwa kwenye jengo ili shirika liweze
kufanya shughuli zake, kesi ambayo ilisikilizwa na majaji watatu waheshimiwa
jaji Msasali, jaji Msofe, na jaji Rutakanga Julai 22,2011.
Tarehe 23. 08.2011,
TGNP iliamua kwa mujibu wa sheria kuwatoa kwa nguvu wapangaji hao ambao kwa
muda wote wa zaidi ya miaka 10 wamekuwa wakifanya shughuli zao kwenye jengo la
TGNP bila kulipa kodi wala ruhusa yao, lakini siku chache baadaye walirudi.
Pamoja na ushindi walioupta TGNP bado waliendelea kuheshimu maamuzi ya mahakama
kutokana na shauri walilolipeleka mahakamani.
Mwaka 2012 walalamikaji walienda tena Mahakama Kuu
wakiomba kurekebisha majina ya watu waliosomewa hukumu kuwa watu wengine walio hukumiwa hawakuwa sehemu
ya kesi hii!! TGNP tuliona kuwa hii
ni mbinu tuu ya kuchelewesha kesi ambayo imekuwa ikitumika kwa miaka mingi. Jaji Mwaikugile aliikubali
hiyo barua akitaka wakaandike vizuri zaidi ili hoja yao isikilizwe. Kesi hii
imepangiwa kusikilizwa tena hapo tarehe 26 Februari 2013, lakini hadi tarehe
08.03.2013 hawakuwa wamewasilisha na leo tarehe 13.03.2013 jaji ametupilia
mbali ombi lao.
Kesi hii imekuwa ni changamoto kwa TGNP, huu ni
mwaka wa 16 tangu shirika linunue jengo hili.
Sote kwa pamoja
tunaamini katika haki na na rasilimali lazima zirudi kwa wananachi!
Imetolewa na:
Usu Mallya
Mkurugenzi Mtendaji
TGNP
Rais Kikwete akutana na Mkurugenzi Mkuu wa WIPO Dr. Francis Gurry Ikulu jijini Dar.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa
katika mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Haki Miliki Duniani
(The World Intellectual Property Organization –WIPO) Dr. Francis Gurry
(wa tatu kushoto) akiwa na ujumbe wake wakati alipomtembelea Ikulu
jijini Dar es Salaam jana.
Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la Haki Miliki Duniani (The World Intellectual Property
Organization –WIPO) Dr. Francis Gurry katika mazungumzo na Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete alipomtembelea
Ikulu jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Viwanda na Biashara Dr. Abdallah Kigoda (wa kwanza kushoto) na
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Bi.Joyce Mapunjo (katikati)
wakimsikiliza kwa makini Rais Dr. Kikwete wakati akizungumza na
Mkurugenzi Mkuu wa WIPO (hawapo pichani).
Baadhi ya Maafisa mbalimbali wa Ikulu jijini Dar es Salaam.
Mh.
Rais Dr. Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja na Mkurugenzi
Mkuu wa WIPO Dr. Francis Gurry aliyeambatana na Ujumbe wake. Wa pili
kushoto ni Waziri wa Viwanda na Biashara Dr. Abdallah Kigoda.
Rais
Dr. Jakaya Mrisho Kikwete akimwonyesha Mkurugenzi Mkuu wa WIPO Dr.
Francis Gurry mmoja ya mti wa Mwembe (haupo pichani) uliodumu kwa miaka
mingi Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais
Dr. Jakaya Mrisho Kikwete akimsindikiza mgeni wake Mkurugenzi Mkuu wa
WIPO Dr. Francis Gurry mara baada ya mazungumzo alipomtembelea Ikulu
jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Waziri wa Viwanda na Biashara Dr.
Abdallah Kigoda.
Rais Dr. Jayaka Mrisho Kikwete na Mkurugenzi Mkuu wa WIPO Dr. Francis Gurry. (Picha na Zainul Mzige wa Mo Blog).
Wednesday, March 13, 2013
CARDINAL JORGE MARIO BERGOGLIO ACHAGULIWA KUWA PAPA MPYA; KUTUMIA JINA LA PAPA FRANCIS
Hatimae Jopo la Makardinali 115 wa Kanisa
katoliki wamemchagua Kardinali wa Buenos
Aires kutoka Latin Amerika Jorge
Mario Bergoglio (68) kuwa kiongozi
mpya atakaye chukuwa nafasi ya Papa
Benedict aliyejiuzuli hivi karibuni.
Jorge Mario Bergoglio
ambaye ni Muagrgentina tayari amechagua jina la atakalo litumia
katikakipindi
chake cha Uongozi kuwa atatambulika kama Papa Francis.
Jopo
la Makardinali wamemchagua Cardinali kutoka Latin America Cardinal
Jorge Mario Bergoglio, kushika wadhifa mpya wa Papa
katika uchaguzi uliofanyika kwa mara ya
tano kwa kura zilizopugwa na Makadinali 115 waliokuwa wakikutana katika
kanisa
la Sistine Chapel huko Vatican , Roma.
Maelfu
ya watu walikuwa wamefurika katika eneo la la St. Peters huko Vatican
huku
mamilioni wengine wakishuhudia Papa huyo mpya akitangzawa mbele yao.
Subscribe to:
Comments (Atom)
























