Balozi Ombeni Sefue
Serikali
inapitia upya ulinzi wa viongozi wastaafu ili kuepuka fedheha
iliyotokana na vurugu alizofanyiwa Waziri Mkuu mstaafu, Jaji Joseph
Warioba hivi karibuni.
Mpango huo umeelezwa na Katibu Mkuu Kiongozi,
Balozi Ombeni Sefue mwishoni mwa wiki, akisema Serikali imekerwa na
kufedheheshwa kutokana na tukio hilo lililotokea wakati wa mdahalo wa
Katiba Inayopendekezwa katika Hoteli ya Blue Pearl, Dar es Salaam
Novemba 2, mwaka huu.
“Kimsingi tutakachokifanya ni kupitia upya mpango
wa ulinzi wa viongozi wote waliostaafu, japokuwa huwa tunafanya hivyo
mara kwa mara, lakini kwa hili la Mzee Warioba tunaliangalia kwa umakini
wake.
“Tumekerwa sana na tukio lile, halikutufurahisha
hata kidogo kama Serikali kwa kuwa limemvunjia heshima Mzee Warioba,
yule ni mzee wetu, anahitaji heshima, kwanza heshima yake na ulinzi.”
Kauli hiyo ya Sefue imekuja wakati mdahalo huo
uliovunjika baada ya Mzee Warioba kushambuliwa, ukiwa umetangazwa
kufanyika upya Jumapili Novemba 16, mwaka huu katika hoteli hiyohiyo.
Mjumbe wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba,
Humphrey Polepole alithibitisha jana kuandaliwa kwa mdahalo huo kuanzia
saa 9.00 alasiri siku hiyo. Asante
kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza
kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya
neno Jambo Tz