MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imetoa wito wa kuwaita
Mkrugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini (DCI), Mkuu
wa Jeshi la Polisi (IGP) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali
(AG) kufika
mahakamani kesho Jumatanoo, Machi 21 kujibu kesi ya kutomfikisha mahakamani
Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi (TSNP), Abdul Nondo.
Taarifa za
wito huo umetolewa na Wakili wa Mwanafunzi huyo wa Chuo Kikuu cha Dar es
salaam, Wakili Jebra Kambole ambaye ametoa taarifa hiyo fupi kupitia kwenye
ukurasa wake maalum wa Twitter.
Kambole
amesema “Wito umetolewa leo (jana Machi 19) Mahakama kuu mbele ya Jaji
Samejikwamba DCI, IGP na AG wanapaswa kufika mahakamani 21/03/2018 kujibu kesi
ya Abdul Nondo”.
Kambole
amesema washitakiwa katika kesi hiyo itakayosikilizwa Jumatano, ni IGP Simon
Sirro ameitwa kwa sababu yeye ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini hivyo vituo
vyote na polisi wapo chini yake lakini bado Nondo amekuwa hapatikani katika
vituo vya polisi.
Aidha,
amesema kuwa katika jalada lililofunguliwa leo, Mkurugenzi wa Upelelezi wa
Makosa ya Jinai (DCI), naye kahusishwa kwa sababu mara ya mwisho Nondo
alipokelewa na yeye alipofikishwa Dar es salaam kutoka Iringa na kwamba
alimchukua kama muathirika wa tukio la utekwaji na siyo mshtakiwa.
Hata hivyo
Kambole amesema ameshafanya jitihada nyingi za kutaka kuonana na mteja wake
lakini hadi sasa juhudi zake hazijafua dafu.
Abdul Nondo
anashikiliwa na Jeshi la Polisi tangu Machi 7, ambapo awali aliripotiwa kupotea
na kesho yake kujikuta Iringa.
Baadaye
alisafirishwa hadi Dar kwa ajili ya upelelezi zaidi. Kamanda wa Polisi Kanda
Maalumu ya Dar, Lazaro Mambosasa akizungumza na wanahabari alisema
wanamshikilia Nondo kwa ajilili ya upelelezi na watakapokamilisha watamfikisha
mahakamani.
Na GPL
No comments:
Post a Comment