Wednesday, January 18, 2017

ALIYETABIRI KIFO CHA MUGABE AKAMATWA....!!!

Mchungaji Patrick Mugadza 

Maafisa wa polisi nchini Zimbabwe wamemkamata na kumzuilia mhubiri aliyetabiri kwamba Rais Robert Mugabe atafariki mwezi Oktoba mwaka huu.

Mchungaji Patrick Mugadza alikamatwa akiwa mahakamani mjini Harare Jumatatu ambapo alikuwa ameenda kwa kesi nyingine dhidi yake, wakili wake Gift Mtisi ameambia wanahabari.
Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe.

Mchungaji huyo alikuwa anakabiliwa na mashtaka ya kuvalia bendera ya taifa. Like page yetu ya facebook ya Jambo Tz pia tufollow instagram @jambotz.
"Alikuwa amefika mahakamani kwa kesi hiyo polisi walipomkamata wakati wa mapumziko na kumfungulia mashtaka kwa sababu ya unabii huo," Bw Mtisi aliambia AFP.

"Awali alishtakiwa kwa kudunisha na kukosea heshima mamlaka ya rais lakini shtaka hilo likabadilishwa baadaye na kuwa kuwatusi watu wa asili fulani au dini fulani."

Mchungaji Mugadza, ambaye huhudumu katika mji wa Kariba kaskazini mwa nchi hiyo, aliandaa kikao na wanahabari wiki iliyopita ambapo alitabiri kwamba Mugabe angefariki Oktoba 17 mwaka huu.

Kumfanyia mzaha Rais Mugabe au kutoa unabii au ubashiri kumhusu ni jambo hatari nchini Zimbabwe. Nchini humo kuna sheria ambayo huharamisha "kudunisha mamlaka ya au kumtusi rais."

Mwaka 2015, Mugadza alikamatwa na kuzuiliwa kwa karibu mwezi mmoja baada ya kujitokeza hadharani na bango lililokuiwa na ujumbe uliomwambia Mugabe kwamba watu wamekuwa wakiteseka chini ya utawala wake.

Siku ya maadhimisho ya uhuru mwaka jana, alitoa mahubiri akiwa amejifungia kwenye boriti ya taa nje ya duka kubwa zaidi la kibiashara mjini Harare, akisema hiyo ilikuwa ishara ya raia kukandamizwa Zimbabwe.Kumekuwa na uvumi kuhusu afya yake na mara kwa mara husafiri mataifa ya Asia kwa matibabu.

Bw Mugabe amekataa kumtaja mrithi wake na chama chake cha ZANU-PF kimekuwa kikiyumbishwa na makundi ya watu wanaotaka kumrithi.

Mwishoni mwa mwaka uliopita, raia na wafuasi wa vyama vya upinzani waliandamana kupinga utawala wake. Like page yetu ya facebook ya Jambo Tz pia tufollow instagram @jambotz.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...