Saturday, August 13, 2016

MAALIM SEIF AMTEMBELEA MH. NDUGAI

Ujumbe wa Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad umemtembelea Spika wa Bunge, Job Ndugai nyumbani kwake Salasala Dar es Salaam kumjulia hali baada ya kutoka India alikokwenda kuchunguzwa afya yake.

Maalim Seif ambaye pia ni Makamu wa Kwanza Rais Mstaafu wa Serikali ya Zanzibar, ameambatana na Kaimu Mwenyekiti wa CUF, Severina Mwijage, Naibu Katibu Mkuu CUF Tanzania Bara, Magdalena Sakaya na Naibu Katibu Mkuu mstaafu, Julius Mtatiro.
 
Ndugai amemhakikishia Maalim Seif kuwa hali yake kiafya imeimarika sana.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...