Friday, June 24, 2016

MAOMBI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU 2016/2017

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu inapenda kutoa taarifa kwa Umma na wadau wake wote kuwa inatarajia kuanza kupokea maombi ya Mikopo kwa mwaka wa masomo 2016 /2017 kuanzia tarehe 27 Juni 2016 hadi tarehe 31 2016.

Katika kipindi hicho waombaji wa mikopo watarajiwa wanapaswa kusoma mwongozo wa utoaji mikopo na ruzuku (GUIDELINES AND CRITERIA FOR ISSUANCE OF STUDENTS’ LOANS AND GRANTS FOR THE 2016/2017 ACADEMIC YEAR) uliopo kwenye tovuti hii ya Bodi ili kufahamu sifa za mwombaji na taratibu kufuata kabla ya kuomba mikopo kwa njia ya mtandao.

Utoaji wa Mikopo unaongozwa na Sheria ya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya juu Na. 9 ya 2004 (kama ilivyorekebishwa) hususani vifungu vyake vya 16 na 17.
Kwa taarifa hii, waombaji wote wa mikopo wanatakiwa kusoma mwongozo huo kabla ya kujaza maombi ya mikopo na wazingatie kuwa tarehe ya mwisho ya kuomba mikopo ni Julai 31, 2016.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...