Tuesday, May 03, 2016

MTOTO WA MWAKA MMOJA AOKOLEWA AKIWA HAI KWENYE KIFUSI KENYA

Mtoto wa umri wa mwaka mmoja unusu amepatikana akiwa hai kwenye vifusi vya jengo lililoporomoka Ijumaa jijini Nairobi. Jengo hilo la ghorofa sita liliporomoka katika mtaa wa Huruma baada ya mvua kubwa kunyesha.

Kwa mujibu wa gazeti la Daily Nation, msichana huyo alitolewa kwenye vifusi mwendo wa saa kumi usiku na kukimbizwa hospitalini. Kamanda wa kitengo cha taifa cha kudhibiti majanga Pius Maasai anasema hali ya mtoto huyo ni thabiti, kwa mujibu wa gazeti hilo. Watu 22 wamethibitishwa kufariki na wengine karibu 90 hawajulikani walipo. 

Juhudi za uokoaji bado zinaendelea siku ya nne baada ya mkasa huo kutokea. Kufikia sasa, watu 136 wameokolewa. Polisi wanasema wamiliki wa jumba hilo, ambalo maafisa wa baraza la jiji wanasema halikufaa kuishi watu, wamekamatwa na wanazuiliwa na polisi. Taarifa zinasema watafikishwa mahakamani baadaye Jumanne. Tangaza biashara yako hapa. Pia like page yetu ya facebook Jambo Tz. tu-follow instagram @jambotz.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...