Saturday, May 14, 2016

KAGAME AKANA KUWASAIDIA WAASI WA BURUNDI


Rais wa Rwanda Paul Kagame

Rais wa Rwanda Paul Kagame amekana madai yaliotolewa na Umoja wa Mataifa kwamba taifa lake linaendelea kuwasaidia waasi katika nchi jirani ya Burundi.

Kagame amesema kuwa tatizo la Burundi linatoka ndani ya nchi hiyo, na sio nje. Burundi imekabiliwa na mgogoro mbaya wa kisiasa tangu rais Pierre Nkurunziza kuamua kupigania muhula mwengine mwaka uliopita.

Ni mwaka mmoja kamili tangu rais Nkurunziza kuepekua jaribio la mapinduzi. Rwanda ilikana madai kama hayo kuhusu kuwaunga mkono waasi katika ripoti ya awali ya Umoja wa Mataifa mnamo mwezi Februari.

Pia Kagame amekosoa wachapishaji wa ripoti hiyo ambayo inatarajiwa kuwasilishwa katika baraza la usalama la Umoja wa Mataifa baadaye,ikisema mda wake ungetumika vyema kuangazia matatizo yanayokumba mataifa badala ya kuyazidisha. 

Ripoti hiyo iliopatikana na chombo cha habari cha Reuters imeishtumu Rwanda kwa kutoa mafunzo pamoja na usaidizi wa kifedha kipindi chote cha mwaka 2016 kwa waasi wanaolenga kumuondoa madarakani rais Pierre Nkurunziza.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...