Thursday, February 19, 2015

HAYA NDIO MAJINA YA WAKUU WA WILAYA WAPYA, PAUL MAKONDA, SHABAN KISSU...!!!

http://jambotz8.blogspot.com/

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete  amefanya mabadiliko ya wakuu wa Wilaya ili kuboresha utendaji kazi.
Mabadiliko hayo yamezingatia kuwepo kwa nafasi wazi ishiri na saba (27) zilizotokana na:

a) Kufariki dunia Wakuu wa Wilaya 3;
b)Kupandishwa cheo Wakuu wa Wilaya 5 kuwa wakuu wa Wakuu wa Mikoa:
c)Kupangiwa Majukumu Mengine wakuu wa Wilaya 7; na
d)Kutengua uteuzi wa Wakuu Wawilaya wengine 12.

katika babadiliko hayo Rais Kikwete amewateua wakuu wapya wa Wilaya 27 kujaza nafasi hizo zilizo achwa wazi.
Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.


Aidha, Wakuu wa Wilaya siti na nne (64) wamebadilishwa vituo vyao vya kazi na Wakuu wa Wilaya arobaini na mbili (42) wameendelea kubaki katika vituo vyao vya sasa. 
Walio teuliwa ni pamoja na Zelothe Steven (Musoma), Mboni Muhita(Mufundi), Paul Makonda (Kinondoni), Shaabani Kissu (Kondoa)

SOMA MAGAZETI YA LEO FEBRUARI 19, 2015

.

.
.
Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

OBAMA: VITA DHIDI YA MAAGAIDI SI UISLAM

Rais Barack Obama wa Marekani
Rais Barack Obama ameliambia kongamano dhidi ya misimamo mikali ya kidini akisema kuwa kuwa wako kwenye vita si na Waislamu bali na magaidi waliouchafua Uislamu.
Bwana Obama amesema ni sharti dunia ikabiliane na itikadi zilizopindishwa na makundi kama Islamic State yanayochochea vita na kuwapa vijana mafundisho yenye misimamo mikali ya imani ya kidini .
Ameyasema hayo katika mkutano wa siku tatu unaofanyika mjini Washington ambapo amesema dunia inatakiwa kukabiliana na makundi ya aina hiyo.
Rais Obama ameeleza kuwa manung'uniko waliyonayo vijana lazima yashughulikiwe ili kuondokana na hisia za makundi yenye misimamo mikali ya kiitikadi. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

LIBYA YAOMBA KUONDOLEWA VIKWAZO

Afisa wa Libya katika kikao cha kimataifa
Serikali ya Libya inayotambuliwa kimataifa imeliomba Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuiondolea nchi hiyo vikwazo vya silaha ili kukabiliana na kuzorota kwa hali ya usalama nchini humo.
Akihutubia kikao cha dharura cha baraza hilo, waziri wa mambo ya nje wa Libya,Mohammed al-Dairi amesema hatua hiyo itaisaidia serikali ya Libya kujenga jeshi lake, ili kuwatokomeza Islamic State na makundi mengine ya wapiganaji.
Waziri huyo wa mambo ya nje wa Libya aliungwa mkono na waziri wa mambo ya nje wa Misri Sameh Shoukry, ambaye amesema jumuia ya kimataifa inatakiwa kuisaidia serikali ya Libya ili kuonyesha mamlaka yake nchini humo. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

REAL MADRID WANG'ARA LIGI YA MABINGWA

 Cristiano Ronaldo wa Real Madrid akishngilia bao lake katika mchezo wa ligi ya mabingwa kati ya Real Madrid na Schalke uliomalizika kwa Real Madrid kushinda 2-0 
 
Michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya, hatua ya kumi na sita bora, iliendelea Jumatano usiku kwa kuzikutanisha timu za FC Basel ya Uswisi na FC Porto ya Ureno katika mchezo ambao FC Basel ndio waliokuwa wenyeji na mchezo wa pili ukiwa kati ya wenyeji Schalke 04 ya Ujerumani dhidi ya mabingwa watetezi Real Madrid ya Hispania.
Tuanze na mchezo wa FC Basel dhidi ya FC Porto. Mpambano huo ulimalizika kwa matokeo ya sare ya bao 1-1. Wenyeji FC Basel ndio waliokuwa wa kwanza kujipatia goli katika dakika ya 11 likifungwa na Gonzalez ambalo lilidumu hadi kipindi cha pili, FC Porto waliposawazisha katika dakika ya 75 kwa mkwaju wa penalti iliyofungwa na Danilo baada ya mchezaji wa FC Basel Samuel Walter kuunawa.
Katika mchezo huo ambao ulitawaliwa kwa kiasi kikubwa na wageni, FC Porto wakimiliki kwa asilimia 63% huku wenyeji wakiwa na asilimia 37% ulimalizika kwa mwamuzi wa mchezo huo Clattenburg kuwaonya wachezaji tisa kwa kadi za njano, watano wakiwa ni wa FC Basel na wanne kutoka FC Porto. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

Sunday, February 01, 2015

SOMA MAGAZETI YA LEO FEBRUARI 01, 2015

.
.
.
Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...