Waziri wa Nishati na
Madini Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akitoa maelekezo kwa mtaalamu kutoka
kampuni ya Symbion iliyopewa kazi ya kujenga miundombinu ya umeme katika kijiji cha Nyamikoma kilichopo
wilayani Busega Bw. Steve Thomson
(kushoto)
Meneja wa Tanesco- Kanda
ya Ziwa Mhandisi Joyce Ngahyoma, akifafanua jambo mbele ya Waziri wa Nishati na
Madini Profesa Sospeter Muhongo na wananchi wa kijiji cha Nyamikoma wilayani Busega
(hawapo pichani)
Mkazi wa kata ya
Ijitu iliyopo wilayani Busega
ambaye jina lake halikupatikana mara moja akitoa hoja yake
mbele ya Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo ( wa pili kutoka
kushoto waliosimama mbele) mara Waziri
alipofanya ziara katika kijiji hicho na kusikiliza kero za wananchi
Diwani wa Kata ya
Ijitu iliyopo wilayani Busega Vumi Magoti akielezea kero za umeme katika kata yake mbele
ya Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo ( wa pili kutoka
kushoto), viongozi na wananchi (hawapo
pichani).
Waziri wa Nishati na
Madini Profesa Sospeter Muhongo akipokelewa na baadhi ya watendaji kutoka Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) Kanda ya
Ziwa na Nishati na Madini mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Mwanza. Profesa Muhongo
anafanya ziara katika mikoa ya Simiyu,
Tabora na Shinyanga lengo likiwa ni kukagua miradi ya umeme vijijini inayotekelezwa na Wakala wa
Nishati Vijijini (REA) kwa kushirikiana na Taneesco. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
Waziri wa Nishati na
Madini, Profesa Sospeter Muhongo akisaini kitabu cha wageni katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya
Busega kabla ya kuanza ziara katika wilaya hiyo ili kujionea utekelezaji
wa miradi ya umeme vijijini pamoja na
kuzungumza na wananchi.
Mkazi wa kijiji cha Ihale kilichopo wilayani Busega mkoani Simiyu ambaye jina lake halikupatikana mara moja
akiuliza maswali mbele ya Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter
Muhongo (kulia) na wananchi (hawapo
pichani) mara Waziri alipofanya
mazungumzo na wananchi wa kijiji hicho ili kusikiliza kero zao.
Waziri wa Nishati na
Madini Profesa Sospeter Muhongo akisisitiza jambo kwenye mkutano na
wananchi wa kata ya Ijitu iliyopo wilayani Busega
Waziri wa Nishati na
Madini Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akitoa maelekezo kwa Meneja wa Tanesco-
Kanda ya Ziwa Mhandisi Joyce Ngahyoma ( wa mwisho kushoto) ya kuitaka
Tanesco kuongeza kasi ya
usambazaji wa umeme vijijini.
Waziri wa Nishati na
Madini Profesa Sospeter Muhongo akisisitiza jambo katika mkutano wake na wananchi wa kijiji
cha Bushigwamala wilayani Busega (hawapo pichani)
Sehemu ya umati wa wananchi
wa kata ya Kalemala wilayani Busega waliojitokeza kwenye mkutano na Waziri wa
Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo wakifuatilia kwa makini hotuba yake. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
No comments:
Post a Comment