Friday, October 31, 2014

PINDA ATAKA TANZANIA ISITEGEMEE WAFADHILI



Waziri Mkuu wa Tanzania, Mizengo Pinda

Suala la baadhi ya wafadhili wa TZ kubana au kuchelewesha fedha walizoahidi kusaidi bajeti ya nchi linaendelea kuiumiza serikali.
Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Mizengo Pinda, amesema umefika wakati sasa kwa Tanzania kujitegemea kwa mapato ya ndani kwa asilimia 100 badala ya kuegemea kwa wahisani ambao amedai wanakuwa na maslahi yao katika kusaidia.
Hivi karibuni wahisani wamesitisha kutoa fedha hizo kuishinikiza Tanzania kuchukua hatua dhidi ya upotevu wa mabilioni ya fedha kutoka Benki Kuu ya Tanzania katika mazingira yanayodaiwa kuwa ya rushwa.
Kiongozi huyo mwandamizi wa serikali ya Tanzania ametoa kauli hiyo muda mfupi baada ya kurejea kutoka ziara ya ughaibuni ambako alihudhuria mikutano katika nchi mbali mbali akishughuli maswala kadhaa ikiwa ni pamoja na uwekezaji. Asante kwa kutembelea blog hii, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz


Japokuwa Waziri Mkuu Pinda hafafanua kwanini serikali haichukui hatua za haraka kukamilisha uchunguzi wa upotevu wa takriban dola milioni 120 kutoka Benki Kuu ya Tanzania katika mazingira yanayodaiwa kugubikwa na rushwa kubwa, amesema wahisani hao wasingeisumbua Tanzania kama ingekuwa inajitegemea asilimia 100 kutokana na mapato ya ndani ya nchi.
“Ukishakuwa tu ni mtu ambaye unaonekana wewe bila wao tabu, ndiyo shida inaanzia hapo.Ndiyo maana wakati mwingine inabidi kusema bwana sisi tujitahidi, TRA huyu huyu twende naye akiweza kuongeza zaidi kidogo basi tutamshukuru sana.
“First and foremost tumtumie yeye na tuone hiki kidogo tunachokipata kutoka TRA tunavyoweza kukutumia vizuri zaidi kutupunguzia matatizo yetu. Kama zikija hizo nyingine well and good lakini si option ambayo unasema inakupa faraja kubwa sana. Kwasababu anything jambo lolote likitokea wanabana tu, halafu matokeo yake inakuwa ovyo sana katika shughuli zenu za maendeleo,” alieleza Bw Pinda.
Ingawa kauli yake haitapunguza maumivu ya wananchi wanaosubiri huduma na utekelezaji wa miradi ambayo ilishapangwa, pia ni vigumu kufanikisha jambo analolisema kwa muda mfupi.
Waziri Mkuu Pinda alipoongea na BBC hivi karibuni alikiri kwamba madai hayo ya utoroshaji wa fedha ni jambo linaloitia doa serikali ya Tanzania.
Swala hilo linaonyesha kuiumiza kichwa serikali wakati hasa kutokana na shughuli nyingi za maendeleo kuchelewa au kukwama, huku ikijikuta ikiwa haina njia nyingine ya haraka kurekebisha hali ya mambo.
Hata hivyo Waziri wa Fedha na Uchumi, Saada Mkuya Salum, akizungumza Dar Es Salaam amesema baadhi ya wahisani wamekwishatoa fedha na mazungumzo yanaendelea na waliobaki.
Ripoti ya uchunguzi unaofanywa na Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za serikali ambayo imekuwa ikifanya kazi hiyo kwa miezi kadhaa inasubiriwa kwa hamu ili ibainike endapo kulikuwa na hila katika kuchomolewa fedha zilizokuwa zimewekwa kwenye akaunti maalum katika Benki Kuu ya Tanzania kusubiri usuluhishi wa swala la kibiashara umalizike. Asante kwa kutembelea blog hii, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...