Thursday, October 09, 2014

MDEE NA WENZAKE WAPATA DHAMANA



Halima Mdee na wenzake wakitoka mahakamani baada ya kuachiwa huru kwa dhamana leo.

Wafuasi wa Chadema wakijiandaa kuwapokea wanachama wao baada ya kuachiwa huru.

Halima akiwa na wanachama wa Chadema baada ya kuachiwa huru.

Halima akionesha ishara ya  Chadema

Halima Mdee akisalimiana na wanachama wake baada ya kuachiwa huru.
Wakili wa kujitegemea wa Chadema, Peter Kibatara, akizungumza na wanahabari. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz


Wafuasi wa Chadema wakionyesha bango lenye ujumbe wa kumpongeza mbunge wao.

Mdee akiwa juu ya gari akitoka nje ya mahakama.

Gari la wanachama wa Chadema likitoka katika mahakama.
Mbunge wa Kawe, Halima Mdee na wenzake 8 leo wamepata dhamana katika Mahakama ya Kisutu, Dar. Kesi yao kutajwa tena Oktoba 21, 2014.
Siku ya jana washtakiwa hao walipanda kizimbani mbele ya Hakimu Mkazi Kaluyenda na kusomewa mashtaka mawili na Wakili wa Serikali Mkuu, Kangola aliwataja washtakiwa kuwa ni Mbunge wa Kawe, Mdee, Rose Moshi, Penina Peter, Anna Linjewile, Mwanne Kassim, Sophia Fanuel, Edward Julius, Martha Mtiko na Beatus Mmari.
Mdee na wenzake hao wanashitakiwa kwa makosa mawili la kwanza washtakiwa wote wanadaiwa Oktoba 4 mwaka huu, Mtaa wa Ufipa wilayani Kinondoni, walikaidi amri ya Ofisa wa Polisi SP Emmanuel Tillf iliyowataka watawanyike.
Shtaka la pili washtakiwa wote wanadaiwa Oktoba, mwaka huu, maeneo ya mtaa wa ufipa jijini Dar es Salaam wakiwa na lengo moja walikusanyika kinyume na sheria wakitaka kwenda ofisi ya rais. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...