Saturday, August 23, 2014

SERIKALI YAOKOA ZAIDI YA MILIONI 40

Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba
Dar es Salaam. Serikali imeokoa zaidi ya Sh40 bilioni tangu ilipoanza kutumia mfumo mpya wa malipo kwa watumishi wake.
Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba alisema hayo jana, wakati akitoa ufafanuzi juu ya kuchelewa kwa malipo ya wafanyakazi wa baadhi ya taasisi za Serikali kwa mwezi uliopita.
“Niliagiza kuanza kwa mfumo mpya wa malipo kwa watumishi wote wa Serikali kuanzia mwaka huu wa fedha ili kubaini malipo hewa yaliyokuwa yakifanywa na wahasibu wasio waadilifu. Tangu mfumo huo uanze Julai, tayari tumeokoa zaidi ya Sh40 bilioni,” alisema Nchemba.
Serikali ilitangaza kuondokana na mfumo wa ‘malipo ya dirishani’ ambao ulikuwa unatoa fursa ya wizi wa fedha za umma kupitia mishahara iliyokuwa ikilipwa kwa wafanyakazi hewa wengi.
“Kuna mishahara mingi ilikuwa inalipwa kwa marehemu au wafanyakazi wasiokuwepo ambayo ilikuwa inawaneemesha baadhi ya watendaji wa idara. Tumeanza kwa kuziba mwanya huo ili kudhibiti upotevu wa fedha,” alisema naibu waziri huyo. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...