Thursday, April 17, 2014

ANGALIA UKAWA WALIVYOLISUSA BUNGE MAALUM LA KATIBA JANA

Wajumbe wa Bunge  Maalum la Katiba ambao wanaunga mkono mfumo wa  Serikali za tatu wakitoa katika Ukumbi wa Bunge leo mjini Dodoma baada ya kususia kikao


Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz  





Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz  

Wajumbe wa Bunge  Maalum la Katiba ambao wanaunga mkono mfumo wa  Serikali za tatu wakitoa katika Ukumbi wa Bunge leo mjini Dodoma baada ya kususia kikao
***********

Wajumbe karibu wote wa vyama vya upinzani wanaoshiriki Bunge Maalum la Katiba mjini Dodoma, wametoka nje ya kikao cha leo jioni, wakipinga kitendo cha Chama Cha Mapinduzi (CCM) chenye wajumbe wengi ndani ya bunge hilo, kuwaburuza.

 

Wakati akitoa mchango wake, Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba aliliambia Bunge kuwa wanashangazwa na kitendo cha CCM kutaka kutumia wingi wao, kutengeneza katiba ambayo hailingani na mawazo ya wananchi, kama yalivyowasilishwa na Tume ya Jaji Joseph Warioba.

 

Alisema kitendo kilichofanywa na Waziri wa Nchi, ofisi ya Waziri Mkuu, William Lukuvi, kwenda katika kanisa na kusema wanaotaka muundo wa serikali tatu wanataka kuifanya Zanzibar kuwa nchi ya kiislamu ni uchochezi unaoweza kuligawa taifa na hata kusababisha machafuko.

 
Alisema pia wanashangazwa na Rais Kikwete kupokea na kusaini rasimu hiyo, lakini akaja bungeni na kuipinga kwa nguvu kubwa. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz  

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...