Saturday, November 02, 2013

MASHABIKI SIMBA WATAKA WACHEZAJI WAKONGWE WARUDISHWE


mashabiki_wa_simba_wakifurahia_ushindii_dc4d7.jpg
MASHABIKI WA SIMBA 
Mashabiki Simba wamepiga kelele na kutala benchi lao la ufundi libadilike na kuwarudisha wachezaji wakongwe.
Zaidi ya mashabiki waliotuma ujumbe mfupi kupitia barua pepe na wale waliopiga simu ya mkononi ya SALEHJEMBE, wamemtaka Kocha Mkuu, Abdallah Kibadeni na wasaidizi wake kufikiria na kugeuza misimamo waliyonayo.
"Kweli Kibadeni anatuangusha, ni kocha mkongwe lakini anaonyesha hana msimamo, ninahisi anaburuzwa na watu wengine maana anatoa uamuzi ambao unaonyesha kuna chuki. Wakongwe warudishwe," alisema Mohammed Kassim.
Juma Mroki, Thomas Mapunda waliojitambulisha wanaishi Dar es Salaam na Songea, walisema wakongwe ndiyo tatizo la timu hiyo.
"Angalia tumeongoza hadi dakika ya 90, lakini tumeshindwa kujilinda. Uzoefu pia ni jambo muhimu, wakongwe wasidhalauriwe eti kwa kuwa tuna vijana."
Baadhi ya wachezaji wakongwe wa Simba ambao wameshushwa kikosi cha pili ni Henry Joseph na Ramadhani Chombo 'Redondo'.
Lakini mshambuliaji mwenye kasi, Haruna Chanongo, naye ameshushwa kikosi cha pili kwa kuwa tu alishindwa kucheza vizuri mechi moja dhidi ya Yanga!
Mashabiki Simba, jana walifanya vurugu baada ya timu yao kushindwa kulinda bao na Kagera wakasawazisha katika dakika za nyongeza.
Walifanya vurugu na kuvunja viti huku baadhi yao wakiumia baada ya askari polisi kupambana nao wakati wakijaribu kuzuia vurugu hizo.
Simba imekuwa ikisonga kwa mwendo wa kusuasua na kusababisha kuendelea kuporomoka na sasa iko katika nafasi ya nne baada ya Yanga walioshika usukani jana, Azam FC na Mbeya City.
Chanzo: salehjembe

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...