Sunday, November 17, 2013

HASSAN DILUNGA ATUA YANGA

dilunga a6713
SAA chache baada ya kufunguliwa kwa Dirisha Dogo la Usajili kwa msimu wa 2013/14, vinara wa Ligi Kuu ya Vodacom, Yanga jana walifanikiwa kumsajili kwa mkataba wa miaka mitatu kiungo Hassan Dilunga kutoka Ruvu Shooting ya Pwani.

Kwa mujibu wa kanuni, klabu za Ligi Kuu na Daraja la Kwanza zenye fursa ya kusajili wachezaji katika dirisha dogo ni zile ambazo hazijatumia nafasi zote 30 za wachezaji, usajili uliofunguliwa jana Novemba 15 na kutarajiwa kufungwa Desemba 15.

Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili wa klabu ya Yanga, Abdallah Bin Kleb, alisema jana kwamba usajili wa kiungo huyo ni utekelezaji wa maagizo ya Kocha Mkuu, Ernie Brandts, aliyoyaacha na benchi lake la ufundi kwa ajili ya kuboresha kikosi.

"Kocha aliacha mapendekezo ya usajili tuyafanyie kazi, la kwanza lilikuwa ni kuhakikisha tunampata Kaseja ili kuongeza nguvu miongoni mwa makipa, ambao tuliukamilisha mwishoni mwa wiki na sasa tumelimaliza la kiungo Hassan Dilunga," alisema Bin Kleb na kuongeza.

Kikubwa kuhakikisha kuwa, tunatekeleza maagizo yote yaliyo katika ripoti ya benchi la ufundi na kuyafanyia kazi ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kuboresha kikosi chetu kwa ajili ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu na michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Usajili wa Dilunga kiungo aliyeteuliwa kikosi cha timu ya taifa, 'Taifa Stars', inayojiandaa kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Harambee Stars, ametua Jangwani siku chache baada ya mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu walipomsajili mlinda mlango wa zamani wa Simba na Stars, Juma Kaseja, aliyekuwa hana timu tangu kumaliza mkataba wake na Wekundu wa Msimbazi.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...