Friday, October 18, 2013

RIPOTI YA MO IBRAHIM: RWANDA, TANZANIA ZINA UTAWALA BORA ZAIDI EAC

Kagame Kikwete2
Rais wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Kikwete (kushoto)  na Rais wa Rwanda, Mhe. Paul Kagame, nchi zao zimetajwa kuwa na utawala bora katika jumuiya ya Afrika mashariki
……………………………………………………………………………………………………………………………
Mahmoud Ahmad Arusha
Tasisi ya Mo Ibrahim juu ya Utawala Bora Afrika, imebaini nchi za Rwanda na Tanzania kuwa nchi zenye utawala bora zaidi katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kati ya nchi 52 za kiafrika.
Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa Jumatatu na taasisis ya Mo Ibrahim imesema Rwanda imepata wastani wa asilimia 57.8 ikiwa ni zaidi ya wastani wa kiafrika wa asilimia 51.6.
Hii inamaanisha kwamba nchi hiyo imeboresha utawala bora kwa zaidi ya asilimia 10.9 tangu mwaka 2000, ikiwa nafasi ya kwanza kwa nchi za Afrika mashariki ikifuatiwa na Tanzania iliyoshika nafasi ya 17 barani Afrika kwa kupata asilimia 56.9 huku Uganda ikiwa ya tatu ECA kwa kuwa ya 18 kwa kupata asilimia 56. Kenya imekuwa ya 21 na kushika nafasi ya nne kwa kupata asilimia 53.6 huku Burundi iliyopata asilimia 43.8 ikishika nafasi tano kwa EAC.
”Rwanda imekuwa ikifanya vizuri mwaka hadi mwaka tangu mwaka 2000, ikiwa ni maboresho makubwa zaidi katika nyanja ya Maendeleo ya Binadamu hususa ni katika sekta ya elimu na afya,” ripote ilisema.
Mauritania imeshika nafasi ya kwanza katika Afrika kwa kupata asilimia 82.9 ikifuatiwa na Botswana aliyopata asilimia 77.6 ambapo Cape Verde imeshika nafasi ya tatu kwa kupata asilimia 76.7. barani.
Ripoti hiyo imebaini kwamba asilimia 94 ya nchi za Afrika ikiwemo Rwanda watu wake wanaishi katika nchi ambazo zimeboresha kwa ujumla masuala ya utawala bora tangu mwaka 2000.
Asilimia sita ya watu wanaoishi kwenye nchi ambazo kiwango cha utawala bora kimeshuka tangu mwaka 2000 ni pamoja na nchi za Guinea-Bissau, Madagascar, Somalia, Libya na Mali.
Taasisi hiyo ya Mo Ibrahim pia hutoa tuzo kwa viongozi bora barani Afrika.Hata hivyo tuzo hiyo haijatolewa kwa mara ya nne sasa.
Tuzo hiyo hotolewa kwa kiongozi wa Afrika aliyechaguliwa kidemokrasia aliyeonesha kwa vitendo uongozi bora,kutumikia muhula wake wa uongozi na kuachia ngazi miaka mitatu iliyopita.
 JT/LC/NI

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...