Friday, October 18, 2013

MWANAFUNZI AUNGUZWA MAKALIO KISA KAPOTEZA MBUZI

Untitled 22
Mwanafunzi wa darasa la nne shule ya msingi Bukokwa,  Wilaya ya Sengerema  mkoani Mwanza Cristina John (13)  aliyeunguzwa na jiko la mkaa na dada yake Paulina John baada ya kupoteza Mbuzi aliyekuwa malishoni.
Untitled 33
Paulina John  aliyefanya unyama wa kumuunguza mdogo wake Cristina John bila huruma na hajachukuliwa hatua zozote za kisheria huku vyombo vya dola vipo na vinafanya kazi.(picha na Daniel Makaka, Sengerema).
Na. Daniel Makaka, Sengerema.
Mwanafunzi mmoja  aitwaye Cristina John  mwenye umri wa miaka 13, ambaye anasoma darasa la nne 4,  katika shule ya msingi Bukokwa iliyopo kata ya Nyakarilo wilayani Sengerema ameunguzwa  jiko lilokuwa na mkaa wa moto na dada yake.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Afisa mtendaji wa kijiji hicho Bwn. Timoth John  wakati akiongea na redio Sengerema hivi karibuni amesema kuwa, mtoto huyo ameunguzwa  na  jiko hilo lililokuwa na mkaa wa moto katika makalio yake ikiwemo sehemu zingine za mwili wake, kwakile kilichoelezwa kuwa  alipoteza mbuzi wakati akiwa amewapeleka malishoni.
 
Amefahamika kuwa tukio hilo limebainika baada ya  mtoto huyo kuomba msaada wa kupelekwa hospitalini kupatiwa matibabu, kutokana na  maumivu yaliyosababishwa na majeraha aliyoyapata.
 
Imeelezwa kuwa baada ya kutoa taarifa kwa wananchi wasamalia wema walimchukua na kumpeleka  katika zahanati ya kijiji hicho, na kupatiwa matibabu na baadaye taarifa hizo walizifikisha kwa Afisa mtendaji wa kijiji hicho, huku wakilaani kitendo hicho  kuwa ni cha kinyama na mhusika anapaswa kufikishwa katika vyombo vya dola.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...