Tuesday, October 29, 2013

MWIGAMBA AZIDI KUANIKA MADUDU YA CHADEMA


*Awaonya wanaomwita msaliti
*Dk. Slaa aibua mapya

MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba, aliyesimamishwa uongozi asema atakichafua chama hicho kama ataendelea kuitwa msaliti.

Hatua hiyo, imekuja baada ya Mwigamba kukiri hadharani kusambaza waraka unaowatuhumu viongozi wa chama hicho katika mtandao wa Jamii Forum (JF), akitumia jina la Maskini Mkulima. 
 
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Arusha jana, Mwigamba aliwaonya viongozi wa Chadema wanaomwita msaliti. 
 
Alisema kama wanataka awe msaliti, yupo tayari kumwaga mambo yote hadharani, tena kwa ushahidi usio na shaka hata kidogo.

Mwigamba, aliyejiunga na Chadema mwaka 2004, akiwa mwanachama wa kawaida, alisema akiwa makao makuu mjini Dar es Salaam kama mhasibu mkuu wa chama, ndipo alipoanza kutambua udhaifu mkubwa wa kiuongozi ndani ya chama chake.

“Niliondoka pale makao makuu kwa mizengwe, kiongozi mmoja mkubwa kabisa alinifukuza kazi kwa kunipigia simu, tena baada ya kuwasiliana na Mkurugenzi wa Fedha,Anthony Komu akiwa nje ya Dar es Salaam na kumwagiza anifukuze,” alisema Mwigamba.


Alisema kwa bahati mbaya, udhaifu huo umeshindwa kushughulikiwa na vikao rasmi vya chama, kwani yeyote anayejaribu kukosoa ama kuhoji iwe ndani ya vikao rasmi ama nje, hutangazwa kuwa ni msaliti.

Alisema kutokana na hali hiyo, ni wajumbe wachache ndani ya Chadema, hasa kwenye Kamati Kuu, ambao wanaweza kusimama kidete na kukosoa uongozi.

Aliwataja wajumbe hao, kuwa ni Dk. Kitila Mkumbo, Profesa Mwesiga Baregu, Mzee Shilungushela na marehemu Magadula Sherembi kabla hajafariki dunia.

Hata baada ya kuondolewa Aprili, mwaka jana, alirejea Arusha na hakuwahi kujitokeza kwenye vyombo vya habari ama mitandao kuzungumzia tatizo la viongozi na uongozi ndani ya chama.

“Matatizo yaliyomo ndani ya chama ambayo wanachama wa kawaida wanaokiamini chama na viongozi wake wangeyasikia, hakika wangeweza kukata tamaa.

“Nimefanya hivyo kwa mapenzi na kwa maslahi ya chama changu, sasa kama viongozi wenzangu wanataka niwe msaliti basi waniambie hata leo nimwage ambayo yote hadharani, tena kwa ushahidi usio na shaka hata kidogo.
RAI

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...