Friday, September 20, 2013

MANGULI KATIKA WIZI WA MTANDAO WAKAMATWA KATIKA OFISI ZA TIGO BUGURUNI HAWA HAPA NA JINSI WANAVYOIBA MTANDAONI

Mrembo huyu ni mmoja wa watuhumiwa wa kesi hii ya wizi wa mtandao baada ya kutumia kitambulisho chake na  kutaka kuja kurudisha line ambayo sio yake kwa kuahidiwa kupewa pesa kidogo kama ujira wake na katika melezo yake akasema hawatambui wahusika wenzake kwani amekutana nao tu sinza na wakampa dili hilo na kuamua kuchukua bajaji ambao iliwaleta mpaka ofisi za tigo buguruni rozana 
Huyu ndio staring mwenyewe aliyechonga mchongo wote na kumshawishi huyu mwanamke kutumia kitambuluisho chake kufanyia wizi huo wa kimtandao
Mrembo akijitetea kuwa hahusiki kabisa katika wizi huu na pia kujitetea kuwa kaacha mtoto mdogo nyumbani 
Hapa akitoa maelezo kuwa yeye si mwizi  na hawafahamu kabisa wahusika wenzake na yeye ni mfanyabiashara wa vipodozi
Watuhumiwa wenzake wakificha sura zao huku wakitoa maelezo kwa wafanyakazi wa tigo na walinzi waliowatia chini ya ulinzi baaada ya kuweka mtego mzuri wa kuyanasa mataperli haya ya kimtandao 
Hiki ndicho kitambulisho alichokitaka kutumia huyu mwanamke kuswap line ambayo sio yake lakini aliweka jina la mhusika wa line na namba alizokuwa anapiga mara nyingi lakini sura yake bahati mbaya kwa umakini wa mfanyakazi mmoja wa tigo kwa jina Octavian Rweyendera alifanikiwa kubaini udanganyifu huo na kuamuru awekwe chini ya ulinzi  mara moja 
Aliyesimama hapo yeye alibiwa kiasi cha milioni moja kwa njia ya sim banking ya NMB baada ya line kuharibika ghafla kumbe mmoja wa watuhumiwa alirenew na kuiba pesa 
Hiki pia ni kitambulisho  cha mteja huyo hapo juu  aliyeibiwa pesa kwenye acount yake ya NMB kiasi cha milioni moja kwa njia ya sim banking baada ya mmoja wa hawa watuhumiwa  kuja kurudisha laini yake kwa kutumia kitambulisho hiki ambacho kimetengenezwa kwani si halisi na hatimaye kufanikiwa kuiba pesa kwa sim banking baadae 
Hapa mtuhumiiwa mmoja akiwa amejilaza chini kwa kugoma kutoa maelezo kwa walinzi waliowaweka chini ya ulinzi 
Hapa huyu binti akilia kwa uchungu na kuomba asamehewe
Wakiwa ndani ya gari ya polisi kuelekea kituo cha polisi Buguruni
Umati wa watu uliofurika kushuhudia tukio hilo la aina yake 
Mmoja ya wafanyakazi mahiri wa tigo Bw Octavian Rweyendera ambaye alifanikisha kukamatwa kwa watuhumiwa hao akitoa maelezo kwa baadhi ya maafande wa polisi jinsi watuhumiwa walivyotaka kufanya wizi huo wa kimtandao 
Askari polisi wakisikiliza kwa makini jinsi watuhumiwa hao walivyokamatwa
                    PICHA NA HABARI NA MWANAHARAKATI MZALENDO BLOG

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...